Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Tuesday, May 31, 2016
Kilichotokea UDOM kwa kufukuzwa wanafunzi mapya yaibuka.soma zaid.

Kilichotokea UDOM kwa kufukuzwa wanafunzi mapya yaibuka.soma zaid.

JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si
walimu kugoma kufundisha programu ya
Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati
na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na
Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira
mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni
hapo.
Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa
Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na
Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa
muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri
wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali
inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa
hawana pa kwenda.
Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na
Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo
lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa
walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na
upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo
kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote
kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao.
Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma
kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoelewana
kati ya walimu na Menejimenti ya chuo kutokana
na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu
hiyo chuoni hapo.
Hatuzungumzii fedha zaidi tunazungumzia suala
la kuboresha elimu ili taifa lipate walimu wa
baadaye katika kufundisha Sayansi, Hisabati na
Tehama, vifaa vya kufundishia navyo ni
changamoto kubwa,” alisema.
Katibu huyo alisema kama Jumuiya ya
Wanataaluma wanapata hisia kwamba Wizara ya
Elimu, imeamua kwa makusudi kushirikiana na
uongozi wa chuo kupotosha uhalisia wa jambo
hilo kwani hakuna hata wakati moja ambao
wamefanya mawasiliano na walimu wenyewe
kupata ukweli kutoka upande wao.
“Alichosema waziri bungeni juzi ni taarifa ya
upande moja ambayo haitatupeleka kwenye
utatuzi wa kudumu wa suala hili kutokana na
ukweli kwamba walimu nao wana mengi ya
kuzungumza,” alisema katibu huyo.
Alisema serikali imejenga desturi ya kuonana na
menejimenti za vyuo pindi yanapotokea matatizo
bila kupata taarifa kutoka vyanzo vingine hali
ambayo imekuwa inasababisha vyanzo sahihi vya
matatizo kutojulikana kwa uwazi.
Alisema changamoto za ufundishaji kutokana na
uhaba na walimu kulingana na idadi ya wanafunzi
waliopo. Akitoa mfano alisema kwa sasa Chuo
cha Sayansi Asilia na Hesabu, kina upungufu wa
walimu 128 waliokuwa wanahitajika kufundisha
programu hiyo kwa ufanisi; na kwa muhula
uliopita walimu 72 tu ndio walibeba mzigo wa
upungufu huo na muhula huu hali ilikuwa
inaelekea kuwa mbaya zaidi.
“Wingi wa wanafunzi na uhaba huu wa walimu
ulisababisha upangaji wa ratiba na kufundisha
kutokana na ukweli kwamba kozi ziligawanywa
katika mikondo mingi ambayo walimu
walilazimishwa kuifundisha huku wakiwa na
majukumu ya kufundisha kozi za shahada na
majukumu mengine,” alifafanua.
Alisema chuo kimekuwa na desturi ya kupokea
wanafunzi wengi bila kuzingatia idadi ya walimu
waliopo na miundombinu ya kufundishia na
kujifunzia na hiyo si mara ya kwanza kwa chuo
kufanya hivyo, kwani mwaka 2008 walileta
wanafunzi wengi ambao matokeo yake walimu
kufundisha masomo mengi kuliko uwezo wao wa
kazi.
Alisema taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma ilipotoshwa,
kwani haijaeleza ukweli wa madai uliowasilishwa
na chuo husika. Alisema katika Chuo cha Sayansi
Asilia na Hesabu taarifa inasema
yaliyowasilishwa ni madai ya Sh milioni 367.8 na
kupungua mpaka Sh milioni 90 wakati uhalisia ni
kwamba madai hayo hata yangebanwa namna
gani yasingepungua mpaka chini ya Sh milioni
223.7.
Alisema mfano mwingine ni Chuo cha Elimu
Masafa na Sayansi za Kompyuta ambao taarifa
inasema waliwasilisha madai yanayozidi Sh
milioni 100 wakati taarifa ya chuo inasema ni
madai ya Sh milioni 53.7 tu.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Edson Baradyana
alisikitishwa na yaliyotokea na kuitaka serikali
kufanya jitihada za makusudi ili kumaliza
mgogoro huo na hilo litawezekana kama walimu,
wanafunzi na Menejimenti kukaa pamoja.
Baradyana alisema wanafunzi hawakutendewa
haki kwani ilitolewa notisi ya ghafla ya kuondoka
chuoni huku wengine wakiwa hawana nauli na
hawakujua pa kwenda hali inayofanya waendelee
kuzurura mitaani.
Alisema wanaamini kama Menejimenti ya chuo
ingeonesha ushirikiano wa karibu kwa walimu
wanaofundisha programu hiyo na kushirikiana,
hayo yasingetokea au yasingekuwa makubwa
kiasi hicho.
“Lazima kuangaliwa na kutatuliwa kwa
changamoto nyingine zilizoibuliwa na
wanataaluma na wanafunzi katika uendeshaji wa
programu hiyo badala ya kujikita kwenye suala la
malipo tu, serikali iwe na utaratibu wa
kuwasiliana na walimu na wanafunzi mara
kunapotokea matatizo vyuoni ili kupata taarifa
toshelezi kutoka pande zote,” alisema Mwenyekiti
wa Udomasa.
Aidha, wakati wa kurejeshwa nyumbani kwa
wanafunzi hao wa Udom kukibebwa kisiasa na
vyama vya upinzani, taarifa ya serikali imeeleza
kuwa wahadhiri waliogoma, walitaka kulipwa
posho ya zaidi ya Sh milioni 900.
Akitoa taarifa ya pili bungeni juzi usiku, Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (pichani)
alisema wanafunzi hao si sehemu ya kazi zilizoko
katika mikataba ya ajira ya wahadhiri hao, ila ni
sehemu ya kazi ya ziada.
Kwa kuwa kazi hiyo ni ya ziada, Profesa
Ndalichako alisema walikubaliana walipwe posho
ya kazi ya nyongeza ambayo uongozi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma ulikuwa tayari kutoa zaidi ya
Sh milioni 200.
Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, wahadhiri
hao walisisitiza kuwa wanataka posho hiyo iwe
zaidi ya Sh milioni 900, jambo lililokataliwa na
Mkaguzi wa Ndani wa Mahesabu wa Udom
aliyesema kuwa kiwango hicho ni kikubwa kuliko
uhalisia wa kazi yenyewe.
Kutokana na kutokubaliana kati ya wahadhiri hao
na uongozi wa Udom, wahadhiri hao ndio
wakaitisha mgomo wa kufundisha wanafunzi hao
huku wakiendelea na kazi za kufundisha walio
katika programu za shahada ya kwanza na
kuendelea.
Profesa Ndalichako alisema kwa uamuzi huo wa
wahadhiri, serikali isingeweza kuwachukulia
hatua kwa kuwa wamegomea kazi ya ziada na si
kazi waliyoajiriwa na kuingia mkataba na chuo.
Kwa hali hiyo, Profesa Ndalichako alisema
serikali ililazimika kuingilia kati ambapo Mei 10,
mwaka huu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella
Manyanya alikwenda chuoni hapo kutafuta
suluhu.
Mbali na Naibu Waziri, alisema hata makatibu
wakuu wa wizara hiyo nao walikwenda
kuzungumza na wahadhiri hao bila mafanikio,
huku wanafunzi hao wakikaa chuoni bila kuingia
darasani kwa wiki ya tatu.
Profesa Ndalichako alisema mbali na madai ya
wahadhiri hao, pia wakati wa kutafuta suluhu ya
jambo hilo, walitazama suala la tija kwa
wanafunzi hao wa diploma maalumu ambao ni
zaidi ya 7,800 na pia kwa wanafunzi wa shahada
ya kwanza ambao pia wanapaswa kufundishwa
na wahadhiri hao.
Kutokana na kukosa masomo kwa wiki tatu
mfululizo na kuwepo kwa uwezekano wa
kukosekana tija katika ufundishaji, Profesa
Ndalichako alisema ndio uamuzi wa kuwarudisha
nyumbani wanafunzi hao ukafanyika ili serikali
iangalie upya utaratibu wenye tija zaidi wa
kuwaendeleza wanafunzi hao.
Aidha, Profesa Ndalichako alisema wakati
wanafunzi hao wakitakiwa kurudi nyumbani,
walizingatia hali yao ya kipato, kwa kuwa tayari
walikuwa wameshapewa fedha za kujikimu za
siku 60 tangu Aprili 21, mwaka huu. Profesa
Ndalichako aliwataka wanafunzi hao kuvuta
subira wakati serikali inatafuta namna bora ya
kuwapatia elimu hiyo kwa kuzingatia tija kwao.chanzo habar leo.

Mwalimu apandishwa mahakani kwa kugushi vyeti.soma zaid.

Mwalimu apandishwa mahakani kwa kugushi vyeti.soma zaid.


Dar es Salaam. Mwalimu wa Shule ya Msingi
Kisutu, Marth Komanya amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu
mashtaka manne yanayomkabili likiwamo la
kugushi cheti cha ualimu.
Mshtakiwa amefikishwa mahakamani hapo leo na
kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi
Catherine Kiyoja.
Wakili wa Serikali, Grace Mwanga amedai
mahakamani hapo kuwa siku zisizojulikana
mshtakiwa alighushi cheti chenye namba S.
375\55 ambacho kilionyesha amemaliza elimu ya
sekondari wakati akijua kuwa siyo kweli.
Shtaka la pili, mwalimu huyo amedaiwa
kuwasilisha nyaraka katika Manispaa ya Ilala
ambazo zilikuwa zinaonyesha amemaliza elimu
ya sekondari wakati akijua siyo kweli.
Mwanga amedai katika shtaka la tatu na nne
kuwa mshtakiwa amegushi cheti cha ualimu
chenye namba 71844 kikionyesha alipata daraja
la 3A na kuwasilisha katika Manispaa ya Ilala,
wakati akijua kuwa ni uongo.
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka
yanayomkabili alikana kutenda makosa hayo.
Hakimu Kiyoja ameahirisha kesi hiyo hadi Juni
13, mwaka huu itakapotajwa tena.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili
ambao ni wafanyakazi kutoka taasisi
inayotambulika kisheria waliosaini bondi ya Sh2
milioni kila mmoja.

Rais john magufuli awapa somo wawekezaji.soma zaid.

Rais john magufuli awapa somo wawekezaji.soma zaid.


RAIS John Magufuli amesema Serikali ya Awamu
ya Tano, imejipanga kuwasaidia na kuwaunga
mkono wawekezaji wote wa ndani,
watakaoanzisha viwanda nchini ikiwa ni pamoja
na kuwahakikishia ulinzi wa viwanda vyao.
Pia amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha
anatengeneza mazingira yatakayowapunguzia
kwa kiasi kikubwa kodi wawekezaji wa ndani na
kupandisha kodi zaidi kwa bidhaa zinazoingia
kutoka nje ya nchi.
Dk Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana
katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa ajili ya
utoaji wa Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora
nchini.
Alisema Tanzania ni nchi yenye utajiri wa
rasilimali, fursa ya masoko, nguvukazi na
mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo kipaumbele
kikubwa kitakuwa ni kuhakikisha wazalendo
wanapata fursa ya kufungua viwanda kwa wingi
na kutumia ipasavyo fursa hiyo.
“Mchango wetu Afrika kiuchumi duniani uko chini
ya asilimia tano, sasa ili tuweze kufikia malengo
ya kukua zaidi kiuchumi, Afrika hatuna budi
kufanya mageuzi ya sekta ya viwanda,”
alisisitiza.
Alisema endapo wafanyabiashara wa Tanzania
watawekeza na kuanzisha viwanda nchini,
watapata faida kubwa, wataongezea nchi
mapato, kuingiza zaidi fedha za nje na
kutengeneza ajira kwa wingi.
Alisema kuendelea kutegemea na kutoa
kipaumbele kwa bidhaa za nje hakuna faida zaidi
ya hasara kwa Watanzania kwani pamoja na
bidhaa hizo wakati mwingine kuingizwa kwa njia
za panya na kuwa feki au bandia, pia
watengenezaji wake wako nje ya nchi.
Alisema kwa kuwa watengenezaji wake wako nje
ya nchi, Tanzania haipati mapato zaidi ya ushuru
wa kuingiza bidhaa hizo lakini pia ajira
zinazotengenezwa zaidi ni kwa nchi ambazo
bidhaa hizo zinatengenezwa.
Aliwataka Watanzania hasa watendaji
kuondokana na tabia ya wivu kwa kuwanyima
fursa wawekezaji wa ndani pindi wanapotaka
kuwekeza na badala yake kupendelea na
kuwaamini zaidi wawekezaji kutoka nje.
“Matokeo yake, tunakuwa na rasilimali nyingi
lakini tunashindwa kuziboresha, wanakuja watu
wa nje wanachukua mahindi yetu wanasaga na
kuuza Sudan Kusini kwa bei ya juu, tuacheni hii
dhambi ya wivu ya kunyima fursa pindi mmoja
wetu akitaka kuwekeza sehemu…”
“…nimeshamwambia Waziri wangu Serikali hii ya
Awamu ya Tano inatoa fursa mtu kuwekeza
popote hata kama ni mzalendo, ukitaka kuwekeza
kwenye mbolea, gesi, saruji, kilimo au mafuta
ruksa,” alisisitiza.
Alisema kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili au ya
tatu Afrika kwa ufugaji wa ng’ombe lakini cha
kushangaza hakuna kiwanda cha kutengeneza
viatu, mabegi wala mikanda. “Ng’ombe wetu
hawa wanachukuliwa watu wanaenda
kutengeneza bidhaa hizi wanazirudisha na
kutuuzia kwa bei ya juu.”
Alisema uwekezaji katika sekta ya viwanda
ukikua nchini hata wakulima wa pamba, korosho,
kahawa na mazao mengine ya biashara
watazalisha kwa wingi na kupata faida kwa kuwa
watakuwa na soko la uhakika lakini pia viwanda
hivyo vitatengeneza ajira na kuuza bidhaa hiyo
kwa bei ambayo Watanzania wataimudu.
Alisema serikali yake imejipanga kuwaunga
mkono wawekezaji wa kizalendo watakaoanzisha
viwanda na nguvu kubwa imeelekezwa katika
uwekezaji wa viwanda vya uzalishaji utakaotumia
kwa wingi malighafi zinazozalishwa nchini.
Dk Magufuli alisema lengo la Serikali ya Awamu
ya Tano ni kuhakikisha kupitia sekta hiyo ya
viwanda ifikapo 2020 ichangie katika Pato la
Taifa kwa asilimia 40 lakini pia ajira
zitakazozalishwa kupitia viwanda pia zifikie
asilimia 40.
“Naamini jambo hili linawezekana kwa sababu
nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali
zinazowezesha kujenga uchumi wa viwanda,
tunayo ardhi ya kutosha, nguvu kazi, misitu,
samaki kupitia uvuvi, soko la uhakika kwa kuwa
tumezungukwa na nchi zisizo na maji,” alisema.
Aidha, alisema Tanzania ina fursa nzuri za
uwekezaji kwa kuwa iko katika ushirikiano wa
Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) hivyo kuwa na uwezekano
wa soko la watu zaidi ya milioni 390.
Alisema nchi zote duniani zilizokuwa na hali
mbaya ya uchumi ziliweza kuendelea baada ya
kuwekeza zaidi nguvu zake katika sekta ya
viwanda na sasa nchi hizo ndio zinazoongoza
duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa.
Alitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni China, Korea
Kusini, Thailand, Malaysia, Vietnam iliyochukua
mbegu za korosho nchini na sasa ndio
inayoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo na
Mauritius inayoongoza duniani kwa uzalishaji
sukari.
Rais aliwaahidi wawekezaji wa ndani kuwa
serikali italinda viwanda vyote vya ndani kwa
kuhakikisha inaondoa mazingira yote yanayoweza
kusababisha vikose soko, vishindwe kuzalisha na
kufa.
Akizungumzia changamoto zinazoikabili sekta ya
viwanda nchini, alisema kubwa ya miundombinu
tayari serikali inaifanyia kazi, na mwaka ujao wa
fedha imetenga Sh trilioni moja kwa ajili ya
kuanza ujenzi wa reli ya kisasa.
Aidha, alisema Tanzania iko katika mazungumzo
ya mwisho na Zambia kwa ajili ya kuifanyia
ukarabati reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na
Zambia (Tazara) pamoja na kujipanga kuondoa
kabisa kero ya umeme kupitia miradi mbalimbali
ya umeme inayoendelezwa nchini.
Kuhusu suala la utitiri wa tozo kwa wawekezaji
wa viwandani, Dk Magufuli alieleza kuwa serikali
imeshaunda kamati ya kitaifa kwa ajili ya
kuangalia mazingira ya tozo na endapo kutakuwa
na tozo zisizo na tija zilizolenga kuwanufaisha
wachache zitaondolewa.
“Ni kweli nchi yetu ina vikodi vingi hasa kwenye
mazao kama vile kahawa, pamba na korosho, na
ninafahamu kuna kodi nyingine ni kwa ajili ya
kuliwa na baadhi ya watu, hizi nitaziondoa. Ndio
maana wengine wananiita mkorofi lakini
ninasimamia haki na si lingine,” alisema.
Waziri Mwijage alisema serikali imeanza
kuonesha kwa vitendo dhima yake ya kuijenga
Tanzania ya viwanda kupitia Mpango wake wa
Maendeleo wa miaka mitano 2016/17 hadi
2020/25.
Mwenyekiti wa CTI, Dk Samuel Nyantahe
alimpongeza na kumshukuru Rais kwa kutambua
umuhimu wa sekta ya viwanda katika kujenga
uchumi na kutaja changamoto kadhaa ikiwemo
miundombinu, utitiri wa kodi, uingizwaji wa
bidhaa bandia na utitiri wa mamlaka za udhibiti.

Baada ya kusimamishwa zitto ameandika  maneno haya kwenye ukurasa wake wa fb.soma zaid.

Baada ya kusimamishwa zitto ameandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa fb.soma zaid.

Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati
kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa
nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia.
Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya
ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe.
Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima
udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu
wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio
unaendesha Bunge kwa remote control.
Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa
kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji
tulizoanza kuzijenga.
Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala
tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na
wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka
Uongozi madhubuti na sio itawapendeza wa imla.
Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali
kurudi huko.

Sakata la wabunge wa upizani walioadhibiwa kituo cha LHRC kimetoa tamko.soma zaid.

Sakata la wabunge wa upizani walioadhibiwa kituo cha LHRC kimetoa tamko.soma zaid.


LHRC YAWAKINGIA KIFUA WABUNGE
WALIOADHIBIWA
Siku moja baada ya kuibuka vurugu bungeni,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) leo
kimetoa tamko lenye maagizo matano ikiwamo
wabunge wote waliosimamishwa kurejeshwa
bungeni ili kuendelea na majukumu yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Dk Helen
Kijo Bisimba alitaja maagizo mengine ni kuitaka
Serikali isitishe uamuzi wake wa kuwafukuza
wanafunzi wa UDOM na badala yake itafutwe
suluhu kwa amani.

Rais uhuru kinyatta uso kwa uso na Raila Odinga.soma zaid.

Rais uhuru kinyatta uso kwa uso na Raila Odinga.soma zaid.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anafanya
mazungumzo na kiongozi wa upinzani nchini
humo Raila Odinga ili kuondoa wasiwasi wakati
ambapo taifa hlo linajiandaa kwa uchaguzi
mwaka mkuu ujao.
Bw Odinga alikatiza ziara yake ya kushiriki katika
mazishi kusini magharibi mwa eneo la Natol ili
kuhudhuria mkutano huo wa Uhuru Kenyatta
katika mji mkuu wa Nairobi.
''Nilipokea simu kutoka ikulu ya mkutano na rais
Uhuru Kenyatta.Naomba ruhusa yenu watu wa
Narok nielekee kuzungumza naye,alinukuliwa na
gazeti la Daily Nation akiwaambia
waombolezaji.Nitatangaza kwa Wakenya iwapo
tumekubaliana na iwapo hatujakubaliana pia
nitawaelezea'', aliongezea bw Odinga.
Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord
umeapa kuhudhuria mkutano jijni Nairobi hapo
kesho,licha ya kwamba serikali ilitangaza
kupigwa marufuku.
Watu kadhaa wameuawa katika ghasia kati ya
polisi na wafuasi wa upinzani wanaopigania
mabadiliko ya sheria ya kupiga kura.

Habar ya hivi punde# wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam wamegoma.soma zaid.

Habar ya hivi punde# wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam wamegoma.soma zaid.


Dar es salaam. Wanafunzi wa chuo kikuu cha
cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma
wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa
ajili ya kujikimu.
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi,
Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni
matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa
zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo
zitatolewa.
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila
baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki
mbili pasipo kupatikana.
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili
kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa
ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.chanzo mwananch.

Monday, May 30, 2016
Polisi mkoan morogoro inamshikilia Diwani kwa ubakaji.sioma zaid.

Polisi mkoan morogoro inamshikilia Diwani kwa ubakaji.sioma zaid.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia
Diwani wa kata ya Mtibwa wilayani Mvomero
(Chadema), Lucas Edward (38) maarufu kwa jina
la Mwakambaya kwa tuhuma za kumbaka binti
wa miaka 14 mkazi wa Turiani wakiwa katika
nyumba ya kulala wageni.
Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linamshikilia Diwani wa kata ya Mtibwa wilayani
Mvomero (Chadema), Lucas Edward (38)
maarufu kwa jina la Mwakambaya kwa tuhuma
za kumbaka binti wa miaka 14 mkazi wa Turiani
wakiwa katika nyumba ya kulala wageni.
Kamanda Ulrich Matei alisema jeshi la polisi
lilipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba
katika nyumba hiyo ya kulala wageni kuna mtu
ameonekana akiwa na binti mdogo ndipo askari
walipofuatilia nyendo zake na kumkamata.
Alisema askari baada ya kufika katika nyumba
hiyo ya kulala wageni ya Baraka walimkuta
mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumbani
na kwamba uchunguzi wa kitabibu unaendelea ili
kubaini uhalisia.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhani alikiri
kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka
sasa hajafahamu kosa alilokamatiwa.

Rais mstaafu wa chadi ahukumiwa jela maisha.soma zaid.

Rais mstaafu wa chadi ahukumiwa jela maisha.soma zaid.

Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre
amehukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika
kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu ,
ubakaji na utumwa wa ngono.
Hissene Habre alihusika moja kwa moja
katika uhalifu huo ambao ulifanyika
wakati akiwa rais wa Chad.
Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama
wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji
Dakar nchini Senegal, walishangilia wakati
jaji alimaliza kusoma hukumu.
Bwana Habre anatuhumiwa kwa
kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati
wa utawala wake miaka ya 80, madai
ambayo ameyakana
Habre alikamatwa nchini Senegal , na
kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.
Chanzo: BBC

Niger uso kwa uso na Boko haramu.soma zaid.

Niger uso kwa uso na Boko haramu.soma zaid.

Utawala nchini Niger unesema kuwa unajiandaa
kuendesha mashambulizi makubwa dhidi ya
wanamgambo wa Nigeria wa Boko Haram.
Akizungumza na BBC waziri wa ulinzi Hassoumi
Massaoudou, alisema kuwa vikosi kutoka kwa
mataifa jirani wamejiandaa vilivyo kukabiliana na
wapiganaji hao wa kiislamu.
Amesema kuwa Niger na washirika wake
wataendesha mashambulizi ndani ya Nigeria.
Chad, Cameroon, Nigeria na Niger wamekuwa
wakishirikiana katika jitihada za pamoja za
kukabiliana na Boko Haram, ambao huendesha
mashambulizi ya mara kwa mara nje ya mipaka
ya Nigeria.

Wanawake wameandamana huko kenya kwa kukosa wanaume.soma zaid.

Wanawake wameandamana huko kenya kwa kukosa wanaume.soma zaid.

Huko Kenya wanawake wa jimbo la Ndeiya
wameandamana kwa kukosa wanaume wa
kuwapa ujauzito. Hali hiyo imesababishwa na
pombe wanazokunywa ambazo hupunguza nguvu
za kiume.
Mmoja wa wanawake hao alisikika akisema
iwapo tabia hiyo ya ulevi itaendelea itawalazimu
kutoka nje ya ndoa zao.chanzo east afrika television.

Spika msitaafu Anna makinda ateuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi NHIF.soma zaid.

Spika msitaafu Anna makinda ateuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi NHIF.soma zaid.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila
kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani
Lila alikuwa Jaji Kiongozi. Uteuzi huu
umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli
amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa
Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni
Spika Mstaafu wa Bunge Ia Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania umeanza tarehe
25 Mei, 2016.
Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali
Mchumo. Katika hatua nyingine, Rais
Magufuli amemteua Prof. Apollinaria
Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam
(Dar es salaam Institute of Technology -
DIT).
Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (SUA) Morogoro. Prof. Pereka
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye
amemaliza muda wake. Uteuzi huu
umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Mchungaji ahukuwa miaka 20 kwenda jela kwa kosa kumubaka mtoto.soma zaid.

Mchungaji ahukuwa miaka 20 kwenda jela kwa kosa kumubaka mtoto.soma zaid.

A pastor earned himself 20 years in
prison for defiling a 13-year-old girl to
"exorcise the demons in her vagina".
Denis Okelo Mateba visited the minor's
home in Khaunga, Kakamega County, on
December 20, 2011 at 3pm in the absence
of her mother who had gone to a funeral
The minor and her cousin, 12, were
preparing a meal when the man of the
cloth came knocking. They were at ease
with him because he had been to their
home on two previous occasions at the
invitation of the 13-year-old minor's
mother for prayers.
The pastor then asked the girl to
accompany him to the main house so
that he could exorcise demons which
were in her vagina. "Come to the main
house I pray for you so that the demons
that were put in your vagina by your
boyfriend may get out," the man said,
according to the minor, who had no
boyfriend then.
They walked out and left the younger girl
in the kitchen. The minor was taken
aback when the pastor demanded that
she undress. The man then gave her a
concoction of herbs which she drank and
lost her senses. When she came to, she
found herself naked, bloodied and lying
on a sack. The girl's cousin told the
court that she peeped through the
window of the main house when she
heard the victim wailing. "I saw the pastor
lying on top of my cousin and when he
saw me, he stood up, zipped his trousers
and left the house to come and talk to
me."
The defiled girl came as the pastor was
speaking to her cousin outside. She
immediately took a bath. The pastor then
ordered the girl to wash the bloodied
clothes of the defiled minor. He ordered
her to follow him to the shop where he
bought birth control pills, which he asked
her to take to the defiled minor and ask
her to take one every morning.
Source: Standard Digital

# Dodoma Bungeni hapatoshi wabunge wa ukawa watoka nje bunge limeahirishwa

# Dodoma Bungeni hapatoshi wabunge wa ukawa watoka nje bunge limeahirishwa

BUNGE la Tanzania limeahirishwa. Ni kutokana
na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kugomewa kuwasilisha hoja
binafsi kuhusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) kusimamishwa, anaandika Faki
Sosi.

Hatua hiyo imetokana na Tulia Ackson, Naibu
Spika kugomea mwongozo uliotolewa na
mbunge kutoka Ukawa kuhusu kujadiliwa
taarifa ya kusimamishwa kwa wanafunzo
kutoka chuo hiko.
Taarifa kutoka bungeni zinaeleza kwamba,
Ackson aligomea taarifa hiyo jambo limezua
mzozo na hatimaye wabunge kuamua kutoka nje
ikiwa ni ishara ya kutoridhika na uamuzi wa kiti
cha spika. Mwanahalisi Online linaendelea
kufuatilia.
Juzi Udom kilitoa taarifa ya kusimamisha
masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi
maalumu ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na
Teknolojia kwa ngazi ya Stashahada na kisha
kutaka waondoke chuoni hapo mara moja.
Tangazo hilo liliwataka wanafunzi hao kuondoka
kati ya juzi na jana saa 12 jioni. Tangazo hilo
lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo
katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao
kurejea majumbani na kwamba wataelezwa
mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Sayansi,
ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Mstaafu,
Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la
walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM
pekee.
Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo
ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na
kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na
serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya
wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St.
Joseph kusimamishwa baada ya kubainika
kutokuwa na sifa za kudahiliwa.chanzo meanahalisonline.

Sunday, May 29, 2016
Watu walioko marekani kinyume na sheria kukiona cha moto kwenye utawara ya Trumpu .soma zaid.

Watu walioko marekani kinyume na sheria kukiona cha moto kwenye utawara ya Trumpu .soma zaid.

Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump,
amehutubia umati wa waendesha pikipiki Jijini
Washington.
Trumph ametoa hotuba hiyo katika
maadhimishoya kuwakumbuka maafisa wa polisi
wa kiume na wa Kike wa Marekani.
Amesema watu walioko Marekani kinyume na
sheria, wanahudumiwa vyema kuliko maveteran
wa kijeshi suala ambalo amesema halitaendelea
katika utawala wake.

Kampuni ya Dangote imetangaza kushusha bei ya saruji yake.soma zaid.

Kampuni ya Dangote imetangaza kushusha bei ya saruji yake.soma zaid.


Kampuni ya saruji ya Dangote imetangaza bei ya
saruji yake kuwa itakuwa Sh 10,000 popote, ikiwa
ni punguzo.
Imesema punguzo hilo linalenga kuongeza
ushindani kwenye soko la bidhaa hiyo nchini na
kuwezesha watanzania wengi kununua
saruji.Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
SadaLadan-Baki, alisema bei ya saruji yao aina
ya 32.5R itauzwa bei hiyo ya Sh 10,000 kwa
mfuko wa kilo 50; na saruji ya 42.5R itauzwa Sh
10,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka kiwandani
mpaka popote itakapouzwa, ikiwemo jijini Dar es
Salaam, ambako bidhaa hiyo inapatikana.Hatua
hii imetajwa kuwa inafanya saruji ya Dangote
kuwa ya bei nafuu kuliko nyingine, ambazo
zinauzwa kati ya Sh 12,500 na Sh 14,000 jijini
Dar es Salaam.Sada alisema hatua hiyo itasaidia
maendeleo ya miundombinu na kutilia mkazo
mpango wa taifa wa kukabili tatizo la makazi
nchini kutokana na takwimu kuonesha hapa
nchini upo uhaba wa nyumba milioni
tatu.“Tunatambua uhitaji mkubwa wa miundo
mbinu bora, na moja ya njia ya kulikabili tatizo
hili ni kumfanya kila mtanzania kuweza kuwa na
uwezo wa kununua rasilimali za ujenzi kwa
kuweka bei mbadala kwa kila Mtanzania,”
alisema Sada.
Uongozi huo wa kampuni ulisema bei hiyo elekezi
kati ya Sh 10,000 na 10,500 imelenga jijini Dar es
Salaam, ambako ndiko kitovu cha biashara,
kinachoangaliwa na wafanyabiashara kutoka
maeneo mbalimbali.

Hiki hapa ni kikosi cha taifa stars kitachoanza leo zidi ya harambe star ya kenya.soma zaid.

Hiki hapa ni kikosi cha taifa stars kitachoanza leo zidi ya harambe star ya kenya.soma zaid.

Harambee Stars v Taifa Stars.
Hiki hapa ni kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza
mechi hiyo itakayochezwa leo Nairobi:
1. Deogratius Munishi 'Dida'
2. Juma Abdul
3. Mohammed Hussein 'Tshabalala'
4. Erasto Nyoni
5. Aggrey Morris
6. Himid Mao
7. Shiza Kichuya
8. Jonas Mkude
9. Mwinyi Kazimoto
10. Elius Maguli
11. Deus Kaseke

Saturday, May 28, 2016
Kampuni yapigwa stopu kuingiza mafuta ya ndege hapa nchini.soma zaid.

Kampuni yapigwa stopu kuingiza mafuta ya ndege hapa nchini.soma zaid.

Serikali imeisimamisha kampuni ya kimataifa ya
Sahara kutojihusisha na zabuni za uingizaji
mafuta yeyote mbaka uchunguzi utakapokalimika
baada ya kubaini imeingiza nchini maelfu ya tani
ya mafuta ya Ndege yaliyochanganywa na petroli
na kuiamuru kuingia gharama kusafisha matank
ya mafuta na kuyaondoa mafuta hayo nchini.
Maamuzi hayo ya serikali yametolewa baada ya
waziri wenye dhamana ya nishati na madini
kutembelea maghara ya makampuni makubwa ya
usambazaji mafuta nchini na kusikia malalamiko
ya uwepo wa mafuta machafu ya Ndege
yaliyongizwa nchini na kampuni hiyo na
kusababisha hasara kubwa.
Malalamiko hayo yalimfanya waziri wa mwenye
dhamana ya nishati na madini Profesa Sospeter
Mhongo kutoa maamuzi ya serikali baada ya
kubaini ukweli kutoka kwa makampuni makubwa
ya usambazaji ambayo yalidai hayawezi
kuyasambaza mafuta hayo ya Ndege na tayari
yanamikataba na mashirika mbalimbali ya Ndege.
Kutokana na maagizo hayo ya serikali Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa serikali wa
ununuzu wa mafuta kwa jumla-PBPA Bwana
Michael Mjinja alielezea namna ya mafuta hayo
yatakavyoondolewa amesema tayari muingizaji
wa mafuta hayo ameingia nchini na
kinachofanyika ni kuangalia namna
atakavyoyaondoa mafuta hayo.

Bwawa la nyumba ya mungu mikoa ya kilimanjaro na manyara limefungwa kujihusisha na uvuvi.soma zaid.

Bwawa la nyumba ya mungu mikoa ya kilimanjaro na manyara limefungwa kujihusisha na uvuvi.soma zaid.

Mwanga. Serikali imesitisha kwa mwaka mmoja
shughuli za uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu linalotegemewa na wavuvi wa mikoa
miwili ya Kilimanjaro na Manyara kutokana na
kukithiri kwa uvuvi haramu.
Kufungwa kwa bwawa hilo ambalo sasa samaki
wanaovuliwa ni wadogo, kutakuwa na athari za
kiuchumi si kwa wavuvi tu, bali pia
wafanyabiashara na walaji.
Uamuzi wa kufungwa kwa bwawa hilo
linalotegemewa na wananchi wa vijiji vya Wilaya
za Mwanga na Moshi mkoani Kilimanjaro na
Simanjiro mkoani Manyara ulitangazwa na
Serikali juzi.
Akitangaza maazimio 14 ya wadau wa bwawa
hilo waliokutana Mwanga, Katibu Tawala (Ras)
wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi alisema
bwana hilo litafungwa kuanzia Julai Mosi hadi
Juni 2017.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mkuu wa
Mkoa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki na wa
Manyara, Joel Bendera, wadau walikiri hali ni
mbaya katika bwawa hilo kutokana na uvuvi
haramu.
Uvuvi huo haramu umesababisha samaki
wanaovuliwa kushuka kutoka tani 25,000 mwaka
1970 hadi tani 11 mwaka 2016. Taarifa zinasema
kiwango kimekuwa kikishuka taratibu kuanzia
mwaka 1973.
Maswi alisema katika maazimio hayo, viongozi
wa vijiji na kata wakishirikiana na vyombo vya
ulinzi na usalama, wametakiwa kuwabaini
wanaomiliki nyavu aina ya makokoro ifikapo Juni
30 mwaka huu.
Kadhalika, Serikali imetoa muda wa mwezi
mmoja hadi kufikia Juni 30 wamiliki wote wa
makokoro kuyasalimisha kwa hiyari kwa vyombo
vya dola na kwamba wasiofanya hivyo
watakamatwa.
Chini ya maazimio hayo, wavuvi wote
watakaosalimisha makokoro hayo kwa hiyari,
watasainishwa mkataba wa kutorudia tena kuvua
kwa kutumia nyavu hizo na wakirudia
watafikishwa kortini.
Akizungumza katika mkutano huo, Bendera
alisema katika kipindi hicho cha mwaka mmoja,
Serikali haitaruhusu aina yoyote ya uvuvi na
mvuvi atakayeonekana ndani ya bwawa hilo
atakamatwa.
“Mvuvi yeyote atakayeonekana ndani ya Bwawa
la Nyumba ya Mungu atakamatwa. Ni lazima
tukubali kunywa dawa chungu ya mwaka mmoja
lakini tupate samaki wakubwa baadaye,” alisema
Bendera.
Akisisitiza, Sadiki alivitaka vyombo vya ulinzi na
usalama kuhakikisha vinasajili mitumbwi yote
itakayoruhusiwa kuingia ndani ya bwawa baada
ya kufunguliwa Julai 2017.
Baadhi ya wananchi wanaotegemea uvuvi
kujikimu kimaisha, walisema hatua hiyo
itawaathiri kimaisha kwa kuwa bwawa hilo ndilo
shamba lao lakini wanaafiki uamuzi wa Serikali.

Uhasama wa korea kaskazini na korea kusini umechukua sura mpya.soma zaid.

Uhasama wa korea kaskazini na korea kusini umechukua sura mpya.soma zaid.


Korea Kaskazini inasema itashambulia meli
yoyote kutoka Korea Kusini, itakayovuka mpaka
wa baharini kati ya mataifa hayo mawili
unaozozaniwa.
Onyo hilo linajiri baada ya Korea Kusini
kushambulia meli mbili za Korea Kaskazini
zilizovuka mpaka wake kwa muda mfupi.
Pyongyang imetaja shambulizi hilo kama uchokozi
wa kijeshi, lengo likiwa kusababisha hali ya
wasiwasi..
Mapema mwezi huu ,Korea Kusini ilikataa wito
wa Korea Kaskazini,ikisema kwamba lazima
Pyongyang ichukue hatua kusitisha mpango wake
wa nuklia kwanza.

Bidhaa za magendo zakamatwa na TRA mkoani kilimanjaro.som zaid.

Bidhaa za magendo zakamatwa na TRA mkoani kilimanjaro.som zaid.

Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Kilimanjaro
imekamata bidhaa kutoka nje za mamilioni ya
fedha baada ya kuvushwa kwa njia ya magendo
katika maeneo ya Kitobo, Kileo na Njiapanda
zikisafirishwa kwa njia ya magari mawili na
pikipiki tano.
Meneja wa TRA wa mkoa huo Bw. Abdul
Mapembe ameiambia ITV kuwa, katika
oparesheni hiyo ya kudumu wameyakamata
magari mawili moja likiwa na usajili wa kenya
likiwa na bidhaa hizo vikiwemo vifaa vya magari,
televisheni. Pikipiki, simu za mkononi, nguo,
mafuta ya taa, chumvi na sukari.
Bw.Mapembe amesema, wafanyabiashara wa
bidhaa hizo baada ya kukamatwa walitakiwa
wakalete vielelezo vya bidhaa zao kama
wamezilipia ushuru mpakani kama walivyodai
lakini hawajaonekana.
Kiongozi wa oparesheni hiyo Bw. Obednego
Nicholaus amewaonya wenye magari na pikipiki
hizo kuwa kama hawatajitokeza kulipia ushuru
bidhaa zitataifishwa pamoja na magari hayo aina
ya fuso na pikipiki.chanzo itv

Afisa mtendaji na mwenyekiti wa kijiji wilayini songwe watiwa mbaloni kwa ubadhilifu.soma zaid.

Afisa mtendaji na mwenyekiti wa kijiji wilayini songwe watiwa mbaloni kwa ubadhilifu.soma zaid.

Mwenyekiti na Afisa mtendaji wa kijiji cha
Mkwajuni wilayani Songwe, wanashikiliwa na
jeshi la polisi, baada ya wananchi kuwatuhumu
kwa kutafuna zaidi ya shilingi milioni 12 mali ya
kijiji hicho pamoja na kushindwa kusoma mapato
na matumizi ya kijiji kwa zaidi ya miezi tisa.
Wananchi walionyesha furaha yao, wakishangilia
hatua ya viongozi wao kupelekwa mahabusu
baada ya kufanyika mkutano wa hadhara ambao
wananchi hao waliutumia kuazimia viongozi hao
wakamatwe kwa tuhuma za kufanya ufisadi wa
zaidi ya shilingi milioni 12 za ushuru wa minara
ya simu iliyopo kijijini hapo.
Wakiijitetea kwenye mkutano huo, Afisa mtendaji
wa kijiji hicho Severio Malyagila amezikana
tuhuma hizo, kwa madai kuwa fedha hizo
zilitumika kwa idhini ya halmashauri ya kijiji
Hata hivyo wananchi hao hawakuridhishwa na
maelezo ya Afisa mtendaji, na baada ya mjadala
mrefu ndipo mwenyekiti wa muda wa mkutano
huo, akatoa azimio kwa niaba ya wananchi,
maazimio ambayo jeshi la polisi likaanza
kuyatekeleza papo hapo kwa kuwakamata
watuhumiwa.

Thursday, May 26, 2016
Mgombea Urais Marekani Donard Trump Akosolewa.soma zaid.

Mgombea Urais Marekani Donard Trump Akosolewa.soma zaid.

Rais wa Marekani Barack Obama amasema kuwa
viongozi duniani wana sababu ya kukasirikia
matamsha yanayotolewa na mgombea urais wa
chama cha Republican Donald Trump.
Akiongea pembezoni mwa mkutano wa mataifa
tajiri zaidi duniani ya G7 nchini Japan, Obama
alisema kuwa Trump ameonyesha tabia ya
kupuuza masuala ya dunia.
Obama amesema kuwa viongozi wa kigeni
wameshangazwa na uteuzi wake. Hata hivyo
Trump hajasema lolote kuhusu matamshi hayo ya
Obama
Rais Obama pia alipuzilia mbali wasi wasi wa
chama cha Democratic kuhusu mvutano uliopo
kati ya Hillary Clinton na Bernie Sanders.
Obama amesema moja ya tofauti kubwa kati ya
chama cha Democratic na Republican mwaka
huu, ni kwamba wagombea wa Democratic
hawatofautiani sana katika sera zao.
Baada ya washindani wake Trump kwenye uteuzi
wa cha Republican kujiondoa kutoka kwa
kinyanganyiro, sasa anabakisha kura chache za
kumwezesha kupata wajumbe 1,237, anaohitaji ili
kuwa mgombea wa chama cha Republican
kwenye uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba

Kundi la wanamgambo boko haramu wamelipua kiwanda cha mafuta Nigeria.soma zaid.

Kundi la wanamgambo boko haramu wamelipua kiwanda cha mafuta Nigeria.soma zaid.


Kiwanda cha mafuta cha kampuni ya Chevron
nchini Nigeria kimeshambuliwa na
wanamgambo.
Kampuni hiyo ya Marekani inaripotiwa kufuta
shughulia zake kufuatia uvamizi huo.
Kundi linalojiita Niger Delta Avengers, lililisema
kuwa lililipua kituo cha umeme huku wenyeji
wakisema kuwa walisikia mlipuko.
Avengers wanasema kuwa wako kwenye kampeni
ya kutaka wenyeji wa Niger Delta kupata mgao
wa utajiri wa mafuta.
Mauzo ya mafuta yasiyosafishwa yanachangia
asilimia sabini ya pato la taifa nchini Nigeria,
nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Rais magufulia awapa somo makandarasi.soma zad.

Rais magufulia awapa somo makandarasi.soma zad.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo
wakati akifungua Mkutano wa
Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa
Makandarasi (CRB) uliofanyika jijini DSM
“Nawatolea mfano idara ya mahakama,
imetangaza kujenga mahakama za
mwanzo na za wilaya, kwenye bajeti wana
shilingi bilioni 24, makadirio ya kitaalam
yanaonyesha kila jego lisizidi milioni 200,
wakandarasi wazalendo walipoomba
katika nyaraka zao wametaka jengo
lijengwe kwa bilioni 1, sasa nakuuliza
Mheshimiwa Mwenyekiti na ndugu
wkandarasi, hata kama upendeleo,
upendeleo huo utapasua moyo”.
MKWEPA KODI

Wananchi wa jamhuri ya congo waandamana kumpinga rais joseph kabira.soma zaid.

Wananchi wa jamhuri ya congo waandamana kumpinga rais joseph kabira.soma zaid.

Maandamano ya upinzani yanafanyika nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga
uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema
mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia
madarakani baada ya mda wake kukamilika
iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa
mwaka huu.
Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika
maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi
nyumbani kwa mgombea wa urais wa Upinzani
Moise Katumbi.
Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa
mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma
ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa
likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma
ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa
kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi
watu wameshindwa kwenda kazini.
Mjini Goma katika eneo la Birere,amesema kuwa
ni mchezo wa paka na panya ambapo vijana
wamekuwa wakijibizana na polisi kwa kuwarushia
mawe huku nao maafisa hao wakiwatupia vitoa
machozi.
Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa
na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa
polisi.

Mtoto wa Rais yoweri mseveni ameapishwa rasimi kuwa meja jeneral.soma zaid.

Mtoto wa Rais yoweri mseveni ameapishwa rasimi kuwa meja jeneral.soma zaid.

Meja Jenerali,Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa
kiume wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Shirikisha
Mkuu wa kikosi maalum cha uongozi katika jeshi
la Uganda, Brigedia Muhoozi Kainerugaba
ameapishwa rasmi katika nafasi ya Meja Jenerali
wakati wa sherehe ambazo zilifanyika katika
wizara ya ulinzi katika mji mkuu Kampala.
Kikosi maalum cha uongozi kinahusika kumlinda
rais pamoja na mafuta na taasisi nyingine nchini
humo. Kainerugaba ambaye ni mtoto wa kwanza
wa kiume wa Rais Yoweri Museveni alipandishwa
cheo pamoja na maafisa wengine.
Kupandishwa kwake cheo kumechochea shutuma
kwenye mitandao ya kijamii nchini uganda huku
wakosoaji wakidai kuwa ni sehemu ya mpango
wa Rais Museveni kutaka kumsimika mtoto wake
kuwa mrithi wake. Jenerali muasi katika jeshi,
David Sejusa, mratibu wa zamani wa idara za
upelelezi za Uganda katika ofisi ya rais alitoa
shutuma hizo alipozungumza na mwandishi wetu.

Wavuvi wagoma mwanza kisa wananyanyaswa na mabosi wao.

Wavuvi wagoma mwanza kisa wananyanyaswa na mabosi wao.

Zaidi ya wavuvi 1,000 wa kisiwa cha Kasarazi
wilaya ya Sengerema mkoani
mwanza,wamegoma kufanya kazi kwa siku ya
nne mfululizo wakipinga vitendo vya
unyanyasaji,ikiwemo kunyimwa chakula
vinavyodaiwa kufanywa na wamiliki wa
mitumbwi,huku uongozi wa serikali wilayani humo
ukilalamikiwa kwa kufumbia macho vitendo hivyo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Katibu wa umoja huo wa wavuvi wapatao 1,165
waliopo katika kisiwa cha Kasarazi halmashauri
ya wilaya ya Buchosa Boniphace Mgeta
amesema wameamua kugoma kuingia ziwani
kuendelea na shughuli zao za uvuvi kwa madai
ya kunyanyaswa na matajiri hao,huku mkuu wa
wilaya hiyo Zainab Talack akishindwa kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo licha ya kukutana na
pande hizo mbili ofisini kwake .
Uongozi wa wamiliki wa vyombo vya uvuvi wa
kisiwa hicho cha Kasarazi kilichomo ndani ya
Ziwa Victoria, kupitia kwa katibu wao Msilikale
Juma amesema chanzo cha mgogoro huo
ulioanza kufukuta kuazia mwezi Aprili mwaka huu
ni hujuma inayodaiwa kufanywa na baadhi ya
wavuvi wasio waaminifu na kusababisha hasara
ya mamilioni ya shilingi kwa wamiliki wa vyombo
vya uvuvi.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Zainab talack
akizungumza kwa njia ya simu kutokea
wilayani Sengerema amekiri kuutambua mgogoro
na kuzitaka pande zote mbili kukaa chini na
kufanya mazungumzo yenye lengo la kufikia
mwafaka.chanzo itv

Wednesday, May 25, 2016
Wewe mwananch unaamini huyu waziri magembe ni mzigo na ni mwepesi kama tishu?

Wewe mwananch unaamini huyu waziri magembe ni mzigo na ni mwepesi kama tishu?

Dodoma. Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema),
Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni
baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na
Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na
mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo
wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika
wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na
hifadhi za Taifa.
“Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema
(Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni
mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii
nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati
akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na
Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba
mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo
kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa
mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge
aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha
aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya
alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge
hawaamuliwi maneno ya kutumia.
Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta
neno hilo na katika mabishano hayo yaliyodumu
kwa dakika tatu, baadaye, Bulaya alikubali
kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha neno mwepesi
na kuruhusiwa kuendelea kuchangia.
“Mwenyekiti sitafuta neno mwepesi, kama neno
‘tishu’ linawakera basi naliondoa libaki mwepesi,”
alisema Bulaya.
Katika mchango wake, Bulaya alisema wananchi
wanaoishi katika hifadhi zilizopo jimboni mwake
wananyanyaswa na askari wanyamapori wakati
Serikali imeshindwa kuwatengenezea mazingira
mazuri ya kuishi.
Alimtaka waziri huyo kushughulikia kero zote
zinazowakabili wananchi wa Bunda akisema
Serikali haiendeshwi kwa maneno matupu, bali
vitendo na dhamira ya dhati ya kuwahudumia
wananchi.
“Tatua matatizo jimboni kwangu ili niweze
kukupima kama wewe ni mzito au mwepesi,”
alisema mbunge huyo akimwambia Profesa
Maghembe.
Baada ya Bulaya kumaliza muda wake, mbunge
aliyefuatia alikuwa Abdallah Ulega wa Mkuranga
(CCM) ambaye alisema kuna haja ya wabunge
kupimwa kama wamelewa getini ili kujua akili
zao.
“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi kumtukana
mzee kama yule (Maghembe). Kama suala ni
uwaziri basi aangalie hata umri wake kabla ya
kuzungumza... Naungana na aliyesema wabunge
tupimwe vilevi kabla hatujaingia humu ndani.
Unaweza kujenga hoja yako bila kutukana,
huhitaji kutukana ili waziri atekeleze madai
yako,” alisema mbunge huyo.chanzo mwananch.

Watanzia 8 waliotaka kujiunga na Al- shabab wakatwa kenya.soma zaid.

Watanzia 8 waliotaka kujiunga na Al- shabab wakatwa kenya.soma zaid.

Serikali ya Kenya imefichua kwamba
imewakamata raia wanane wa Tanzania
waliokuwa katika harakati za kujiunga na kundi la
wapiganaji la al-Shabab nchini Somalia.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya
habari, polisi wanasema raia hao waliokamatwa
katika kipindi cha miezi miwili iliopita walikiri
kuwa mbioni kujiunga na kundi hilo la ugaidi.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la
watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu
kuweka video mtandaoni likidai uwepo wa
wapiganaji wa Kiislamu nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa
wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na
barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na
kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika
Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Mkuu wa polisi Kenya amesema polisi pia
wametibua shambulio la Islamic State
Polisi wa Kenya pia wanasema wamefanikiwa
kutibua njama ya wanachama wa kundi linalojiita
Islamic State ya kutekeleza mashambulio nchini
humo na kuwakamata washukiwa wawili.
Wawili hao Kiguzo Mwangolo Mgutu na Abubakar
Jillo Mohammed walipewa mafunzo ya kuwa na
itikadi kali kabla ya kuingizwa katika kundi la IS
na Mohammed Ali aliyekamatwa awali na
ambaye anasaidia polisi na uchunguzi, polisi
wamesema.
Kulingana na taarifa hiyo, kufuatia kukamatwa
kwa Mohammed Ali, wafuasi wake wamekuwa
wakipanga kufanya mashambulizi ya kulipiza
kisasi sana wakilenga sekta ya uchukuzi wa
abiria.
Kukamatwa kwa wawili hao, kumezuia kutokea
kwa mashambulio katika miji ya Nairobi na
Mombasa.chanzo star vt.

Hakuto kuwa na chakula cha msaada ni wapi? Soma zaid.

Hakuto kuwa na chakula cha msaada ni wapi? Soma zaid.


Mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo
akiongea na wananchi wilaya ya Bunda
amesema hakutakuwa na chakula cha
msaada bali wanatakiwa walime, na kila
mwananchi alime ekari kuanzia mbili za
mihogo.
Na yeyote atakayeonyesha kulia kuwa ana
njaa watampeleka jela ambako
kunapatikana chakula cha bure.
Pia amesema kucheza pool table ni
marufuku, na atakeyekunywa bia kabla ya
saa kumi na nusu jioni atakamatwa.

Tuesday, May 24, 2016
Kutoka zanzibar hatutishwi na misaada ya wahisani.soma zaid

Kutoka zanzibar hatutishwi na misaada ya wahisani.soma zaid


BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kutobabaishwa na baadhi ya washirika wa
maendeleo waliotishia kususa misaada kwa
malengo ya kisiasa.
Wamesema kwa nyakati tofauti katika vikao vya
baraza hilo vinavyoendelea mjini hapa kuwa, ni
bora kula mihogo na sembe kuliko kupokea
misaada yenye masharti ya kudhalilisha.
Mwakilishi wa Uzini, Mohamed Raza (CCM)
alisema hatua ya kusitishiwa misaada kutoka
nchi washirika wa maendeleo kwa Zanzibar si
mara ya kwanza.
Alikumbusha kuwa wakati wa uongozi wa Rais Dk
Salmin Amour (Komandoo) mara baada ya
kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa
mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, suala hilo
lilitokea.
Alisema Dk Amour alizuiliwa misaada kutokana
na washiriki wa maendeleo kutokubaliana na
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 uliofanyika kwa
madai kwamba haukuwa huru na haki ambapo
CUF ilishindwa na CCM.
“Mwaka 1995 mara baada ya kumalizika kwa
uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama
vingi Dk Salmin aliwekewa vikwazo na nchi
washiriki wa maendeleo kwa madai kwamba
uchaguzi haukuwa huru na haki. Lakini nchi
ilikwenda na kutekeleza miradi yake yote ya
ndani kwa kutumia rasilimali zake,” alifafanua
Raza.
Akitoa mfano, Raza alisema katika kipindi hicho
miradi ya ujenzi wa nyumba za maendeleo
zilizopo Michenzani ulifanyika na kukamilika kwa
ghorofa moja lililopo jirani na kituo cha Polisi
Madema kwa kutumia fedha za ndani
zinazotokana na makusanyo ya kodi.
Naye Mwakilisi wa Tunguu, Simai Mohamed Said
alisema huu ni wakati muafaka kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kujikita zaidi katika
kutumia rasilimali zake kwa ajili ya kuongeza
pato la taifa. Alisema taasisi zinazoshughulikia
utalii hawajaitangaza vizuri Zanzibar katika
ramani ya dunia, kwa hivyo sekta hiyo
haijatumiwa vizuri katika kuingiza pato la taifa.
Alisema sekta ya utalii inaingiza fedha za kigeni
kwa asilimia 46 na pato la taifa kwa asilimia 68
kwa hivyo ni wajibu wa taasisi zinazoshughulikia
kuitangaza Zanzibar kufanya kazi hiyo kwa
kutumia matamasha ya nje ya kimataifa.
“Miongoni mwa njia za kuifanya Zanzibar
kujitegemea na kuacha kupiga magoti kwa
washiriki wa maendeleo ni kutumia rasilimali
zake za ndani ikiwemo sekta ya utalii ambayo ni
tegemeo katika kuingiza fedha za kigeni,”
alisema Raza.

Naibu katibu mkuu wa FIFA ametimuliwa kwa kosa la ufisdi.soma zaid.

Naibu katibu mkuu wa FIFA ametimuliwa kwa kosa la ufisdi.soma zaid.


Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu
katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na
ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya
dola.
Kattnet raia wa Ujerumani mwenye umri wa
miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya
aliyekua katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi
kutokana na kashfa za rushwa.
Kufutwa kazi kwa kiongozi huyu kulikuja mara
moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa
kugundua kulikua na ukiukwaji na uvunjaji wa
majukumu yake.
Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha
mapungufu katika majukumu yake kwa kutumia
pesa za ziada ambazo waliamua kiasi gani rais,
katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.chanzo bbc swahil.

Wabunge wampa mbinu waziri jinsi ya kuondoa migogoro ya ardhi nchini.soma zaid.

Wabunge wampa mbinu waziri jinsi ya kuondoa migogoro ya ardhi nchini.soma zaid.


WABUNGE wameitaka serikali kuweka mkazo
katika kuhakikisha ardhi yote nchini inapimwa.
Pia, wametaka kuwepo na programu ya kupima
ardhi nchi nzima na kuwauzia wananchi, jambo
litakalosaidia kuondoa migogoro ya ardhi.
Wametaka suala la upimaji kutoachwa kwa sekta
binafsi, ambayo kwa mujibu wa wabunge, ina
gharama kubwa; badala yake, serikali ijiwekee
mkakati wa kupima angalau mikoa miwili kila
mwaka.
Aidha, wabunge wameyashukia mabaraza ya
ardhi huku wakikosoa kutumia watu wasio na
taaluma ya sheria katika kuamua kesi. Walitoa
maoni hayo jana wakati wakichangia mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi.
Walisisitiza umuhimu wananchi kupimiwa ardhi
na kupatiwa hati. Walia upimaji ardhi Mbunge wa
Mbinga, Sixtus Mapunda (CCM), alisema kuwe na
programu maalumu ambayo serikali itakuwa na
vifaa vya upimaji nchi nzima na kupima ardhi
yote ; na pale mwananchi anaponunua ardhi
anakuta eneo limepangwa.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu
wa kupima kwa gharama kubwa na wakati huo
huo kukabili migogoro ya ardhi. Alitoa mfano wa
Jiji la Dar es Salaam, ambalo serikali inakabiliwa
na usumbufu wa kulipanga.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary
Mgumba (CCM) aliunga mkono umuhimu wa
kupima maeneo yote, kuondoa utata na kumaliza
migogoro ya ardhi. Mwingine aliyehimiza upimaji
wa maeneo yote ni Mbunge wa Viti Maalumu,
Cecilia Paresso (Chadema ) ambaye alishauri
wananchi wapimiwe maeneo kwa kuwakopesha
kisha walipe madeni hayo taratibu.
Alisema kwa kufanya hivyo serikali mbali na
kuondoa migogoro ya ardhi, pia itaingiza kipato
kutokana na wananchi kulipia hati. Wakosoa
mabaraza Wakati huo huo katika kuchangia,
baadhi ya wabunge wametaka kazi za kiutendaji
katika masuala ya ardhi zifanywe na wataalamu
wa ardhi ; na serikali iachane na utaratibu wa
sasa wa kuwapa kazi watu kiholela.
Walitaka mabaraza ya ardhi yasimamiwe na
wataalamu wa ardhi, badala ya kuchukua watu
wasio na taaluma. Mbunge wa Manyoni
Mashariki, Daniel Mtuka (CCM), alieleza
kushangazwa na kitendo cha serikali kukabidhi
jukumu kubwa la usuluhishi wa masuala ya ardhi
kwa watu ambao hawajasoma na hawajui sheria
za ardhi.
Alisema, wapo wataalamu wengi nchini ambao
wamekwenda kusomea masuala ya ardhi
wanaotakiwa kufanya kazi hiyo, lakini wamekuwa
wakitumiwa watu maarufu vijijini kufanya kazi
hiyo.

Kesi ya uchaguzi aliyoifungua jerry slaa kuendelea leo.soma zaid.

Kesi ya uchaguzi aliyoifungua jerry slaa kuendelea leo.soma zaid.


Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2015 aliifungua
Novemba, mwaka jana dhidi ya mbunge huyo,
msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ukonga na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akipinga
ushindi wa mbunge huyo.
Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania,
Kanda ya Dar es Salaam, leo, inatarajia kutoa
uamuzi wa kupokea au kutopokea kiapo cha
ushahidi katika kesi ya kupinga matokeo
iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa
Ukonga, Jerry Silaa (CCM) dhidi ya mbunge
Mwita Waitara (Chadema).
Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2015 aliifungua
Novemba, mwaka jana dhidi ya mbunge huyo,
msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ukonga na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akipinga
ushindi wa mbunge huyo.
Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata aliiomba
Mahakama kutopokea hati ya kiapo hicho
kilichowasilishwa na Silaa akiongozwa na wakili
wake, Dk Masumbuko Lamwai kutokana na
kukosewa.
Wakili Malata akishirikiana na Dk Onesmo Kyauke
waliweka pingamizi hilo kwa kuwa kiapo hicho
kimekiuka matakwa ya sheria kwa kuwasilisha
nakala halisi zote badala ya nakala iliyotokana na
nakala halisi.
Jana, Mahakama ilipanga kuanza kusikiliza kesi
hiyo na Silaa alitarajiwa kutoa ushahidi wake
mbele ya Jaji Fatuma Masengi.

Monday, May 23, 2016
Taifa linapateza nguvu kazi ya vijana kutoka na matumizi ya madawa ya kulevya.soma zaid.

Taifa linapateza nguvu kazi ya vijana kutoka na matumizi ya madawa ya kulevya.soma zaid.


Serikali imefanikiwa kukamata takribani
kilo 139.69 za dawa za kulevya ikiwemo
kilo 53.49 za Heroin, Cocaine kilo 86.2
kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka
huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya
habari kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti
wa Dawa za Kulevya iliyotolewa na Mkuu
wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu
wa tume hiyo, Amani Msami, pia tume
hiyo imekamata tani 97 za bangi na
mirungi.
Alisema mbali na kukamata kilo hizo,
takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa
Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya
200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya
hao 30,000 hutumia dawa hizo kwa njia
ya kujidunga sindano.
“Serikali imefanikiwa kukamata takribani
kilo 53.49 Heroin, Cocaine kilo 86.2
kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka
huu” alisema Msami na kuongeza kuwa:
“Watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa
kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000
ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa
hiyo kwa njia ya kujidunga”.Msami
alifafanua kuwa mbali na kukamata dawa
hizo, tume hiyo ilikamata tani 81.3 za
bangi na Mirungi tani 15.7.
Aliongeza kuwa mbali na hayo idadi ya
watuhumiwa waliyokamatwa wakijihusisha
na usafirishaji wa dawa za kulevya
zikiwemo Bangi,Mirungi, Heroin na
Cocaine walikuwa 14,503.Hata hivyo,
alisema takwimu hizo zinaonyesha jitihada
za serikali katika kukabiliana na biashara
ya dawa za kulevya nchini na si ukubwa
wa usafirishaji wa Heroin na Cocaine
nchini.
“Moja ya jitihada za Serikali katika
kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya
ni kutungwa kwa Sheria ya kudhibiti na
kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya
mwaka 2015.” Alisema Msami.
Alifafanua kuwa sheria hiyo imeweka
adhabu kali kwa makosa ya kujihusisha
na matumizi na biashara ya dawa ya
kulevya ikiwemo kifungo cha maisha kwa
yeyote atakayesafirisha dawa za kulevya.

Tibaijuka yamkuta tena.soma zaid.

Tibaijuka yamkuta tena.soma zaid.


Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa
Anna Tibaijuka na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk
Charles Mlingwa wamelipuliwa bungeni
wakidaiwa kudaiwa kutumia madaraka yao
vibaya.
Tuhuma hizo zilitolewa jana na wabunge wa
upinzani Conchesta Rwamlaza (Viti Maalum -
Chadema) na Dk Godwin Mollel (Siha - Chadema)
walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Rwamlaza alidai kuwa katika Kijiji cha Kamwila
wilayani Muleba, Profesa Tibaijuka akiwa
serikalini, aliomba eka 1,098 lakini hivi sasa
anamiliki eka 4,000 jambo ambalo linazua
mgogoro na wananchi.
“Hili linaleta matatizo kwa kuwa haiwezekani mtu
awe na eneo hilo lote halafu anakodisha kwa
wananchi,” alisema Rwamlaza.
Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo
na kama Profesa Tibaijuka aliomba heka 1,098
apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizonazo hivi
sasa.
Dk Mollel alimtaka Waziri Mkuu amhamishe Dk
Mlingwa akidai ni tatizo katika wilaya hiyo.
Alisema juzi ulitokea mgogoro kati ya wananchi
wa Arumeru na Siha katika mpaka jambo
lilisababisha kubomoleana nyumba.
“Mkuu wa Wilaya alifika pale akiwa amelewa na
kusababisha wananchi kuchukua hatua hizo
wakati ilitakiwa tu tutumie akili,” alisema Dk
Mollel.
Dk Mollel alisema kama DC huyo ataendelea
kuwa na tabia hiyo, migogoro haitaisha na
wawekezaji hawatawaheshimu wananchi kwa
kuwa kiongozi wao anawaaibisha.
“Kama hamtamtoa huyu DC ambaye anatuaibisha
kwa kuomba vitu vidogovidogo kwa wawekezaji
basi sisi tutamtoa kwa kuwa hatuhitaji aibu.”
Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo
na kama Profesa Tibaijuka aliomba eka 1,098
apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizo nazo
hivi sasa.
Dk Mlingwa ajibu tuhuma
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Mlingwa alisema
tangu kipindi cha kampeni, mbunge huyo alikuwa
akimshambulia kwa maneno ya uongo ili kupata
kura za huruma.
“Hata hii leo (jana) asubuhi alinitumia meseji
akisema ooh nakwenda kukushtaki kwa Rais na
Waziri Mkuu, akaweka na maneno ya vitisho mimi
nikamwambia nenda kwa vile yote ni uongo,”
alisema.
“Nadhani kwa sababu ya ahadi za uongo
alizokuwa nazo kuwa akichaguliwa yeye
mashamba yote ya wawekezaji yaliyoko Siha,
yatakuwa mikononi mwa wananchi jambo ambalo
haliwezekani.”
Dk Mlingwa alisema wawekezaji hao wana hati
za kumiliki mashamba hayo na hilo ndilo ambalo
Serikali imekuwa ikiwaeleza wananchi ukweli ili
kuepuka propaganda za uongo za mbunge.
“Hiyo ndiyo imemfanya aendelee kumsema
vibaya mkuu wa wilaya na mkurugenzi katika kila
nafasi anayoipata hata hayo aliyoyasema bungeni
ameniambia kwa meseji leo atayasema,” alisema.
“Mkuu wa wilaya kwa bahati nzuri hawezi
kujificha tabia na matendo yake kama ningekuwa
mlevi wananchi wangeshasema.”
Wabunge wamvaa Lukuvi
Wabunge wamemshushia ‘zigo’ la migogoro ya
ardhi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi wakimtaka atatue
migogoro hiyo kwa kasi ambayo ameanza nayo.
Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, jana,
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema),
Joshua Nassari alizungumzia mgogoro wa ardhi
katika Wilaya ya Arumeru na kusema mgogoro
huo umekuwapo tangu mwaka 1993.
Nassari alinukuu tangazo katika gazeti la Serikali
na kusema Rais alitangaza kufuta umiliki wa
shamba hilo. Hata hivyo, alisema mwekezaji huyo
aliendelea kumiliki shamba hilo na kuwakataza
wananchi kulima.
“Huyu Mzungu ni nani? Kwa nini anakuwa na
nguvu kuliko Serikali? Rais alitangaza kufuta
umiliki wa shamba hilo tangu mwaka 1993, lakini
mpaka leo anaendelea kumiliki eneo hilo wakati
halitumii,” alisema.
Alisema wananchi wanapodai ardhi yao
wanafunguliwa kesi za kusingiziwa na kufungwa.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Bupe
Mwakanata alimtaka waziri Lukuvi kushughulikia
mgogoro wa shamba la Efatha, uliodumu kwa
muda mrefu bila kutatuliwa.
“Serikali iwasaidie wananchi wake kwa
kuwarudishia ardhi yao ambayo haitumiki
kikamilifu. Wananchi wa eneo hilo wanategemea
kilimo, ukiwanyang’anya ardhi unawasababishia
ugumu wa maisha,” alisema.
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini
alizungumzia mgogoro katika eneo linalozunguka
Ziwa Chala. Alisema eneo hilo amepewa
mwekezaji ambaye anawazuia wananchi kutumia
maji na kusababisha mgogoro kati ya wananchi
na mwekezaji na kati ya wananchi na Serikali.
“Ziwa Chala ndiyo pekee ambalo asilimia 85 ya
maji yake ni safi na salama na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam wako pale kufanya utafiti.
Tunaomba umalize mgogoro huo, ili wananchi
watumie ziwa hilo na ardhi kwa ajili ya kilimo,”
alisema Selasini.
Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso
alisema Mkoa wa Katavi una migogoro mingi
ambayo inasababishwa na mipaka kati ya vijiji
hivyo na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Alisema vijiji vya Kapanga, Lugonesi, Kabage na
Nkungwi vinakabiliwa na mgogoro ya ardhi
ambayo inawafanya wananchi wa maeneo hayo
kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.
“Ninaomba wakati waziri anashughulikia
migogoro ya ardhi atuangalie na sisi mikoa ya
pembezoni. Tuna migogoro mingi ambayo
haijapatiwa ufumbuzi na Serikali haijafanya
jitihada zozote,” alisema.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM),
Omary Mgumba alisema kumekuwa na mgogoro
kati ya Mkoa wa Morogoro na Pwani kwenye vijiji
vya mpakani.
Alimtaka Waziri Lukuvi kutembelea eneo hilo ili
mgogoro uishe na wananchi wafanye kazi ya
uzalishaji.
Mbunge wa Karatu (Chadema), Willy Quambalo
alisema kuna mwekezaji katika wilaya hiyo
ambaye amepewa ekari 3,850 huku wananchi
wakipata shida kwa sababu ameziba njia ambayo
inapita katika eneo hilo.
Lukuvi amtaja Lowassa bungeni
Waziri Lukuvi amemgonganisha Mbunge wa
Monduli, Julius Kalanga na mtangulizi wake
Edward Lowassa, kuhusu shamba la Makuyuni
lililopo jimboni humo.
Lukuvi alifanya hivyo wakati akitoa majibu ya
hoja mbalimbali za wabunge kuhusu hotuba ya
bajeti yake, lakini Kalanga katika mchango wake
alilalamikia kuchelewa kwa utekelezaji wa
uamuzi wa Serikali wa kurejesha mashamba
makubwa kwa wananchi, likiwamo la Makuyuni.
Akijibu hoja hilo, Lukuvi alimwambia Kalanga
kuwa shamba hilo la Makuyuni litarudishwa kwa
wananchi, lakini itakula kwake kwa kuwa liko kwa
Lowassa.
“Rais Mkapa (Benjamin) aliamua shamba hilo
lirudi kwa wananchi na Lowassa ndiye aliyesaini
hati ya shamba hilo,” alisema Lukuvi.
Alisema kuwa atahitaji ushirikiano wa Kalanga na
halmashauri ya Monduli, kulikabidhi shamba hilo
kwa wananchi.
Wakati huo huo, Lukuvi amepiga marufuku watu
wote wenye mashamba makubwa ambao
wanayapima na kuuza viwanja, waache kwa
kuwa haliruhusiwi kuanzia sasa.
“Kama ni shamba litabaki kuwa shamba kama
mtu alinunua shamba anataka kubadilisha liwe
kiwanja imekula kwake,” alisema Lukuvi na
kuongeza kama kuna mtu anataka kufanya hivyo
akabidhi shamba kwa halmashauri ili ligawiwe au
kuuzwa.chanzo habar leo.

Malkia wa pembe za ndovu leo amepandishwa kizimbani.soma zaid.

Malkia wa pembe za ndovu leo amepandishwa kizimbani.soma zaid.

Mwanamke wa Kichina ambaye anafahamika
kama ‘malkia wa pembe za ndovu’ katika eneo la
Afrika Mashariki Yang Feng Glan leo amepanda
kizimbani katika mahakama ya Tanzania
akikabiliwa na shtaka la kuendesha genge
linaloratibu biashara ya pembe za ndovu.

Walimu watatu wa sekondari wilayani muleba mkoani kagera waibiwa nyumbani kwao.soma zaid.

Walimu watatu wa sekondari wilayani muleba mkoani kagera waibiwa nyumbani kwao.soma zaid.

Katika hali ya kusikitisha kumetokea  wizi wilayani muleba mkoani kagera hii keo majira ya saa tatu asubuhi ambapo walimu wa sekondari ya mubuka tarafa ya kasharunga wameibiwa nyumbani kwao wakiwa kazini walimu hao watatu  majina yamehifadhiwa wameibiwa wakiwa shuleni wakiteleza majukumu yao ya kikazi ya kila siku akiongea muhanga wa wizi amesema wameibiwa computer tatu aina ya laptop na hela na simu  ambapo wezi hao wameruka ukuta wa fensi na kutoboa singibodi na kurukia ndani na kuingia kila chumba hili ni tukio la pili hawa walimu kuibiwa.juhudi za kuwatafuta wezi bado zinaendelea.

Mauaji tena hii leo mkoan mwanza mwenyekiti wa serikali ya mtaa amiminiwa risasi begani na kifuani.soma zaid.

Mauaji tena hii leo mkoan mwanza mwenyekiti wa serikali ya mtaa amiminiwa risasi begani na kifuani.soma zaid.

Mail
JIJI la Mwanza linakithiri kwa mauaji ambapo leo
watu wawili wamemfyatulia risasi kifuani na
begani, Aliphonce Musanyenzi, Mwenyekiti wa
Serikali Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa na
kumuua, anaandika Moses Mseti.

Tukio hilo linakuja ikiwi ni siku nne tangu
watu watatu waumini wa Dini ya Kiislamu
kuuawa msikitini jijini humo.
Katika kipindi cha mwezi mmoja sasa watu zaidi
ya 11 wamepoteza maisha kutokana na
kuendelea kuwepo kwa matukio ya kinyama
yanayofanywa na vikundi vya watu visiofahamika.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamikia leo saa 2:
00 usiku wakati Musanyenzi akiwa katika harakati
za kusuluhisha ugomvi wa familia ya Neema
Malangula na anayetajwa kuwa bwana wa
Neema ambaye hajafamika.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, wakati mwenyekiti
huyo akiwa na familia hiyo, ghafla walitokea watu
wawili watembea kwa mguu na kuwaambia
kwamba wapo chini ya ulinzi.
Baada ya kuwaamru, ndipo watu hao waliokuwa
wawili, mmoja wao alimfyatulia risasi za kifuani
na begani Musanyenzi na kufariki dunia.
Diru Luzerera, Shuhuda wa tukio hilo ambaye pia
ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo amesema
kuwa, alitoka na marehemu katika kikao cha
ulinzi na usalama wa mtaa huo saa 12 jioni.
Luzerera amesema kuwa,” marehemu
Musanyenzi baadaye tukiwa kwake alituambia
twende duka lililopo kwake akatununulie soda,
tulipomaliza kunywa soda na wakati
anatusindikiza ndipo tulikumbana na watu hao,”
amesema.
Getruda Henry, mke wa marehemu
Mumusanyenzi amesema kuwa, katika familia
yao hawakuwa na ugomvi na mtu yeyote.
“Nikiwa shambani naendelea na shughuli zangu,
ndipo nikasikia kelele watu wakikimbia hovyo na
mimi nikakimbia kuelekea nyumbani ile nafika tu,
nikakutana na watu wakiwa wamezunguka
nyumba huku mume wangu (Alphonce
Musanyenzi) akitokwa damu,” amesema Henry.chanzo mwanahalisonline.

Hii ni rasimi kocha wa manchester united afukuzwa kazi ya kuifundisha man u.soma zaid.

Hii ni rasimi kocha wa manchester united afukuzwa kazi ya kuifundisha man u.soma zaid.


Manchester United have sacked Louis van
Gaal just two days after the Dutchman led
them to victory over Crystal Palace in the
FA Cup final.
Van Gaal has been made to pay for
United's poor Premier League campaign
and will be replaced by former Chelsea
boss Jose Mourinho.
His Dutch coaching staff - including
United assistant coach Albert Stuivenberg
and goalkeeper coach Frans Hoek - have
also left the club with immediate effect
============
From Sky Sports
Manchester United will make a statement
regarding Louis Van Gaal's future at 1pm
UK Time

AJALI#Boti ya MV mapeza imezama katika ziwa nyasa watu 12 wahofiwa kupoteza maisha.soma zaid.

AJALI#Boti ya MV mapeza imezama katika ziwa nyasa watu 12 wahofiwa kupoteza maisha.soma zaid.

Kuna boti ya Tanzania imezama katika
ziwa Nyasa inasemekana kuna hofu ya
watu 12 wamefariki.
MV Mapeza ilikuwa ikitokea Mbamba Bay
ikielekea Nkhata Bay Nchini Malawi.
Tanzanian boat sinks on Lake Malawi, 12
passengers fears dead
[​IMG]
Tanzanian boat that was sailing from
Mbamba Bay in Tanzania to Nkhata Bay in
Malawi sunk on Lake Malawi in the dawn
hours of Saturday.
Confirming the sad news to Malawi News
Agency (MANA), outgoing Assistant
Surveyor of Vessels responsible for
Likoma Island and Nkhata Bay,
Chikumbutso Ziyaya said that a Tanzanian
MV Mapeza was sailing from Mbamba
Bay to Nkhata Bay but the passengers
last talked to people from Nkhata Bay at
around 3 o'clock in the morning.
"We last talked to MV Mapeza passengers
around 3 in the morning asking to be
rescued after their boat was full of water
due to strong mwera wind,"Ziyaya
explained.
Ziyaya then said that due to lack of funds
his office failed to send a rescue team
the passangers.
"Due to lack of funds we failed to rescue
the passengers. But a private boat owned
by Shad went around 7 in the morning to
rescue the passengers but it was too
late," Ziyaya said.
He then disclosed that of the missing
passengers, seven are Tanzanians while
nationality of the other five passengers is
yet to established.
"I suspect that the boat had a faulty water
pump that is why the vessel was unable
to flash out water from the boat," Ziyaya
said.
According to Ziyaya, the private boat that
went to rescue the passengers returned
to Nkhata Bay without tracing MV
Mapeza.
Most passenger boats that sail from
Likoma Island to Nkhata Bay are not sea
worthy.
Just last week another boat sailing from
Likoma Island to Nkhata Bay had to be
towed by another private boat.
Chanzo: manaonline

Haya ndio maamuzi ya CUF soma zaid.

Haya ndio maamuzi ya CUF soma zaid.


Chama cha Wananchi (CUF) kimesema
kitawashtaki Mahakama ya Kimataifa (ICC)
viongozi wa Serikali ambao walitumia mamlaka
yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka
jana, wakiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani na
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF)
kimesema kitawashtaki Mahakama ya Kimataifa
(ICC) viongozi wa Serikali ambao walitumia
mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu
wa mwaka jana, wakiwamo Waziri wa Mambo ya
Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest
Mangu.
CUF, chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar
kinachodai kuwa mgombea wake wa urais
alishinda kwenye uchaguzi huo uliofanyika
Oktoba 25, 2015, kimesema kwa sasa kinatumia
kampuni mbili za kisheria, moja ya ndani na
nyingine ya nje, kuwasaidia katika kushughulikia
suala hilo.
Mbali na vigogo hao wawili wa Serikali, chama
hicho kimesema hatua hiyo pia itawahusisha
viongozi na watumishi wa umma ambao
hawakuchukua hatua kwa dhuluma iliyofanywa
kwa Wazanzibari wakati na baada ya uchaguzi.
CUF imesema hatua hiyo itachukuliwa baada ya
jana kuzindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za
binadamu visiwani humo wakati wa uchaguzi
huo.
Mbali na kuwafikisha ICC, Mazrui alisema tayari
chama hicho kimeanza kuchukua hatua stahiki ili
kuwafikisha viongozi hao kwanza mbele ya
Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutochukua
hatua dhidi ya uovu uliokuwa unafanywa Zanzibar
wakati wa kipindi hicho.
Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio
la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake
kwenye mahakama hiyo inayopingwa na viongozi
wa Afrika wanaodai kuwa wana vyombo vyao vya
kushughulikia haki za binadamu. Tayari viongozi
wawili wa Kenya, Rais na makamu wake
wameshafikishwa kwenye mahakama hiyo, lakini
kesi dhidi yao ilikosa nguvu baada ya mashahidi
kukataa kwenda kutoa ushahidi.
Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim
alifuta matokeo ya urais, wawakilishi na
madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo
alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.
Alifuta wakati matokeo ya majimbo 31 kati ya 40
yameshatangazwa na kubakia majimbo tisa
ambayo matokeo yalishabandikwa vituoni.
CUF ilidai kuwa ilishinda na Jecha alipotangaza
uchaguzi wa marudio, chama hicho kilijitoa na
hivyo CCM kushinda viti vyote.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,
naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor
Ahmed Mazrui alisema chama chake
kinakamilisha ripoti ya ukiukwaji wa wa haki za
binadamu uliofanywa wakati wa mchakato huo
ambao chama hicho kina ushahidi wa kutosha.
Alisema ripoti hiyo ina matukio yote yaliyotokea
kuanzia uandikishaji, kampeni, kuahirishwa kwa
uchaguzi na hata kurudiwa.
“Hakuna mtu aliyechukuliwa hatua za kisheria ili
kutenda haki kwa waathirika,” alisema
akizungumzia vitendo vya wananchi kupigwa na
askari, kurushiwa risasi za moto, kubambikiwa
kesi, mashambulizi yaliyofanywa na mazombi na
uchomaji nyumba za wafuasi na ofisi za wafuasi
wa chama.
Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF
alifafanua kuwa licha ya viongozi hao wa wizara
na Jeshi la Polisi kuanza kushtakiwa kwenye
mahakama za ndani, ICC itawahusisha watu
wengi zaidi.
Alisema juhudi za makusudi zimechukuliwa na
chama hicho kuwatafuta washauri wa masuala
ya kisheria na uendeshaji wa ICC ili kukusanya
ushahidi wa kutosha utakaowatia hatiani
wahusika wote.
“Waziri, IGP na baadhi ya askari watahusika.
Tunayo majina yao na uchunguzi wetu
utakapokamilika tutawataja,” alisema Mketo.
Kuhusu waziri atakayehusika kwenye mashtaka
yatakayofunguliwa ICC endapo vigezo vitatosha
ni wale waliokuwa kwenye nafasi hiyo wakati
hayo yakitokea.
“Zipo kampuni mbili zinatushauri na kutusaidia
kukusanya ushahidi,” alisema bila kuzitaja, lakini
akafafanua kuwa moja ni ya nje na nyingine ya
ndani. Alisema hazitaji majina kwa kuwa Serikali
inaweza ikaingilia kati na kukwamisha mchakato
mzima.
Baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jana,
Mazrui alisema wamepanga kumuandikia barua
Rais John Magufuli na kumkabidhi nakala kwa
kuwa ni Amiri Jeshi Mkuu, ajue kinachoendelea
ndani ya utawala wake.
Alisema ripoti hiyo pia itapelekwa kwenye
jumuiya, taasisi na mashirika ya kimataifa
yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni.
Alisema CUF imebaini mipango ya Serikali ya
kutaka kuwakamata viongozi wake wa Zanzibar
na “kuwaweka kwenye magereza ya Bara ili
kuwanyamazisha Wazanzibar”.
Ili kuongeza uwazi kwa wanaharakati wa ndani,
alisema ripoti ya chama chake sambamba na
vielelezo vyote muhimu, itapelekwa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma
za Sheria Zanzibar (ZLSC) na taasisi nyingine
zinazojishughulisha na masuala ya haki za
binadamu nchini.
Ili kuongeza uwajibikaji, alisema jopo la mawakili
wa chama chake linashirikiana na wanasheria
wabobezi wa kimataifa ili kukamilisha taratibu
zitakazowezesha kuchukuliwa hatua kwa watu
wote ambao walichochea au walitoa maagizo
yaliyosababisha makosa dhidi ya binadamu.
“Tumeshamuandikia barua IGP na waziri. Hiyo ni
moja ya hatua muhimu kabla hujawashtaki,”
alisema.
Waziri hakupatikana kuthibitisha kupokea barua
hiyo. IGP alisema hajaipata ripoti hiyo, hivyo
hawezi kusema chochote juu ya madai
yaliyosemwa na CUF. “Nikiipata nitaijibu,”
alisema kwa kifupi.
Naibu katibu mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali
Vuai alisema hujuma ni sehemu ya siasa za kila
siku visiwani humo.
Alibainisha kuwa chama chake ambacho
kimekuwa kikitangazwa mshindi tangu siasa za
ushindani ziliporejeshwa mwaka 1992, kimekuwa
kikihujumiwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi na kutoa rai kwa CUF kuchukua
hatua kama ina uthibitisho.
“Makosa yote ya jinai yanashughulikiwa na
vyombo vya dola. Kinachohitajika ni ushahidi wa
kutosha,” alisema Vuai.
Pia alitahadharisha dhidi ya siasa za chuki
ambazo alisema zinaenezwa visiwani humo licha
ya kuwa pazia la Uchaguzi Mkuu limeshafungwa.
“Wapo viongozi wanaenda misikitini kuhubiri
uongo… hii si sawa,” alisema.
Kuhusu hatua za zinazotarajiwa kuchukuliwa na
CUF alisema viongozi wa chama hicho wanajua
kuwa wamekosea, hivyo wanajaribu kutafuta
namna ya kuwatuliza wanachama wao hasa wale
waliopoteza nafasi zao za uwakilishi kwenye
Baraza la Wawakilishi.
“Viongozi wanahangaika. Jinamizi la kususia
uchaguzi bado linawaandama. Hawaeleweki na
ndiyo maana wanajaribu kote kote. Mahakamani
na misikitini. Huko ni kutapatapa,” alisisitiza Vuai.chanzo mwananch.

Back To Top