Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Sunday, July 30, 2017
no image

Tetemeko dogo la ardhi limetokea karegwe Kagera.soma zaid


Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano
limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika
Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani
Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa
kutokea.
Ofisa wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Gabriel
Mbogani amesema ili kupata uhakika wa
tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye
mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa
wapo makini baada ya kupatiwa semina kutokana
na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo
lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa
na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko
wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo
kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema
Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea
kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda
gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa
kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye
kuwa kubwa.
Mkazi wa mji mdogo wa Kayanga, Elieth Kikaka
amesema alitoka nje ya nyumba baada ya
tetemeko hilo kwa kuwa yamekuwa yakitokea
mara kwa mara mkoani Kagera hivyo linapotokea
ni lazima kuchukua tahadhari.
Mwisho

Friday, July 28, 2017
Kigogo uhamiaji asimamishwa kazi leo .soma zaid

Kigogo uhamiaji asimamishwa kazi leo .soma zaid


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesimamisha
kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji-Makao Makuu,
Grace Hokororo kwa kosa la kuwapatia vibali vya

no image

Kaimu Rais wa TFF wallece Karia anahojiwa na uhamiaji kuhusu uraia wake.

MENEJA Miradi ya Maendeleo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa Afrika, Mzimbabwe Solomon Mudege amewasili nchini jana usiku kwa ajili ya kufuatilia kinachoendela kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Bin Zubeiry Sports – Online inafahamu Mudege tayari yupo nchini na pamoja na kukutana na Kamati ya Utendaji ya TFF kesho Dar es Salaam, pia atakuwa na kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisons Mwakyembe. Bado haijafahamika Ofisa huyo amekuja kwa sababu zipi haswa na kama ameitwa na viongozi wa TFF au amekuja kwa maagizo ya FIFA tu. Lakini inafahamika hamkani si shwari kwa sasa katika soka ya Tanzania, kufuatia viongozi wakuu wawili wa TFF, Rais Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa kuwekwa rumande tangu Juni 29 kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. Malinzi, Mwesigwa pamoja na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawafo Mwanga walipelekwa rumande Juni 29 baada ya kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam. Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga. Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani. Lakini baada ya kesi hii kuanza kuunguruma na kuwekwa rumande, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo. Lakini kwa mwenendo wa kesi, Malinzi ndiyo kama amekwishaaga TFF, kwani uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma naye hajashiriki usaili wa wagombea, hivyo haruhusiwi tena kugombea. Karia naye yupo hatarini kuenguliwa katika uchaguzi baada ya kuitwa Idara ya Uhamiaji ya Taifa kuthibitisha uraia wake, akidaiwa kuwa ni raia wa Somalia. Mwenyewe amekiri kuwa na asili ya Somalia, lakini amekataa kuwa si Mtanzania. Uhamiaji inaendelea na uchunguzi dhidi yake.
Thursday, July 27, 2017
Habari mpya.kampuni ya BarrickCold imetangaza kuwa itaanza mazungumzo na serikali kuhusu makinikia wiki ijayo.soma zaid

Habari mpya.kampuni ya BarrickCold imetangaza kuwa itaanza mazungumzo na serikali kuhusu makinikia wiki ijayo.soma zaid

HABARI MPYA: Kampuni ya Barrick Gold
imetangaza kuwa itaanza mazungumzo na
Serikali ya Tanzania kuhusu makinikia wiki ijayo.
# Mwananchileo

Wahenga hawa wametiimiza amri ya mungu kwa kuoana licha ya umri wao kuwa mkubwa. soma zaid

Wahenga hawa wametiimiza amri ya mungu kwa kuoana licha ya umri wao kuwa mkubwa. soma zaid

Wahenga walisema "Akipenda chongo huita
kengeza", huko nchini Uingereza, Mzee mmoja
aliyefahamika kwa jina la Bernard mwenye miaka
93 ameoa Bibi (Ajuza) wa miaka 95, Bibi
Margaret na Bernard walijuana walipokuwa
vijana, lakini wakakutana tena miaka sita iliyopita
katika mazishi ya marehemu mkewe Bernard.
Taarifa zinasema mkewe Bernard (marehemu)
alikuwa rafiki wa mkubwa wa Bibi Margaret.

Mahakama ya Kisutu leo imempa dhamana Tundu Lisu.soma zaid

Mahakama ya Kisutu leo imempa dhamana Tundu Lisu.soma zaid


Mahakama ya Kisutu leo 27/7/2017 mida ya saa
mbili na nusu asubuhi 
IMEMPA HAKI YA DHAMANA Mh Tundu Lissu
kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja
atakayesaini dhamana ya thamani ya milioni
kumi

Wednesday, July 26, 2017
no image

Tafiti zinaonesha mwanaume aliye adhirika HIV anawahi kufa kuliko mwanamke aliyeadhirika ma HIV.soma zaid

Tafiti zinaonesha Wanaune waliothilika na HIV wanawahi kufa mapema kuliko wanawake walioadhirika na HIV.hayo yameelizwa na Elizabeti kupitia clouds media kwenye bawerbreak fast.

Wanaume wanao teswa na wake zao mkoani Lindi wapewa ofa.soma zaid

Wanaume wanao teswa na wake zao mkoani Lindi wapewa ofa.soma zaid

Na. Ahmad Mmow, Lindi. JAPOKUWA shirika lisilo la kiserikali la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto mkoani Lindi (LIWOPAC) limejikita katika kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto. Hata hivyo limetoa wito kwa wanaume waishio mkoani humu wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na wakezao waende wapewe msaada wa kisheria. Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa shirika hilo, Cosma Bulu, wakati wa kongomano la wasaidizi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria waliopo katika halmashauri za mkoa wa Lindi, lililofanyika mjini Nachingwea. Bulu alisema ingawa shirika lake limejikita limejikita zaidi katika kuwasaidia wanawake na watoto, lakini limeona kunaumuhimu mkubwa wa kuwasaidia hata wanaume wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na wake zao. Huku akibainisha kuwa wanaume wanaofanyiwa vitendo vya kikatili wapo. Bali wengi wao wanaona aibu kwenda kuwashitaki wake zao. Japokuwa kisheria zilizopo zinatakiwa kutumiwa na watu wa jinsia zote. "Sisi tunafahamu kuwa wapo wanawake wenzetu wanawanyanyasa , wanatesa na kuwafanyia ukatili. Lakini kutokana na tabia ya mfumo dume wanaona aibu kuja kuomba msaada ili wasaidiwe. Wanaona aibu," alisema Bulu. Mkurugenzi huyo alisisitiza kwa kusema sheria zilizopo hazipo kwa ajili ya jinsia fulani,bali zote. Hivyo hata wanaume wanasitahili kusaidiwa. Ingawa waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi ni akinamana na watoto. Alibainisha kwamba wao kama watoaji wa msaada na watetezi hawana ubaguzi katika kutoa msaada kwa mtu anae hitaji msaada wao. "Sasa tukisema hatuwasaidii wanaume sidhani kama itakuwa sawa. Tena hawa wenzetu hawana chama wala umoja wa kutetea wanaume. Sio kama hawaonewi ila hawasemi, kuna wanawake ni wababe kwelikweli," alisisitiza na kusababisha washiriki kuangusha vicheko. Bulu alibainisha kuwa hawana uwezo wa kumfingulia mtu mashitaka, bali jukumu lao ni kutoa msaada wa kisheria. Hasa kwa wanawake na watoto. Lakini pia kutoa elimu ili jamii iweze kuzitambua na kudai haki za msingi za binadamu. Msaada ambao unatolewa bure bila malipo. Aidha mkurugenzi huyo alitoa wito kwa jamii kujenga tabia ya kuitafutia ufumbuzi na kumaliza migogoro yake badala ya kutegemea na kukimbilia mahakamani na kwenye mabaraza katika mambo ambayo yanaweza kusuluhishwa na jamii yenyewe kupitia vikao vya familia na ukoo. "Sasa hakuna moto wa jioni, muda wa kukutana na kukumbushana maadili mema hakuna, ndio sababu hata uadilifu umepungua miongoni mwa jamii," alisema Bulu. Kongamano hilo la siku mbili lililofadhiliwa na Taasisi ya huduma za uwezeshaji kisheria (LSF) lengo lake kuu ni kuimarisha upatakanaji wa haki katika jamii. Hasa kwa wanawake na watoto kwa kuongeza ubora na uwezo wa utoaji huduma za msaada wa kisheria. Ambapo mradi huo unatambulika kama mradi wa kuboresha huduma za upatakanaji wa huduma za kisheria. Ulioanza mwaka jana na unatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.
Tuesday, July 25, 2017
Mashindano ya mbio za Baiskeli mkoani Simiyu.soma zaid

Mashindano ya mbio za Baiskeli mkoani Simiyu.soma zaid

Mashindano ya Mbio za Baiskeli katika Mikoa mitano ya Kanda ya ziwa yanataraji kufanyika AGOSTI 6, 2017 katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu. Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya uzalishaji wa Vinywaji Baridi ya JAMBO FOOD PRODUCT kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mashindano hayo yatahusisha Umbali wa Kilomita 200 kwa Wanaume, Kilomita 80 kwa Wanawake na Kilomita 5 kwa watu wenye Ulemavu. Pia kutakuwa na Burudani Mbalimbali Kutoka kwa WAGIKA na WAGARO na Ngoma nyingine nyingi za Asili zitatolewa siku hiyo. Zawadi Mbalimbali zitatolewa kwa washiriki ikiwemo Pikipiki na fedha Taslimu zaidi ya Shilingi Milioni nane.
Wednesday, July 19, 2017
Thaban Kamsoko amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu ya Yanga.soma zaid

Thaban Kamsoko amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu ya Yanga.soma zaid

Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba mpya wa
miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban
Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti
Boys, Ramadhani Kabwili.
Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba
Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya
kufikia makubaliano ya mambo kadhaa.
Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya
usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti
Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka
huu nchini Gabon.
Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa
nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha
kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki
Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim
Ajib.

Saturday, July 15, 2017
no image

TANZIA#Wazir Harrison Mwakyembe amefiwa na mke yake Bi.Lina George.soma zaid

Waziri wa habari, utamaduni na michezo
ndugu Harrison Mwakyembe amefiwa na
mkewe aliyekuwa anaumwa kwa muda
mrefu.
Mke wa Waziri Dk Mwakyembe Bi. Linah
Mwakyembe, amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo (Julai 16) katika Hospitali ya
Agha Khani alipokuwa akitibiwa.

Friday, July 14, 2017
Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi.soma zaid

Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi.soma zaid

Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo. Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio. Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo, amesema tatizo la machangudoa kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo limekuwa kero nyakati za usiku pamoja na vijana wanaofanya uhalifu pia wamesababisha watu kuwa na hofu ya usalama wao. Mkazi wa kata hiyo, Mary William, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo. Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa jambo hilo. “Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi. Akijibu kero za wananchi hao kuhusu kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo. Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni. Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael, amesema suala lao limeshapitishwa bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili. Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.
Klabu ya Dar Yanga Afrika imempata msemaji mpya wa klabu( Dismas Ten).soma zaid

Klabu ya Dar Yanga Afrika imempata msemaji mpya wa klabu( Dismas Ten).soma zaid

semaji mpya wa Yanga Dismas Ten.
Klabu ya Yanga leo imemtangaza rasmi
aliyekuwa afisa habari wa klabu ya soka ya
Mbeya City Bwana Dismas Ten kama afisa habari
wao baada ya kuingia nae mkataba leo.
Dismas anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
aliyekuwa afisa habari wa klabu hiyo Jerry Murro
ambaye mwaka jana 09 Julai 2016 alifungiwa na
Shirikisho la soka nchini kujihusisha na soka.
Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Godlisten
Anderson Chicharito kama kaimu afisa habari
ambaye sasa ataendelea na nafasi hiyo chini ya
Dismas Ten.
“Tumeamua kuleta mapinduzi kwenye utoaji
habari kwenye klabu yetu na naamini kwa
muunganiko huu wa Dismas na Chicharito klabu
yetu itafanikiwa sana kupitia kitengo iki cha
Habari na mawasiliano kama vilabu vingine
vikubwa duniani.”-Boniface Mkwasa Katibu Mkuu
Yanga SC.

Waziri wa habar Dkt.Harrisob Mwakiembe ameunda tume hii.soma zaid

Waziri wa habar Dkt.Harrisob Mwakiembe ameunda tume hii.soma zaid


Waziri wa Habari Dkt Harrison
Mwakyembe punde atazungumza
Waziri Mwakyembe: Serikali hairidhishwi
na kampuni ya ubia kati ya TBC na Star
Times hasa kuzalisha hasara kila mwaka.
Waziri Mwakyembe: Nimekutana leo na
Mwenyekiti wa Star Times Bwana Pang
kujadili mkataba huu ili kufanya uamuzi
mwezi huu huu
Waziri Mwakyembe: Nimeunda Timu ya
Wataalamu kufanyakazi kwa siku saba
kutupa mrejesho ili kuamua kama
tunaboresha ubia huu ama la.
Mwenyekiti Star Times amemshukuru Rais
Magufuli kwa nia ya kutaka mkataba uwe
wa mafanikio zaidi.Yeye yuko tayari
kurekebisha kasoro zozote.

Rais wa Uganda Yoweri Mseveni kuongoza hadi kifo.soma zaid

Rais wa Uganda Yoweri Mseveni kuongoza hadi kifo.soma zaid

# Habari:Spika wa Bunge la Uganda Rebecca
Kadaaga amesitisha mjadala kuhusu jaribio la
kutaka katiba ya taifa kufanyiwa marekebisho na
kuondoa kizuizi cha umri kwa wanao wania Urais
na hatimaye amevunja ukimya na kumruhusu
Rais wa sasa Yoweri Museven kuongoza hadi
kifo.
Wabunge nchini humo wameapa kutomheshimu
spika na badala yake kuendeleza mjadala huo.chanzo radio one sterio.

Club ya Simba imemteua Dkt.Anord Kashembe kuwa katibu mkuu mpya.soma zaid

Club ya Simba imemteua Dkt.Anord Kashembe kuwa katibu mkuu mpya.soma zaid


# Habari:Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba
imemteua Dkt. Arnold Kashembe kuwa katibu
Mkuu mpya wa klabu hiyo.

Monday, July 10, 2017
KIBITI:Mtu mmoja ahofiwa kuuawa kwa risasi mke wake amejeruhiwa usiku wa kuamkia leo.

KIBITI:Mtu mmoja ahofiwa kuuawa kwa risasi mke wake amejeruhiwa usiku wa kuamkia leo.

Kibiti. Watu wasiojulikana wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia leo. Kadhalika watu hao walimjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu. Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi amethibitisha kufikishwa hospitalini hapo kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya kupigwa risasi na kusema kwa sasa yupo katika chumba cha matibabu ya dharura. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema tayari polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.chsnzo muungwana blog

KISUTU,DAR: Mbunge Halima Mdee amefikishwa Mahakamani leo.soma zaid

KISUTU,DAR: Mbunge Halima Mdee amefikishwa Mahakamani leo.soma zaid

Halima Mdee aliyekaa akisalimiana na
Esther Bulaya
Mbunge wa Kawe Halima Mdee, hatimaye
amefikishwa Mahakamani Kisutu Dar es
Salaam.
Bado sijajua atashitakiwa kwa makosa
yapi kwani ndo yupo Kisutu.
Hapo awali Mdee aliwekwa Korokoroni
Oysterbay Polisi kwa amri ya Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi. Hata baada
ya Masaa 48 kuisha, hakuachiliwa huru
kwani aliendelea kushikiliwa.
Halima Mdee(Mb, CHADEMA) akamatwa
na Polisi. Apelekwa Oysterbay...

William Ngereja amerejesha 40.4 milion alizochota Escrow.soma zaid

William Ngereja amerejesha 40.4 milion alizochota Escrow.soma zaid


Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na
Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William
Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha
alizozipokea kutoka kwa James
Rugemalira mnamo tarehe 12/2/2014
katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi
cha Shilingi Milioni 40.4 ili kukwepa
kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo.
Ngeleja amesema kuwa alipokea Fedha
hizo bila kujua kwamba fedha hizo
zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya
akaunti ya fedha za Escrow.

Kenya:Raila Odinga amerusiwa kutoka hospital alikolawa baada ya kuugua ghafla soma zaid.

Kenya:Raila Odinga amerusiwa kutoka hospital alikolawa baada ya kuugua ghafla soma zaid.

KENYA: Raila Odinga ameruhusiwa kutoka
Hospitali alikolazwa baada ya kuugua
ghafla akidaiwa alikula chakula chenye
sumu hapo jana wakati akiendelea na
kampeni katika Kaunti ya Kilifi huko
Mombasa.
Mgombea huyo kupitia tiketi ya
Muungano wa NASA amewatoa wasiwasi
watu wake kuwa yuko salama kiafya na
anaelekea Jijini Nairobi kwaa

Monday, July 3, 2017
Rais wa TFF na katibu wake wamerudishwa rumanda kwa kunyimwa dhamana leo mahakamani mpaka july17.soma zaid

Rais wa TFF na katibu wake wamerudishwa rumanda kwa kunyimwa dhamana leo mahakamani mpaka july17.soma zaid

# Habari:Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake
Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana na
hivyo wamerudishwa rumande ambapo Kesi yao
itatajwa tena Julai 17 mwaka huu.
- leo Jumatatu Malinzi na wenzie walifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam kufuatia kushtakiwa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
kwa makosa 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Saturday, July 1, 2017
Gorofa la mkombozi fishing and marine tansport lateketea kwa moto mkoan Mwanza.soma zaid

Gorofa la mkombozi fishing and marine tansport lateketea kwa moto mkoan Mwanza.soma zaid

Sehemu ya ghorofa ya tano ya jengo la Kampuni
ya Mkombozi Fishing and Marine Transoprt
lililopo Kirumba Mwaloni katika Manispaa ya
Ilemela mkoani Mwanza imeungua kwa moto
ambao chanzo chake bado hakijafahamika.
Jengo hilo linalomilikiwa na mfanyabiashara wa
jijini Mwanza Kitana chacha ujenzi wake bado
haujakamilika.
ITV ilifika katika eneo la tukio hilo na kukuta
wananchi wakishirikiana na askari wa jeshi la
zimamoto na uokoaji Mwanza kuzima moto huo
uliokuwa umeteketeza mbao zinazotumika kwa
ujenzi wa ghorofa hilo, huku Afisa mafunzo na
habari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa
Mwanza Mkaguzi Msaidizi Gadaffi Masoud
akifafanua kuhusu tukio hilo.
Tukio hilo la moto limekuja ikiwa ni wiki tatu
baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya
nyuma ya nyumba ya kulala wageni ya
Shinyanga iliyopo mtaa wa Lumumba jijini
Mwanza na kusababisha kifo cha mmiliki wa
jengo hilo Maduhu Masunga maarufu kama mzee
Shinyanga pamoja na kuteketeza silaha
mbili,kiasi kikubwa cha fedha na mali mbalimbali
ambazo thamani yake.picha kwa lisani ya itv.

UGANDA: Msanii wa mziki wa nchini Bob wine ameshinda Ubunge kwa kura 25,659.soma zaid

UGANDA: Msanii wa mziki wa nchini Bob wine ameshinda Ubunge kwa kura 25,659.soma zaid

UGANDA: Mwanamuziki Robert Kyagulanyi
(Bobi Wine) ametangazwa kuwa mshindi
wa kiti cha Ubunge kupitia jimbo la
Kyadondo Mashariki.
- Bobi Wine amepata kura 25,659, huku
Ssebalu akipata 4,566, Kantinti 1,832,
Nkunyingi amepata 575 na Kayongo
akipata 377.
=======
KAMPALA - Robert Kyagulanyi Ssentamu,
best known as Bobi Wine, has taken the
Kyadondo East seat after he was declared
winner by the Electoral Commission
Thursday evening.
The musician-turned-politician beat his
four challengers including NRM's William
Sitenda Ssebalu, FDC's Apollo Kantinti,
and independents Nkunyingi Muwada and
Dr. Sowedi Kayongo Male.
After tallying up the votes from the 93
polling stations across the constituency,
Electoral Commission returning officer
Francis Nkurunziza, announced the final
results and declared Kyagulanyi winner at
9.42pm local time.
Bobi Wine garnered a winning 25,659
votes, Ssebalu got 4,566 votes, Kantinti
managed 1,832 votes, Nkunyingi had 575
and Kayongo received 377 votes.
The number of valid votes was 32,999,
the invalid ones were 311 and 41 votes
were spoiled. The total number of votes
cast was 33,310.
"The first thing I want to do is to
reconcile the leaders of Kyadondo East,"
said Kyagulanyi, after being declared
victor.
"I want politics to bring us together," he
said, just like music does.

Back To Top