Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Sunday, April 30, 2017
Halmashauri zaongoza kwa vyeti feki huku Halmashaur za Dar na Tanga zikiongozwa. Soma zaid

Halmashauri zaongoza kwa vyeti feki huku Halmashaur za Dar na Tanga zikiongozwa. Soma zaid

WAKATI Serikali imetangaza orodha ya majina ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, Halmashauri za Miji, Wilaya, Manispaa na Majiji zimeongoza kwa kuwa na wafanyakazi wenye vyeti bandia huku taasisi za umma zikifuatia. Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais John Magufuli juzi kupokea vitabu vyenye orodha ya watumishi wa umma ambao wamebainika kuwa ama na vyeti pungufu, vyeti tata na vyeti vya kughushi kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki. Hatua ya kufanyika kwa uhakiki huo ambayo ilitokana na agizo la Rais Magufuli inafanya sasa kuwepo kwa nafasi wazi za ajira 12,000 kwa watu wenye sifa ambao wangeweza kuajiriwa katika nafasi hizo lakini nafasi zao zikakosekana kutokana na kuajiriwa kwa watu wasio na sifa. Idadi hiyo inatokana pia na kubainika kuwepo kwa vyeti tata 3,076. Kwa mujibu wa orodha hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dk Laurean Ndumbaro, halmashauri zina idadi ya wafanyakazi 8,716, huku taasisi za umma zikiwa na jumla ya wafanyakazi 1,216. Wakati halmashauri za Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga zinaonekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wafanyakazi wenye vyeti vya kughushi, mikoa ya Simiyu, Mbeya, Songwe, Shinyanga, Ruvuma, Tabora na Singida imekuwa na idadi ndogo zaidi ya wafanyakazi hao. Kwa mantiki hiyo, kubainika kwa idadi kubwa kwa kiwango hicho cha watumishi wenye vyeti vya kughushi katika halmashauri hizo mbali ya kutoa nafasi mpya za ajira lakini pia kutaiwezesha serikali kupata mafanikio katika miradi ya maendeleo kwa kuajiri watendaji wenye sifa stahiki ambao watasimamia miradi kutokana na fedha zake nyingi kuelekezwa katika halmashauri hizo. Ukiondoa halmashauri, vyuo vya elimu ya juu ambavyo ndio tegemeo katika kuzalisha wataalamu, baadhi yake vimebainika kuwa na idadi kubwa ya watumishi wenye vyeti bandia huku Chuo Kikuu cha Sokoine kikiongoza katika kundi hilo kikiwa na wafanyakazi 33. Aidha kwa upande wa kundi hilo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimejidhihirisha kuegemea kwenye weledi kwa kiwango kikubwa baada ya kuwa na mfanyakazi mmoja tu aliyebainika kuwa na cheti bandia. Ukiondoa vyuo hivyo, Chuo cha Utumishi wa Umma kimebainika kuwa na wafanyakazi 10, Chuo Kikuu cha Dodoma wafanyakazi watano, Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili wafanyakazi watano, huku Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam kikibainika kuwa na watumishi sita. Kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu, manufaa ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake ni pamoja na kuviwezesha vyuo hivyo kupata wafanyakazi wakiwemo wahadhiri wenye sifa hatua itakayokuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi ambao sasa watafundishwa na watu wenye sifa za elimu. Aidha orodha hiyo imezitaja taasisi za umma zenye wafanyakazi wenye vyeti bandia ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo imebainika kuwa na wafanyakazi wanane, Mfuko wa Pensheni wa PPF wafanyakazi 16, Shirika la Ndege (ATCL) wafanyakazi 7, Shirika la Reli (TRL) wafanyakazi 24, Mamlaka ya Reli wafanyakazi 39 na Mamlaka ya Anga wafanyakazi 22.

Watumishi wengine 100,000 wanaofanya kazi serikali kuu wenye vyeti feki kuanikwa hadharani. Soma zaid

Watumishi wengine 100,000 wanaofanya kazi serikali kuu wenye vyeti feki kuanikwa hadharani. Soma zaid


SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli
kupokea ripoti ya awamu ya kwanza na pili ya
uhakiki wa vyeti vya kitaaluma vya watumishi wa
umma ambayo imebaini watumishi 9,932 wana
vyeti vya kughushi, watumishi wengine
wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 100,000 nao hatima
yao itajulikana ndani ya siku tano zijazo.
Watumishi hao ni wale wanaofanya kazi Serikali
Kuu, kwa maana ya wafanyakazi wa wizara 18
isipokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, ambayo tayari ripoti yake
imekwishawasilishwa juzi.
Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella
Kairuki, alisema ripoti ya tatu ya uhakiki
itawasilishwa Ijumaa ijayo na imegusa wizara
zote.
Alifafanua kwamba ripoti aliyoiwasilisha juzi kwa
Rais Magufuli, ilikuwa ya awamu mbili ambazo
ziligusa mamlaka za Serikali za mitaa na
sekretarieti za mikoa, taasisi za Serikali,
mashirika ya umma, tume na wakala za Serikali.
Kwa mujibu wa Kairuki, ripoti iliyowasilishwa juzi
iligusa asilimia 75 ya watumishi wote wa
Serikali.
Kwa msingi wa maelezo hayo, MTANZANIA
Jumapili lilifanya makadirio ya kimahesabu kwa
kuangalia kama asilimia 75 ya watumishi
waliohakikiwa ni 400,035, basi asilimia 25
iliyobaki huenda ikawa ni watumishi 133,345.
Kwa mantiki hiyo, hatima ya watumishi hao
itajulikana Ijumaa ijayo wakati ripoti yao
itakapowasilishwa kwa Rais Magufuli.
Awali gazeti hili lilitaka kufahamu idadi ya
watumishi wote wa umma, lakini ilishindikana
baada ya Kairuki kusema kuwa anayefahamu hilo
ni Katibu Mkuu Kiongozi, huku Ikulu nayo ilidai
kuwa suala hilo lipo chini ya waziri huyo.
Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Kairuki
alisema katika mazingira aliyokuwapo ni vigumu
kupata idadi moja kwa moja, hivyo akamshauri
mwandishi amtafute Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi John Kijazi.
“Sasa unaniulizia hapa nitakujibu kweli? Mpaka
na mimi niwasiliane na watu wangu au mpigie
Katibu Mkuu labda yeye anaweza akawa na hizo
takwimu karibu kwa sababu si unajua leo
wanafutwa, mara wameondolewa wengine. Basi
wewe mpigie Katibu Mkuu, usipompata nitumie
ujumbe mfupi wa maneno nimtafute,” alisema
Waziri Kairuki.
Juhudi za kumpata Kijazi ziligonga mwamba
baada ya simu yake kutokuwa hewani.
MTANZANIA Jumapili lilipowasiliana na
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais
Ikulu, Gerson Msigwa, alisema mwenye dhamana
ya kuzungumzia jambo hilo ni Waziri Kairuki.
Alipotafutwa kwa mara nyingine Waziri Kairuki,
simu yake haikupokewa kila ilipopigwa na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi wa mawasiliano kwa
mujibu wa agizo lake, hakujibu chochote hadi
gazeti hili linakwenda mtamboni.
Juzi wakati akiwasilisha ripoti ya awamu ya
kwanza na ya pili, Kairuki alikaririwa akisema;
“Ukiangalia watumishi wengi wako ngazi za
halmashauri ambako wanafikia kati ya asilimia 75
hadi 80 na sisi ndio tumeanza hao, Ijumaa
tunapata ripoti ya mawizara.”
ILIVYOKUWA JUZI
Waziri Kairuki akiwasilisha ripoti ya awamu ya
kwanza na pili ya uhakiki wa watumishi wa
umma mbele ya Rais Magufuli, alisema mpango
wa uhakiki kwa watumishi wa umma
haukuwagusa mawaziri, wakuu wa mikoa na
wakuu wa wilaya, kwa sababu sifa wanazotakiwa
kuwa nazo ni kujua kusoma na kuandika pekee.
“Uhakiki uliwahusu watumishi wa umma pekee,
wakiwamo makatibu wakuu wote na viongozi
mbalimbali katika ngazi ya utumishi wa umma.
“Hatua hii inatokana na ukweli kwamba kwa
mujibu wa sheria, pamoja na miundo ya
maendeleo ya utumishi serikalini, wanatakiwa
kuwa na sifa za msingi za kuingilia na kutumikia
nafasi zao ikiwa ni pamoja na vigezo vya elimu
na vigezo vya kitaaluma, hivyo uhakiki
haukuwahusisha viongozi wa kisiasa.
“Mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wakuu
wa wilaya na madiwani kwa mujibu wa sheria na
taratibu za nchi, wote mnafahamu uteuzi na
uchaguzi unafanyika kwa misingi ya wahusika
kuwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika.
“Na hii ni kwa mujibu wa Ibara 61(1) ya Katiba,
isije ikaonekana ni maneno ya Kairuki,” alisema.
Alisema hatua mbalimbali zimechukuliwa
kuimarisha usimamizi na mifumo maalumu,
hususani ya upokeaji wa taarifa za watumishi ili
kubaini wanaotumia vyeti vinavyofanana.
Kairuki alisema kwa kuzingatia maelezo ya Rais
Magufuli, ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, ilielekeza Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta) kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha
nne, sita na ualimu.
Alitoa mfano wa nchi zilizowahi kufanya ukaguzi
kama huo kuwa ni pamoja na Afrika Kusini, lakini
haikuweza kuwafikia watumishi wote kwa wakati
mmoja.
Akifafanua kilichogundulika kwenye ukaguzi,
alisema kati ya watumishi 400,035 waliokaguliwa,
376,969 wamebainika kuwa vyeti vyao ni halali
ambao ni sawa na asilimia 94.23, wengine 9,932
sawa na asilimia 2.4 wameghushi.
“Alama za siri pamoja na mhuri uliopo katika
vyeti hivyo haufanani na vyeti husika
vilivyotolewa na baraza hilo, kundi la tatu ni
wenye vyeti vyenye utata ambao ni 1,538 sawa
na asilimia 0.3 na vyeti hivyo vinatumiwa na
watumishi 3,076. Hii inamaanisha kuwa cheti
kimoja kinatumika na watumishi zaidi ya mmoja
na vingine watumishi wawili hadi watatu.
“Kundi la mwisho waliowasilisha vyeti pungufu ni
11,596 sawa na asilimia 2.8. Waliwasilisha vyeti
vya kitaaluma. Inatutia shaka kwa sababu
haiwezekani ukaenda kupata sifa ya kujiunga na
vyuo vya kitaaluma haukuwa na cheti cha kidato
cha nne na sita, baraza limewataka waajiri
kuwasilisha vyeti hivyo ili wafanye uhakiki,”
alikaririwa Kairuki juzi wakati akikabidhi ripoti ya
awamu ya kwanza na pili.
Alisema kughushi cheti ni kosa la jinai na hatua
za kisheria zitachukuliwa si kwa waliogushi tu,
bali pia kwa mawakala wanaotengeneza na kuuza
vyeti.
Kwa mujibu wa Kairuki, kanuni za kudumu za
utumishi wa umma, zinasema mwombaji wa ajira
serikalini akitoa taarifa za uongo na zikathibitika
baada ya kuajiriwa, atachukuliwa hatua za
kinidhamu na jinai.chanzo mtanzania digital

Friday, April 28, 2017
Marekani yataka mazungumzo  na Korea kaskazini kumaliza mgogoro. Soma zaid

Marekani yataka mazungumzo na Korea kaskazini kumaliza mgogoro. Soma zaid

Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini yenye lengo la kuondoa zana za nuklia kutoka eneo hilo, kwa mjibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson. Lakini amesema kuwa Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee. Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinza la Umoja wa Mataifa kuwa tisho la Korea Kaskazini la kushambulia majirani zake na zana za nuklia. Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan. Tillerson amezitaka nchi wachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo. "Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu mpango huu hatari." "Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali," Tisho la Korea Kaskazini la kufanya shambulizi la nuklia dhidi ya Korea Kusini au Japan ni la kuwezekana, na ni muda tu kabla ya Korea Kaskazini kufanikiwa kupata uwezo wa kushambulia Marekani." alisema Tillerson.
Breaking News# Jeshi la polisi lapiga marufuku usafi wa CUF jumapili. Soma zaid

Breaking News# Jeshi la polisi lapiga marufuku usafi wa CUF jumapili. Soma zaid

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, imepiga marufuku usafi ulipangwa kufanywa na Chama cha Wananchi CUF upande maalim seif. Hayo yamekuja baada ya Wanachama wa CUF zaidi ya elfu tano na wabunge wa CUF 42 ambao wanamuunga mkono Maalim Seif kupanga kwenda kusafisha ofisi ya chama chao CUF Makao Makuu Buguruni siku ya Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu wa nne. Akiongea na waandishi wa habari Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea akiwa ameambatana na wabunge wengine 41 amesema wameamua kufanya usafi katika ofisi ya chama chao baada ya kuona ofisi hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na Profesa Lipumba na genge lake kufanya mipango ya kuvamia mikutano ya watu, na matukio ya kihalifu. "Siku ya Jumapili ya tarehe 30 mwezi wa nne mwaka huu, wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambao hawamkubali Professa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF wameamua kwenda kufanya usafi kwenye ofisi zao za Buguruni ofisi kuu za chama, hatua hii imekuja baada ya kuona ofisi ile inatumika vibaya kimekuwa ndiyo kijiwe cha wahuni kupanga matukio ya kihalifu kwenda kuvamia mikutano, kuvamia watu sisi kama wanachama tumesema hapana hatuwezi kuacha ofisi yetu itumike vibaya hivyo" alisema Mtolea Mbali na hilo Mtolea amesema wazo hilo lilianzia Temeke lakini limepokewa vyema na sehemu zingine hivyo baadhi ya wanachama kutoka Zanzibar, Tanga na wanachama wa maeneo jirani wataunga na wabunge 42 kufanya usafi huo hapo Buguruni.

Maombi ya Vigogo yakwama kesi ya kuhujumu uchumi.soma zaid

Maombi ya Vigogo yakwama kesi ya kuhujumu uchumi.soma zaid


Mtwara: Maombi ya dhamana ya watuhumiwa wa
kesi ya kuhujumu uchumi inayowakabili
watuhumiwa wanne akiwemo kaimu meneja
mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika (Mamcu)
Kelvi Rajab, yamegonga mwamba baada ya
mahakama kusema haiwezi kusikiliza maombi
hayo kwa sasa, pengine mpaka pale ambapo hati
ya Mkurugenzi wa mashtaka ya pingamizi la
dhamana iliyowasilishwa Mahakamani na upande
wa Jamhuri itakapokuwa imeondolewa.

Thursday, April 27, 2017
Madaktari 258 walioomba kwenda kufanya kazi kenya wametakiwa kuripoti vituo vya kazi hapa nchini siku 14 kuanzia leo. Soma zaid

Madaktari 258 walioomba kwenda kufanya kazi kenya wametakiwa kuripoti vituo vya kazi hapa nchini siku 14 kuanzia leo. Soma zaid


KUITWA KAZINI: Madaktari 258 walioomba
kwenda kufanya kazi Kenya watakiwa kuripoti
katika vituo vya kazi hapa nchini siku 14 kuanzia
leo, Wizara ya Afya yasema.chanzo mwananch

Elimu haina mwisho:# Mzee wa miaka 78 ameanza Darasa la kwanza. Soma zaid

Elimu haina mwisho:# Mzee wa miaka 78 ameanza Darasa la kwanza. Soma zaid


Huko Sirari Mkoani Mara, Mzee wa miaka 78
amejitokeza na kuanza darasa la kwanza mara tu
baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya
awali.

Rais Magufuri kupokea taarifa la zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma. Soma zaid

Rais Magufuri kupokea taarifa la zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma. Soma zaid


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho
tarehe 28 Aprili 2017, atapokea Taarifa ya
zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi
wa Umma katika Ukumbi wa Chimwaga
Mkoani Dodoma.
Taarifa hiyo itawasilishwa kwa
Mheshimiwa Rais na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah
Kairuki.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi
wa Umma liliendeshwa na Serikali kuanzia
Mwezi Oktoba mwaka 2016.

Raia Odinga achaguliwa kupeperusha bendera uchaguzi wa Urais kenya. Soma zaid

Raia Odinga achaguliwa kupeperusha bendera uchaguzi wa Urais kenya. Soma zaid

BREAKING NEWS
Raila Odinga ndiye Mgombea urais kupitia NASA
huku mgombea mwenza akiwa kalonzo musyoka

Kenya# mamia ya wakenya wafurika katika mkutano wa upinzani. Soma zaid

Kenya# mamia ya wakenya wafurika katika mkutano wa upinzani. Soma zaid

Habari:Mamia ya wananchi nchini Kenya
wafurika katika uwanja wa Uhuru Park Jijini
Nairobi kuhudhuria mkutano wa upinzani Nchini
humo ambao unatangaza mgombea atakaye
wania kiti cha urais akitumia muungano wa
NASA kwenye uchaguzi wa Mwezi Agosti Nane.

Mali za Said Lugumi za kamatwa kwa kudaiwa kodi na TRA. Soma zaid

Mali za Said Lugumi za kamatwa kwa kudaiwa kodi na TRA. Soma zaid

Kampuni ya Yono Kupitia TRA
yamekamata majumba matatu ya Lugumi
yaliyoko Ndege Beach Mbweni kwa
kudaiwa kodi ya zaidi ya Bilioni 14.
Nawasilisha kutoka MINJINGU.
=======
Kampuni ya udalali ya Yono, imefanikiwa
kukamata mali za wafanyabiashara
wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia
zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya
kukamata mali hizo kwenye maeneo
mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es
Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.
Katika operesheni hizo maofisa wa Yono
wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa
Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo
imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya
kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela,
Yono imepewa kazi na TRA kukusanya
madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar
es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa
na Zanzibar.
Aliwataka watanzania kuunga mkono
jitihada za Rais John Magufuli za kuleta
maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili
zipatikane fedha za kujenga miundombinu
kama barabara, reli, shule, madaraja,
hospitali na zahanati.
Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi
ya mali za Kampuni ya Lugumi
zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo
alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli
ambapo wanashikilia nyumba za kifahari
za mfanyabiashara huyo.
“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba
za Lugumi zimefungiwa ni kweli,
amefungiwa nyumba zake za kifahari na
anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa
Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8,
Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan
Construction anadaiwa Sh bilioni
45,”alisema.
Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa
madeni yao TRA ndani ya siku 14 na
kwamba muda huo ukipita watapewa
maelekezo na serikali kama ni kuuza mali
hizo ili kufidia madeni yao.
Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye
hakupenda jina lake litajwe alithibitisha
kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko
Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na
mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari
lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.
“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo
nyumba mtakuta alama ambazo huwa
Yono wanaweka kwa nyumba
inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule
Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba
tunazoshikilia,” alisema
Chanzo: HabariLeo

Wednesday, April 26, 2017
Gambo awataka waliokula peas za uma kufunguliwa mashitaka. Soma zaid

Gambo awataka waliokula peas za uma kufunguliwa mashitaka. Soma zaid

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ametaka kurejeshwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Juma Iddi, Mwekahazina Kessy Mpakata pamoja na Dr. Bakari Salum ambao wataungana na Katibu wa Afya Optat Ismail ili kujibu tuhuma zinazowakabili za ubadhirifu wa Fedha za mfuko wa pamoja wa kapu la Afya (Busket Fund). Gambo ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya ziara yake Jijini hapa ambapo alikuatana na wafanyakzi wa Jiji, Taasisis za Serikali, Bodi na Kamati za Shule, Viongozi wa Dini, Wazee wa Mji pamoja na Makundi Maalum. Alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kupokea Taarifa ya Tume aliyoiunda kukagua matumizi ya mfuko huo wa Afya endapo taratibu zilizingatiwa katika mapato na matumizi na kama Fedha hizo ziliwafikia wananchi kupitia huduma bora za Afya. Aliongeza kusema kuwa kupitia Taarifa ya Tume hiyo alibaini ubadhirifu wa Fedha hizo kwani zilipelekwa kwenye Hospital ya St. Elizabert pamoja na Isnasheer pasipo kuwa na Mikataba inayoeleweka na mikataba mingine kutokuonekana kabisa hivyo kuwa na mashaka na matumzi ya Fedha hizo na manunuzi ya madawa kufanyika pasipo kuwa na risit za kielektroniki. “Alisema kuwa haiwezekana Fedha zitumiwe kana kwamba hakuna miongozo wala maelekezo ya Serikali kwa sababu Hospital zingine zimekwisha fungwa lakini bado inaonekana Fedha zilipelekwa sasa sijui zilikuwa zinatumiwa kwenye eneo gani wakati Hospital Haifanyi Kazi” Rc Gambo pia alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia kuwasimamisha Kazi watumishi 23 wa Timu ya Menegimet ya Afya(CHMT) kupisha uchunguzi wa matumizi ya Tsh Mil 63 walizojilipa posho pasipo kuwa na Taarifa ya kazi(Activity report). Ziara hii za siku tabo itahusisha uzinduzi na uwekaji na ufunguaji wa miradi ya maendeleo, mikutano ya hadahara pamoja na kutatua kero za wananchi wa Jiji hili. Nteghenjwa Hosseah Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji Arusha.

Friday, April 21, 2017
Watumishi 2200 wapandishwa vyeo.soma ziaid

Watumishi 2200 wapandishwa vyeo.soma ziaid

BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni 22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2017, Sh. Bilioni 10.5 zimelipwa kwa walimu 22,420, hivyo kufanya jumla ya walimu waliolipwa katika kipindi hicho kufikia 86,234 na kwamba katika fedha hizo, Sh. Bilioni 13.4 zililipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi 6 wa Chuo cha ualimu Korogwe. “Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale watakaostahili,” alisem
Thursday, April 20, 2017
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamta msanii Agnes Masogange.soma zaid

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamta msanii Agnes Masogange.soma zaid

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes
Gerald maarufu kama Masogange kwa
kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya
kutumia dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu
Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati
kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai
mahakamani hapo kwamba upelelezi wa
kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini
mshtakiwa, wadhamini wake na wakili
wake hawakufika hivyo wakili Nkini
akaomba mahakama itoe hati ya
kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu
ni mara ya pili ameshindwa kufika
mahakamani hapo.
Hakimu Mashauri alikubali maombi ya
wakili wa Serikali na kutoa hati ya
kumkamata mshtakiwa ambaye ni
Masogange.
Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa
aheshimu mahakama kutokana na
kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka
2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya
Februari 7 na 14 mwaka huu, katika
maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar
es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina
ya heroin(Diacety Imophine). Pia inadaiwa
kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia
dawa za kulevya aina ya oxazepam.
Chanzo: Mtanzania

Kama kweli unataka kufanikuwa wekeza akili yako katika jambo hili.soma zaid

Kama kweli unataka kufanikuwa wekeza akili yako katika jambo hili.soma zaid

Kuna wakati mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo. Na umakini ni ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika kufikiri na kutenda jambo hilo. Kamwe hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa umaikini. Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo. Hivyo umakini katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo. Mwisho jitahidi kuwa makini juu ya mambo haya; 1. Kuwa makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda. 2. Kuwa makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka. Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu wengine. 3. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea. 4. Kuwa makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati. 5. Kuwa makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija gani kwako. 6. Kuwa makini katika kutambua thamani ya muda na pesa. Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.

Mamia ya raia nchini Venezuela waandamana kupinga serikali.soma zaid

Mamia ya raia nchini Venezuela waandamana kupinga serikali.soma zaid

Ghasia na kufyatua risasi kulijitokeza baada ya mamia ya raia wa Venezuela walipoandamana mitaani wengine wakimuunga mkono rais Nicolas Maduro na wengine wakiipinga serikali. Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani mjini Caracas, ambapo kijana mmoja alipigwa risasi na kupoteza maisha. Katika Mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka vurugu. Upinzani unataka uchaguzi mpya wa urais kutokana na kudorora kwa uchumi nchini humo. Rais Maduro ameulaumu upinzani kwa kusababisha vurugu. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema rais Maduro anakiuka Katiba ya Venezuela Wapinzani wa rais wa Venezuela, Nicolas Maduro wameitisha maandamano mapya siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kutokea ghasia. Kiongozi mkuu wa upinzani Henrique Capriles amezungumza na waandishi wa habari kuwa siku ya leo watakutana raia wote wa Venezuela wakiwa na lengo la kushinikiza rais Maduro kuondoka madarakani. Chanzo: BBC Swahili

Ntoto wa darasa la kwanz mkoani Pwani ahofia kufa maji.

Ntoto wa darasa la kwanz mkoani Pwani ahofia kufa maji.


Mtoto wa darasa la kwanza mkoani
Pwani.anahofiwa kufa maji baada ya kuzama
mtoni wakati wakiogelea.
Mtoto wa darasa la kwanza katika shule ya
msingi Ubena Tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani
aliyefahamika kwa majina ya Karim Salum
anasadikika kufariki dunia baada ya kuzama
kwenye maji ya mto Ngerengere wakati akiogelea
na wenzake huku jitihada za kutafuta mwili wake
zikigonga mwamba kutokana na wananchi
kuutafuta mwili huo kwa zaidi ya siku mbili
mfululizo bila mafanikio.
ITV imeshuhudia wananchi wakiendelea na
jitihada za utafutaji wa mwili wa mtoto Karim
Salum anayesadikiwa kufa maji huku vijana
walioshuhudia mtoto huyo akizama ndani ya maji
wakieleza tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi
Alasiri wakati wakijaribu kuogelea ndani ya mto
huo.
Naye Babu wa mtoto huyo Bwana Issa
Bung’ombe ameeleza kusikitishwa na tukio hilo
na kwamba mtoto huyo aliaga nyumbani
akielekea mtoni kuchota maji ndipo kadhia hiyo
ilipomkuta.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha
Bwawani Abdalah Seifu ameiomba serikali kupitia
vyombo vya uokoaji kuwasaidia kuongeza nguvu
ya kumtafuta mtoto huyo anaye sadikiwa kufa
maji ili kuokoa mwili wake.

Wabunge waendelea kuchezeana.soma zaid

Wabunge waendelea kuchezeana.soma zaid

Dodoma. Mazoea ya baadhi ya wabunge kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuzima hoja za wabunge wenzao, jana uliibuka tena baada ya Mbunge wa Makambako, Deo Sanga kuomba mwongozo uliozima hoja ya kutaja majina ya wabunge 11 wanaodaiwa kutaka kutekwa. Sanga aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni 68 (7) pamoja na 64 A,B,C, alisema ndani ya Bunge yameongelewa mambo yanayohusu mahakama, usalama, mauaji na kutekwa. “Nilikuwa nadhani kupitia kanuni hizi naomba mwongozo wako nini kazi ya Bunge mheshimiwa naibu spika?” alihoji. Mwongozo huo uliibuka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Angelina Malembeka kuwataka wabunge waliosema kuna orodha ya wabunge 11 wanaotakiwa kutekwa kuwataja majina yao. Hoja ya Malembeka ilimlenga Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ambaye siku za karibuni aliliambia Bunge kwamba ameambiwa na mmoja wa mawaziri kuwa kuna wabunge 11 watatekwa na Usalama wa Taifa. Hata hivyo, mwongozo wa spika ulioombwa na Sanga ulizima kiu ya Malembeka aliyetaka kumbana Bashe ataje majina ya wabunge hao 11, badala ya kutaja idadi pekee. Akijibu mwongozo wa Sanga, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliamua kupiga marufuku masuala ya Usalama wa Taifa kujadiliwa bungeni.

Apandishwa kizimbani baada ya kukutwa na kobe 100.soma zaid

Apandishwa kizimbani baada ya kukutwa na kobe 100.soma zaid

MKURUGENZI wa Kampuni ya Afrilulu, Antony Gulfer (47) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa nyara za serikali, ambazo ni kobe zaidi ya 100 wenye thamani ya Sh milioni 18.3. Gulfer ambaye ni raia wa Australia, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha. Mushi alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kukutwa na nyara hizo za serikali kinyume na sheria ya wanyamapori. Alidai kuwa Machi 10, mwaka huu maeneo ya Kilomoni Kunduchi jijini Dar es Salaam, Gulfer alikutwa na nyara za serikali, ikiwemo kobe wanne aina ya tinged, pia kobe 108 aina ya Leopard na wengine wanne aina ya Aldabra. Inadaiwa kuwa kobe wote hao wana thamani ya dola za Marekani 8,190, sawa na Sh milioni 18.3. Mushi alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo, haujakamilika na anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mkeha alisema kuwa mahakama hiyo, haina mamlaka ya kuhusu dhamana na kwamba mshtakiwa anaweza kwenda kuomba Mahakama Kuu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Monday, April 17, 2017
Marekani na Korea ya Kasikazini hapatoshi subira imeshindikana.soma zaid

Marekani na Korea ya Kasikazini hapatoshi subira imeshindikana.soma zaid


# Habari:Makamu wa Rais wa Marekani Mike
Pence amesema kipindi cha taifa hilo kuwa na
subira na Korea Kaskazini kimepita.
Bw. Pence ametoa kauli hiyo alipozuru eneo
ambalo haliruhusiwi kuwa na wanajeshi katika
mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.
# BBC

Sunday, April 16, 2017
Jazishi ya mwinjilist Onoratus Mwinuka anayedaiwa kutekwa na kuuwawa.soma zaid

Jazishi ya mwinjilist Onoratus Mwinuka anayedaiwa kutekwa na kuuwawa.soma zaid

DAR ES SALAAM: Huku tukio la msanii wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na wasanii wenzake watatu kutekwa studio likiwa bado halijapoa, mwinjilisti aliyefahamika kwa jina la Onoratus Mwinuka (51), mkazi wa Mabwepande jijini Dar, amedaiwa kutekwa na kuuawa kisha mwili wake kufukiwa ardhini huko Mabwepande, Risasi Jumamosi linakudadavulia. HABARI KAMILI Kwa mujibu wa dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Mwinuka, taarifa za kupotea kwa kaka yeka alizipata Machi 14, mwaka huu kutoka kwa watoto wa marehemu ambapo walisema tangu baba yao alipoondoka alfajiri ya Machi 13, mwaka huu hakuwa amerejea tena nyumbani. Veronica aliendelea kusema watoto hao walimwambia pia katika alfajiri hiyo ya saa kumi, marehemu aliondoka na mfanyakazi wake wa kiume aitwaye Ayubu aliyekuwa na kawaida ya kumsindikiza kila mara kutafuta usafi ri ili apeleke maziwa ya ng’ombe mjini kisha akishapata usafi ri yeye hurudi nyumbani. Inadaiwa kuwa, siku hiyo, walipofi ka kituoni, lilitokea gari aina ya Toyota Noah, wakamuuliza marehemu kama anakwenda, akakubali na kupanda, gari likaondoka. “Baada ya hao watoto kunipa taarifa hizo sikuweza kushituka mara moja maana nilifahamu pengine kaka alikuwa amepitia kwenye shughuli zake nyingine za kiuinjilisti maana alikuwa ni muinjilisti lakini baada ya kupita siku hiyo aliyopotea, siku iliyofuata kuna wizi ulitokea nyumbani kwake ndipo nikashituka,” alisimulia Veronica. WIZI WATOKEA NYUMBANI KWA MAREHEMU Veronica aliendelea kusema kuwa, wizi huo uliofanyika ulifanywa na mmoja wa wafanyakazi wa marehemu ambaye aliiba fedha zinazokadiriwa kufi ka shilingi milioni 30 ambazo marehemu alikuwa amezitoa benki siku moja kabla ya kupotea kwake kwa ajili ya kununua gari ndogo (pick up) ya mizigo na kuwalipia wanaye ada ya shule. “Kiukweli niliona si hali ya kawaida hasa nilipounganisha matukio ya kuibiwa nyumbani na kupotea kwake. “Lakini mbaya zaidi kaka nyumbani alikuwa amebaki mwenyewe. Mkewe alikuwa nyumbani kwao kwa ajili ya kumuuguza mdogo wake, kwa hiyo niliamua kuwataarifu ndugu zangu wengine, akiwemo shangazi yetu ambapo akatutaka tutoe taarifa kwenye vyombo vya usalama.” ATAFUTWA MPAKA MOCHWARI “Mkewe pia alirudi, tukaenda kwenye ofisi za serikali ya mtaa kisha kwenye Kituo cha Polisi Mabwepande ambako tulitoa taarifa na kupewa RB ili kumtafuta yeye pamoja na mfanyakazi yule aliyeiba. Kazi ya kumtafuta sehemu mbalimbali ikaanza ikiwemo mahospitalini, mochwari na sehemu nyingine mbalimbali lakini hatukuweza kumpata kaka kwa zaidi ya siku ishirini baadaye,” alisema Veronica. AZIDI KUSIMIULIA Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema kuwa, ilifi ka hatua ndugu wakakata tamaa kwamba hawezi kupatikana tena, lakini hivi karibuni mdogo wao mwingine wa mwisho aitwaye Alphonsia Mwinuka alifi ka kutoka Mbozi, Mbeya kwa ajili ya kazi hiyo ya kumtafuta kaka yao. Baada ya kufi ka akishirikiana na kijana wa kazi (Ayubu) aliyekuwa na marehemu siku ya mwisho kuonekana pamoja na watoto wa marehemu, walianza msako upya katika misitu inayozunguka nyumba ya marehemu. SIKU YA MWILI KUONEKANA “Kiukweli siku hiyo tulimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio. Giza lilipoanza kuingia mimi nilikuwa tayari nimechoka, nikamwambia Ayubu pamoja na mtoto wa marehemu aitwaye Daniel mwenye miaka kama saba kwamba, waende upande mwingine kumtafuta mimi nikarudi nyumbani.” DALILI ZA KUONEKANA MWILI WA MAREHEMU “Baada ya muda walirudi na kuniambia kuna sehemu porini ilichimbwa, pia ilikuwa na ufa jambo lililoashiria kwamba kuna kitu kilizikwa. Ayubu alisema alipatilia shaka hivyo kupapiga picha kwa kutumia simu yake ya kisasa (smart phone). “Baada ya kunionesha na mimi zile picha niliitilia shaka ile sehemu. Lakini sikuongea jambo lolote mpaka siku iliyofuata, tulitoa taarifa kwenye vyombo vya usalama na kwenda kwenye eneo lile tukiambatana na wananchi wa mtaa ule, lengo ni kuangalia pale mahali palizikwa nini,” alisema Alphonsia. ENEO LA TUKIO Alphonsia alisema, walipofi ka jirani na eneo hilo aliloliona kwenye picha mnato za simu, cha kushangaza, yule kijana akaanza kuwazungusha, lakini baada ya kumbana aliweza kuwaonesha na baada ya kuchimba waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umeharibika sana. “Kiukweli ilitusikitisha mnomno, hatukuweza kuamini kuwa mwili tuliokuwa tunauona ulikuwa ni wa ndugu yetu, hasa baada ya mkewe kuyatambua mavazi. Kutokana na tukio lenyewe ilionesha ndugu yetu alitekwa na watu waliomuua kisha wakamzika pale. “Ni vigumu kufahamu sababu hasa ilikuwa nini lakini ni jambo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu. “Baadaye polisi walipokuja, walimchukua Ayubu kwa ajili ya kwenda kusaidia upelelezi na mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya taratibu zingine za kipolisi,” alisema Alphonsia. TAMKO LA SERIKALI YA MTAA Naye mwenyekiti wa mtaa huo, Abdallah Omar alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alilaani vikali matukio ya utekaji nyara yanayoendelea nchini na kusema ni kinyume na haki za binadamu. Mwili wa marehemu ulizikwa juzi Alhamisi kwenye Makaburi ya Mabwepande. Ameacha mke na watoto wanne. KUMBUKUMBU MUHIMU Matukio ya utekaji yanazidi kushamiri nchini, hadi sasa rekodi inaonesha, waliowahi kutekwa ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ben Saanane (hajapatikana), aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, Absolom Kibanda (alijeruhiwa), Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka (alijeruhiwa) na Roma Mkatoliki (alijeruhiwa) na wenzake watatu. Hata hivyo, baadhi ya matukio hayo yamekuwa yakihusishwa kufanywa na wabaya wa waathirika hao ambapo baadhi ya wabunge, akiwemo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, hivi karibuni alitoa hoja ya kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguzaa matukio hayo. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kwa upande wake alisema serikali inachunguza matukio hayo ili kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo.chanzo muungwana blog

Rais Trump ameamuru jeshi la marekani kuvamia Somalia.soma zaid

Rais Trump ameamuru jeshi la marekani kuvamia Somalia.soma zaid

Hii Ni Maanadalizi ya Vita Dhidi ya Korea Kaskazini..!!! Udaku Special Blog / 4 hours ago Zaid ya wapiganaji 100 wa Alshabab, ikiwemo makamanda 20 wa Alshabab wanaaminika kuuawa kwenye shambulizi la anga lililotekelezwa na Marekani mapema jana(Jumamosi) katika eneo la El-Adde kusini kwa Somalia. Wenyeji na maafisa usalama katika eneo hilo ambapo wanajeshi wa Kenya walivamiwa na kuuawa na kundi hilo mwezi januari mwaka jana(2016) walisema kua walisikia ndege za kivita zikiangusha mabomu kwenye maficho ya kundi hilo. Shambulizi hilo linajiri siku chache baada ya Marekani kusema kuwa itatuma jeshi lake nchini Somalia kutoa mafunzo na vifaa kwa jeshi la Somalia na AMISOM ili kuiwezesha kushinda vita dhidi ya Alshabaab. Source: China Xinhua News

Makachero wa marekani waanza kuingia Korea ya Kasikazini tayari kwa vita.soma zaid

Makachero wa marekani waanza kuingia Korea ya Kasikazini tayari kwa vita.soma zaid

Hii habari ya majasusi wa USA, majasusi hawa wa America wenye Asili ya korea wamejipenyeza ndani ya korea kaskazi kuanzia December mwaka jana Na kwa taarifa zilizovuja Rais wa korea kaskazin ameamuru kusitisha Visa kwa raia wanaotoka nchi za magharibi kutokuingia North Korea kwa muda usiojulikana Pia ametoa wito kwa raia wazalendo wa korea kaskazin kutoa taarifa kwa mtu yeyote wanaemshukia hana maadili ya korea kaskazin Siku ya jumapili iliyopta wanajeshi watatu wamenyongwa korea kaskazin wakishutumiwa kuvujisha mipango ya jeshi Lao kwa jeshi la USA Pia Rais wa korea kaskazin jana alia muru kurushwa kwa kombora kwa siri kubwa ambalo badae lilifeli na mwana jeshi moja wa korea kaskazin anasemekana alituma kila kitu kilichofanyika makao mkuu pentagon Ndio maana Leo mkuu wa idara ya jeshi u pande wa peninsula alitangazaa kushindwa kwa kombora lililorushwa la North Korea kufeli vibaya Mike pence, makamu Rais wa USA Ambaye yupo njian kuelekea South Korea Inasemekana ameambatana na nyambizi zisizoonekana katika peninsula ya korea kaskazin Majasusi wa USA wamenasa mawaasiliano kati ya wazir wa mambo ya nje ya urusi, wakiwasiliana na wenzao wa China Pmj na uturuki na North Korea na iran Wakat huo huo makao Rais pence anawasiliana na Donald Trump akiwa njian kuelekea South Korea Wazir wa mambo ya nje wa uingereza amempigia simu wazir wa mambo ya kigeni wa USA kumhakikishia juu ya North Korea kurusha kombora lililofeli Na Inasemekana usiku mzima wa jana Rais Trump alikuwa kwenye mazungumzo mazito na waziri wa ulinzi wa USA pamoja na mkuu wa majeshi Wakuu ni baampa to baampa Mimi naomba USA asipagane Ase, maana madhara yake yatakuwa ni kwa dunia nzima

Makachero wa marekani waanza kuingia Korea ya Kasikazini tayari kwa vita.soma zaid

Makachero wa marekani waanza kuingia Korea ya Kasikazini tayari kwa vita.soma zaid

Hii habari ya majasusi wa USA, majasusi hawa wa America wenye Asili ya korea wamejipenyeza ndani ya korea kaskazi kuanzia December mwaka jana Na kwa taarifa zilizovuja Rais wa korea kaskazin ameamuru kusitisha Visa kwa raia wanaotoka nchi za magharibi kutokuingia North Korea kwa muda usiojulikana Pia ametoa wito kwa raia wazalendo wa korea kaskazin kutoa taarifa kwa mtu yeyote wanaemshukia hana maadili ya korea kaskazin Siku ya jumapili iliyopta wanajeshi watatu wamenyongwa korea kaskazin wakishutumiwa kuvujisha mipango ya jeshi Lao kwa jeshi la USA Pia Rais wa korea kaskazin jana alia muru kurushwa kwa kombora kwa siri kubwa ambalo badae lilifeli na mwana jeshi moja wa korea kaskazin anasemekana alituma kila kitu kilichofanyika makao mkuu pentagon Ndio maana Leo mkuu wa idara ya jeshi u pande wa peninsula alitangazaa kushindwa kwa kombora lililorushwa la North Korea kufeli vibaya Mike pence, makamu Rais wa USA Ambaye yupo njian kuelekea South Korea Inasemekana ameambatana na nyambizi zisizoonekana katika peninsula ya korea kaskazin Majasusi wa USA wamenasa mawaasiliano kati ya wazir wa mambo ya nje ya urusi, wakiwasiliana na wenzao wa China Pmj na uturuki na North Korea na iran Wakat huo huo makao Rais pence anawasiliana na Donald Trump akiwa njian kuelekea South Korea Wazir wa mambo ya nje wa uingereza amempigia simu wazir wa mambo ya kigeni wa USA kumhakikishia juu ya North Korea kurusha kombora lililofeli Na Inasemekana usiku mzima wa jana Rais Trump alikuwa kwenye mazungumzo mazito na waziri wa ulinzi wa USA pamoja na mkuu wa majeshi Wakuu ni baampa to baampa Mimi naomba USA asipagane Ase, maana madhara yake yatakuwa ni kwa dunia nzima

Thursday, April 6, 2017
Ni kweli mwanaume mwenye miaka 29 bado anaitwa mtoto katika mapenzi?.soma zaid

Ni kweli mwanaume mwenye miaka 29 bado anaitwa mtoto katika mapenzi?.soma zaid

Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi! Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au?? By Seth De Jesus Giovanni
kiongozi wa freemason Tanzania na Afrika mashariki afariki dunia.soma zaid

kiongozi wa freemason Tanzania na Afrika mashariki afariki dunia.soma zaid

Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya
Freemason Tanzania na Afrika Mashariki,
Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande
afariki Dunia.
Sir Andy amekuwa mwanachama wa
Freemasons kwa takribani miongo 6
tangu ajiunge.
Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928
ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi
Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).

Wednesday, April 5, 2017
Mapenzi yasababisha utoro kazini.

Mapenzi yasababisha utoro kazini.

Kuna jambo linanishinda hapa mwenzenu huyu mwanamke anapenda mapenzi sana mpaka nataka nihame nyumba. Kitu kinachonishinda nikiwa faragha na huyu mwandani wangu.... nikishamaliza huwa nakuwa nimechoka na kizunguzungu. sasa kama siku tatu zilizoissha niliitwa na bosi wangu kuhusu tabia nayoionyesha. nilijitetea sana. Nikaanzisha mtindo, namuomba work mate wangu anisainie kissha nakuja baadaye. kwa kweli hili swala la mapenzi kila siku nimelishindwa. Nikitoka kazini napita sehemu flani napoteza muda saa ziende. nikifika nyumbani nakuta nasumbiriwa kama kitoweo. ukimkaushia mara akutekenye, akukalie, fujo tupu unajikuta ushafanya. kwa kweli hapa pamenishinda, nakosa nguvu nakuwa kama mgonjwa. Nitumie mbinu gani angalau ipungue ata kwa mwezi mara mbili maana nashindwa sasa.
Back To Top