Simulizi ya ERIC SHIGONGO,DIMBWI LA DAMU sehemu ya 14.soma zaid
ERIC SHIGONGO
DIMBWI LA DAMU-14
Masaa mawili kabla �nyumba ya Manjit
�kulipuliwa kwa moto na majambazi waliotumwa
na wafanyabiashara maadui zake, Leah na
Victoria waliondoka kwenda kula chakula cha
usiku katika mgahawa wa Foodmasters uliokuwa
hatua chache tu kutoka nyumbani kwao, cha
kushangaza siku hiyo wote wawili hawakutaka
kula chakula cha kupikwa nyumbani. Kokote
alikokwenda nje ya nyumba Victoria hakukisahau
kipande cha noti walichogawana na kaka yake,
alikuwa tayari kupoteza vitu vingine vyote lakini
si kipande hicho
Ghafla wakiwa katika mgahawa huo kabla hata
chakula hakijaletwa walishutshwa na mlio ya
ving’ora vya magari ya zima moto vikipita kwa
kasi kubwa nje ya mgahawa.
Kila mtu alionyesha mshangao mkubwa na
kilichofuata baada ya ving’ora hivyo ulikuwa ni
moshi mkubwa ulioonekana kuzunguka maeneo
ya nyumba yao, Leah alishtuka sana na kukimbia
kwenda nje ya mgahawa akiwa amemshika
Victoria mkono, nje alimwigiza ndani ya gari na
safari ya kurudi nyumbani kwao ilianza haraka!
“Dada kuna nini?”
“Moto, moto unawaka?Sijui ni nyumbani kwetu?”
“Moto? Nyumbani kwetu?”
“Ndiyo!”
“Haiwezekani dada!” Kuna wakati Victoria
alimwita Leah mama na wakati mwingine
alimwita dada, alishindwa atumie jina gani.
“Acha twende tukaangalie!”Alisema Leah
akiliendesha gari lake kwa kasi kubwa, mapigo
ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi kubwa,
walivyozidi kukaribia dalili zote zilionyesha kuwa
ni nyumba yao iliyokuwa ikiungua! Kadri alivyozidi
kuelekea nyumbani ndivyo moto na moshi
ulivyozidi kuongezeka.
“Ni nyumba yetu!” Leah alisema akimpigapiga
Victoria begani.
“Imeungua?”
“Ndiyo inaungua na sijui nini kimetokea mpaka
ikashika moto! Kwanini matatizo yamekuwa
mengi kiasi hiki kwetu?” Alijiuliza Leah bila kujua
la kufanya.
Bila kutegemea machozi yalianza kumtoka kwani
vitu vingi vyenye thamani vilikuwa vimeungulia
ndani ya nyumba yao, roho ilimuuma sana Leah.
Kwa matatizo waliyokuwa nayo katika familia yao
alijua tayari walikuwa wamekwisharejea katika
umasikini! Leah alikata tamaa!
“Tutafanya nini sisi? Manjit nae ana madeni ya
mamilioni ya dola za watu, tutakuwa wageni wa
nani sasa?” Alijiuliza Leah huku akilia! Muda wote
akiwa amekumbatiana na Victoria wote wakilia.
Ghafla bila kutegemea jambo hilo Victoria
alishtukia Leah akichomoka kutoka mikononi
mwake na kuanza kukimbia kwenda mbele , kwa
jinsi hali ya joto ilivyokuwa mahali waliposimama
pamoja na kutokuona Victoria alijua lazima Leah
alikimbilia motoni!
Victoria alianza kulia akipiga kelele na kuomba
msaada huku nae akijaribu kutembea taratibu
kwenda mbele akiita jina Leah kwa sauti ya juu.
“Dada Leah! Dada Leah! Dada Leah! Uko wapi?”
Alisema huku akizidi kutembea kwenda mbele
zaidi.
Hakusikia sauti ya Leah ikiitika mahali popote na
joto lilizidi kuongezeka, moto nao ulizidi kuwaka
kuelekea mahali aliposimama, mara ghafla
alishtukia akinyakuliwa na mikono mikubwa na
mazito ya mwanaume!
“Wewe unafanya nini hapa wakati moto
unakuelekea? Utawaka ohooo!”
“Dada yangu ameingia ndani ya moto, dada
yangu ameingia ndani ya moto! Tafadhali
mtoeni!”Alizidi kulia.
“Ameingiaje?”
“Amekimbilia ndani tu!”
“Kwanini?”
“ Hii ni nyumba yetu!”Alizidi kueleza Victoria huku
akilia.
Ilikuwa ni mikono ya mtu wa zimamoto
alimchukua victoria na kwenda kumkalisha mbali
kabisa ya moto! Ambako Victoria alikaa na
kuendelea kulia akijua wazi Leah alikuwa amejiua
motoni, alikuwa ameamua kuteketea pamoja na
nyumba na vitu vyao.
Nusu saa baadaye watu wengi walifurika eneo la
tukio wakishangaa na miongoni mwao alikuwepo
Manjit aliyekuwa amerejea nchini Canada kutoka
Baghdad muda mfupi kabla!
******************
Manjit aliumia sana moyoni mwake kuona
nyumba yao ikiteketea, aliamini mama yake
pamoja na Victoria walikuwa ndani ya moto huo!
Bila hata kusita aliamua kukimbia kuelekea ndani
ya jengo kwa lengo la kwenda kuwaokoa Victoria
na mama yake Leah! Mbele kidogo moshi mkali
ulijitokeza akawa haoni mbele yake, akashindwa
kusonga mbele na kugeuza akikimbia kurudi nje!
Alifanikiwa kutoka hadi nje ya jengo ambako
alifikia mikononi mwa maaskari wawili wa Zima
moto! Walimkatama na kumkimbiza hadi sehemu
alipokalishwa Victoria na kuanza kumpepea kwa
sababu alionekana kushindwa kuhema vizuri!
“Kifua chake kimejaa moshi hebu mpelekeni
hospitali haraka!” Aliamuru mmoja wa maaskari
na Manjit alinyanyuliwa haraka na kupakiwa
ndani ya gari la wagonjwa kukimbizwa hospitali
ambako aliwekewa mashine ya oksijeni na dakika
kama ishirini hivi baadaye alirejea katika hali
yake ya kawaida na kuanza kulia akiomba
aonyeshwe mahali mama yake na Victoria
walipokuwa!
“Mama yako bado hajaonekana ila Victoria yupo!”
“Mama yuko wapi? Naomba basi mmlete hata
Victoria niongee naye nina uhakika atakuwa
anafahamu mahali mama alipo, mali si kitu
kwangu ninachotaka ni mama yangu peke yake!”
Alisema Manjit huku akizidi kulia, hakuugua
mahali popote mwilini kwake.
Hali yake haikuwa mbaya hata kidogo na
angeweza hata kuruhusiwa kutoka wodini lakini
madaktari hawakufanay hivyo baada ya kupewa
taarifa kuwa alitaka kuingia ndani ya nyumba
iliyowaka moto ili afe! Walizidi kumweka wodini
hadi asubuhi ya siku iliyofuata aliporuhusiwa na
kupelekwa chini ya uangalizi wa polisi hadi eneo
la tukio na kushuhudia shughuli za uzimaji wa
moto zikimalizika! Mtu wa kwanza kumwona
mahali pale alikuwa ni Victoria, alimkimbilia na
kukumbatiana kwa furaha.
“Anti Vicky mama yupo wapi?” Aliuliza baada tu
ya kumbusu kila upande wa shavu lake!
“Alikimbilia kwenye moto! Hivyo atakuwa
amekufa!”
“Hapana haiwezekani! Mama hawezi kufa”
“Ni kweli, mimi nilikuwa naye hadi mara ya
mwisho, alichomoka mikononi mwangu na
kukimbilia motoni, nina imani atakuwa
amekufa!”Alisema Victoria akilia na wote
walikumbatiana na kuendelea kulia, ilibidi
waondolewe hadi hotelini ambako Manjit alipanga
vyumba viwili na yeye na Victoria waliishi
wakiangalia ni nini cha kufanya baada ya hapo!
Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Manjit na
Victoria, Manjit alishindwa kuelewa ni nani
aliyekuwa akimfanyia hujuma hizo! Kilikuwa ni
kitendawili alichoshindwa kabisa kukitegua.
Akiwa hotelini alizidi kumtafuta mama yake
akiamini bado alikuwa hai, alitangaza hata katika
vyombo vingi vya habari na kuahidi zawadi kubwa
kwa mtu yeyote ile angefanikisha kupatikana kwa
mama yake, lakini kwa masaa mengi hakuna mtu
hata mmoja aliyejitokeza kudai kumwona Leah!
Manjit alizidi kuchanganyikiwa na hakujua kipi
cha kufanya!
Siku ya tatu wakati watu wa idara ya Uokoaji
wakiendelea na kazi ya uokoaji walikuta mabaki
ya binadamu aliyeungua vibaya katika chumba
kilichoonekana kuwa sebule, ingawa ilikuwa si
rahisi kufahamu kama mabaki hayo yalikuwa ya
mama yake au la, Manjit alilazimika kuamini
hivyo na mazishi ya heshima zote yalifanyika,
akaamini kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa
mama yake! Akabaki na mtu mmoja tu
aliyemtegemea nchini Canada, huyo hakuwa
mwingine bali Victoria.
Ikiwa ni wiki moja baada ya mazishi ya mama
yake, vituo vyake vyote vya mafuta vilikamatwa
na shirika la kodi nchini Canada, kwa madai ya
kuchunguza kama Manjit alilipa kodi zake sawa
sawa, vituo vyote vilitiwa makufuli, wafanyakazi
wote wakaondolewa na maaskari waliwekwa
kuvilinda! Kifupi hali ilikuwa mbaya mno kwa
Manjit! Kwani ni biashara hiyo peke yake
aliyoitegemea katika maisha yake. Alishindwa
kuelewa angeishije.
Mwezi mmoja baadaye alichukua pesa zake zote
zilizokuwa benki na kulipa nusu ya deni la mafuta
alilodaiwa na Patrick, akaunti yake ikabaki bila
hata senti! Hakuelewa hata kidogo pesa za
kumalizia deni hilo angepata wapi, Manjit
alitamani kufa lakini alishindwa kuufikiria uamuzi
huo kwa sababu ya Victoria! Alishindwa kuelewa
angebaki na nani? Huo ndio ulikuwa wasiwasi
wake mkubwa, kama Victoria angekufa katika
moto hata yeye pia angefuata na wote watatu
wangehamia kuzimu alikotangulia baba yake.
***************
Hali haikuwa nzuri pia nchini Iraq, Abdulwakil
baba yake Patrick, alikasirishwa sana na kitendo
cha mtoto wake kukopesha kiasi kikubwa cha
mafuta bila kumshirikisha.
“Ulikuwa mgonjwa baba!”
“Pamoja na hayo yote lakini kwanini ulimkopesha
mtu ambaye hana uwezo wa kulipa?”
“Baba, Manjit amekuwa mteja wetu wa muda
mrefu na isitoshe alionyesha karatasi zake za
zabuni ya kuuza mafuta jeshini! Niliona anafaa
nikaamua kumpa mafuta”
“Haiwezekani ni lazima afikishwe mahakamani ili
ashinikizwe kulipa pesa hizo!”
“Sawa baba!”
Siku iliyofuata Patrick aliwaita wanasheria wa
kampuni yao ofisini na kuwapa majukumu ya
kuhakikisha Manjit anakamatwa na kufikishwa
mahakamani haraka iwezekanavyo, ili
kumshinikiza alipe deni alilodaiwa.
“Sawa mzee, tufanya kazi hiyo lakini ili iwe rahisi
zaidi tafadhali muagizie aje hapa Iraq ili kuwa
rahisi zaidi kumkamata!”
“Nitafanya hivyo leo na ninafikiri kesho atafika
hapa!”
“Itakuwa vizuri sana!”
Jioni ya siku hiyo Patrick alipiga simu Canada na
kumwomba Manjit apande ndege kwenda
Baghdad siku iliyofuata ili wapate kuliongelea
deni lake na ni kwa jinsi gani angeweza kulilipa!
Alimtahadharisha kuwa kushindwa kwake kufika
Baghdad kungemaanisha kufikishwa mahakamani
na kwa mujibu wa mikataba waliyowekeana ni
lazima angefungwa, Manjit hakuwa na la kufanya
zaidi ya kukubali kwenda Iraq.
“Lakini nitasafiri na anti yangu ambaye ni kipofu,
sitaweza kumwacha hapa Canada peke yake
watamuua!”
“Hiyo haina tatizo kabisa!”
Siku iliyofuata asubuhi Manjit na Victoria
walipanda ndege ya shirika la ndege la Gufl
kwenda Baghdad, ndani ya moyo wake Victoria
ilikuwa ni kama kuiaga Canada! Hakuamini kama
wangerudi tena katika nchi hiyo ingawa
hakuelewa ni kwanini moyoni mwake aliwaza
hivyo. Walipotua Baghdad, Manjit alichukua teksi
iliyowapeleka moja kwa moja hadi ofisini kwa
Patrick, haikuwa shida kumwona kwa sababu
alishawataarifu walinzi juu ya ujio wao.
“Pole sana Manjit kwa yaliyojitokeza lakini
naamini yana mwisho wake!”
“Mungu anajua tu!”
“Habari za Canada?’
“Ndugu yangu ni kama Ulivyosikia!”
“Sasa itakuwaje katika deni lililobaki?”
“Hata mimi sifahamu maana pesa zote
nilizokuwa nazo benki ndizo nilizokupa na sielewi
nitapata wapi pesa zaidi!”
“Unasemaje?” Aliuliza Patrick kwa hamaki.
“Kwa kweli sijui mahali pa kupata pesa zaidi!”
“Utalipa tu!”
“Patrick sina biashara nyingine yoyote, vituo
vyangu vyote vya mafuta vimefungwa!”
“Hayo mimi hayanihusu utalipa tu sababu
umejileta mwenyewe hapa Baghdad! Vinginevyo
utaozea jela!”
“Patrick!!!!!!!!!!!!!!!!!!!”
“Nini?”
“Tafadhali nivumilie kidogo au nipe kazi yoyote
katika kampuni yako ili niweze kulipa deni langu!”
“Haiwezekani hata kidogo ni lazima ulipe
pesa!”Alisema Patrick akinyanyua simu yake.
“Hebu waambie hao vijana waingie upesi!”Patrick
alisema na dakika kama tatu baadaye mlango
ulifunguliwa wakaingia vijana watano wenye
nguvu sawasawa na kuwakamata Manjit na
Victoria! Wakaanza kuwavuta kuwatoa ofisini
kwao Patrick.
“Hebu huyo mama mwacheni, mpelekeni kituo
cha polisi huyo tapeli wa kimataifa, niachieni
huyo mama hapa!”
“Sawa bosi!”
Victoria huku akilia machozi alirudishwa na
Manjit alitolewa hadi nje ambako alipakiwa ndani
ya gari na safari ya kwenda kituo cha polisi
ilianza haraka iwezekanavyo.
“Mama huyo kijana ni nani yako?”
“Ni mtoto wa dada yangu!”
“Dada yako mbona wewe mweusi yeye
mchanganyiko?”
“Ni habari ndefu sana kijana, ila ninaweza
kukueleza ukitaka!”
“Nieleze bibi!”
“Niache kwanza nipumzike, itanitia uchungu sana
kuyaongelea mambo hayo, naomba unitafutie
chakula na mahali pa kulala ili nipumzike na
ninachokuomba sana usimfunge mwenzako ana
matatizo makubwa mno!”
“Hata mimi namhurumia bibi lakini baba yangu
hataki kabisa, anadai deni hili limemuongezea
ugonjwa wake!”
“Nipeleke mimi nikaongee naye labda
atanielewa!”
“Sidhani!”
“Wewe nipeleke tu! Kwani baba yako anaitwa
nani?”
“Anaitwa Abdulwakil
“Ni mwenyeji wa wapi?”
“Tanzania!”
“Tanzania? Alifikaje huku?” Aliuliza Victoria kwa
mshangao.
“Ndiyo! Alikuja miaka mingi sana akiwa mtoto”
“Mbona hata mimi pia nilitokea Tanzania?”
“Kweli?”
“Ndiyo!” ERIC SHIGONGO

“Basi si ajabu mtafahamiana!”
“Inawezekana!”
Victoria anapelekwa kukutana na Nicholaus bila
kufahamu! Baad ya kupotezana kwa miaka mingi!
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Ijumaa mahali hapa.