Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Friday, September 30, 2016
Kauli ya Freemani Mbowe kuhusu hali ya kisiasa nchini tokea kusitishwa kwa Operasheni Ukuta.soma zai

Kauli ya Freemani Mbowe kuhusu hali ya kisiasa nchini tokea kusitishwa kwa Operasheni Ukuta.soma zai


• Hadi jana na hadi sasa viongozi wa Dini
hawajaleta Taarifa yoyote kuhusu kama waliweza
kukutana na Rais
• Sisi kama Chama Cha Siasa tumetekeleza
wajibu wetu
• Tunawaheshimu viongozi wa Dini na
Tutaendelea kuwaheshimu
• Sasa kama chama cha Siasa tutaendelea sasa
kutekeleza wajibu wetu
• Kazi ya siasa sio kazi ya siku moja
• UKUTA ni Fikra. Yaani fikra za kupambana na
ukandamizaji wa haki na demokrasia, Kwa
muktadha huu tuna wajibu wa kufanya siasa
ndani ya wigo uliowekwa nchini na pia kimataifa
• Tanzania sio kisiwa. Ndio maana chama kiliona
Umuhimu wa kutuma ujumbe Mzito kwenye ziara
maalumu nchi za Ulaya .Nchi za Ujerumani na
Denmark kuendelea kuujulisha Ulimwengu juu ya
ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu na
Demokrasia kinyume na jinsi ambavyo serikali
imekua ikijipamba kuwa ya amani na Utulivu
Hiyo ilikua ziara ya awamu ya kwanza
Bado Ujumbe Mwingine utatumwa kwenye nchi
nyingine kama Uingereza,Marekani,Canada ,
Malaysia,Japan na hata ndani ya Umoja wa
Afrika na kwenye mtangamano wa kikanda kama
SADC na EAC
• Tunataka utawala ujue mipaka yetu haiishii
Namanga na Tunduma
Tutatumia Taasisi za kimataifa
• Kurugenzi yetu ya Sheria inaendelea na kazi
nzuri ya kutumia Mahakama za ndani na za
kimataifa kupeleka mashauri yetu
• Viongozi wetu mbalimbali wanakabiliwa na kesi
mbalimbali zinazoitwa kesi za Uchochezi
• Tumesikia Juzi polisi katika kujihalalishia uovu
wao walipojua CCM sasa wanakaribia kuanza
vikao vya ndani wanatangaza kuruhusu Mikutano
ya ndani
• Sisi tunaandaa mikutano ya kisiasa nchi nzima
• Ukuta wa Oktoba Mosi utasogezwa mbele kwa
Tarehe Maalumu
• Rais anatumia jeshi kupambana na Sisi lakini
hakuweza kuwatumia kwenye Tetemeko Kagera
na kuwaacha raia wetu wakiteseka
• Leo anatumia jeshi kuumiza Raia na vituko
vingine eti kufagia na wengine kupanda Miti
• Rais aliyekwepa mikutano ya kimataifa kwa
kisingizio cha Tetemeko la Ardhi Kagera
hakufika,Hakupeleka jeshi ila alikaa İkulu
akisubiri Ripoti
MİGOGORO İNAYOPANDİKİZWA
________________________________
• Prof.Lipumba amekituhumu CHADEMA kuhusika
na migogoro ndani ya CUF
• Sikusudii kumjadili Lipumba.Maana sitaki kumpa
nafasi na umuhimu aliokuwa nao zamani
He's politically İrrelevant.
• CHADEMA kitashirikiana na chama chochote
chenye dhamira ya dhati
• CUF tunaheshimu maamuzi yao ya vikao halali
• Natoa Rai kwa Wanachama wa CHADEMA nchi
Nzima kupuuza kauli za Prof.Lipumba na tuache
kumpa ushirikiano wowote kwa kuwa ni msaliti
wa mageuzi anayetafuta kuangamiza Upinzani
MSAJİLİ WA VYAMA VYA SİASA
_________________________________
• Jaji Mutungi amechochea mgogoro CUF na
hatuna sababu za kumuheshimu
• Atambue kuwa tutasimama na CUF na ajue
yeye sio Msajili wa kwanza.
• Mbinu zake na Watawala zitashindwa
• Serikali inatumia nguvu kubwa sana na taasisi
nyingine kununuliwa
• Kwa mfano TWAWEZA .Upo ushahidi kuwa
walipewa pesa na serikali kupika Utafiti siku moja
kabla ya UKUTA kwa bahati mbaya hawakupika
kwa kiwango cha kuifanya ripoti ionekane kuwa
na sifa za kiutafiti
Aluta Continua.!
Freeman Aikaeli Mbowe.
Mwenyekiti, CHADEMA Taifa.

Uchumi wa Tanzania wakua kwa asilimia 7.9

Uchumi wa Tanzania wakua kwa asilimia 7.9


Uchumi wa Tanzania wapaa, kasi yake yafikia
7.9%, serikali yajiendesha kwa fedha za ndani,
ikiwa ni pamoja kulipia matumizi yake yote, huku
mapato ya yakiongezeka kwa asilimia 34.

Thursday, September 29, 2016
Donard Trump amepoteza utajili $800m ya utajiri wake ndani ya mwaka mmoja.soma zaid

Donard Trump amepoteza utajili $800m ya utajiri wake ndani ya mwaka mmoja.soma zaid


Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania
urais kupitia chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya
utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja,
kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw
Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani
ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi'
kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la
New York.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika
kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas:
Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa
kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais
wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu
mwenye busara katika biashara na majadiliano.
Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu,
alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati
umefika kwa taifa hili kuwa na mtu
anayefahamu mengi kuhusu pesa."
Mapema mwaka huu, hoteli mpya ya Trump
ilifunguliwa Washington DC, karibu na White
House
Alipoteza vipi $800m?
Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa
Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu,
wanasema hilo limetokana na kudorora kwa
soko la nyumba, afisi na ardhi New York.
Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na
Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba
maarufu la Trump Tower linalopatikana
Manhattan.
Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake
cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida,
pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba
la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda
thamani.
Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni?
Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa
zake binafsi, kwenye kampeni kufikia sasa.
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake
dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $
100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye
mashirika makubwa kama vile NBC Universal,
Univision na Macy's.
Ivana na Donald Trump mwaka 1989
Utajiri wake kamili?
Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha
taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya
Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni
kumi."
Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn,
Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao
Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw
Trump pia huhesabu thamani ya jina lake,
ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni
karibu $3.3bn.

Saed kubenea na wenzake kupanda mahakamani Octoba 12.soma zaid

Saed kubenea na wenzake kupanda mahakamani Octoba 12.soma zaid

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kumjeruhi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresa Mmbando inayowakabili Saed Kubenea,
Halima Mdee, Mwita Waitara na wengine
watatu, umekamilika.
Wakili wa Serikali, Flora Massawe mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameiomba
Mahakama ipange tarehe kwa ajili ya
washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Baada ya ombi hilo, Hakimu Shaidi aliahirisha
kesi hiyo hadi Oktoba 12, washtakiwa
watakaposomewa maelezo hayo kuhusu shtaka
linalowakabili.
Kubenea ambaye ni Mbunge wa Ubungo
aliunganishwa kwenye kesi hiyo na kuwa
mshtakiwa wa sita. Mdee na Waitara pia ni
wabunge wa Kawe na Ukonga.
Washtakiwa wengine ni Manase Njema,
ambaye pia ni diwani wa Kimanga,
mfanyabiashara Rafii Juma na Ephraim
Kinyafu, ambaye ni diwani wa Saranga Kimara.
Wanadaiwa Februari 27, katika Ukumbi wa
Karimjee, wilayani Ilala Dar es Salaam
walimjeruhi Theresia na kumsababishia
majeraha. Washtakiwa wapo nje kwa dhamana

Wednesday, September 28, 2016
Wizara ya Elimu imepokea msaada wa sh.6 billion kutoka kutoka kwa shirika la misaada na maendeleo la Uingeleza(DFID)soma zaid

Wizara ya Elimu imepokea msaada wa sh.6 billion kutoka kutoka kwa shirika la misaada na maendeleo la Uingeleza(DFID)soma zaid

Dar es Salaam. Wizara ya Elimu na mafunzo ya
Ufundi Stadi, imepokea kiasi cha Shilingi
6.3bilioni kutoka kwa Shirika la Misaada na
maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya
kufanyia ukarabati wa shule zilizoharibiwa na
tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema
leo Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi
Profesa Joyce Ndalichako amesema msaada huo
utasaidia kujenga shule za Ihungo na Nyakato
ambazo zimeharibika kwa kiasi kikubwa.
"Shule hizo zitajengwa vizuri na kwa uimara zaidi
ili kuzuia matatizo ya aina hiyo pindi yatapo
tokea tena" amesema.
Amesema fedha hizo zimetolewa na shirika hilo
mara moja hivyo ujenzi na ukarabati utaanza
mara moja ili kuondoa adha wanayoipata
wanafunzi.
"Utaratibu umeshafanyika na wakandarasi
wanaendelea na taratibu ili kuanza ujenzi huo"
amesema

Wazir mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema nchi kwa sasa imepoteza mwelekeo.soma zaid.

Wazir mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema nchi kwa sasa imepoteza mwelekeo.soma zaid.


Dar es Salaam . Waziri Mkuu mstaafu, Jaji
Joseph Warioba amesema kwa sasa nchi
imepoteza mwelekeo katika masuala ya itikadi,
Sera na maendeleo, badala yake imebaki
kuongozwa kisiasa na matukio.
Akizungumza katika mhadhara wa tatu wa
Mwalimu Nyerere leo Dar es salaam, Warioba
aliyekuwa Mgeni rasmi amesema tofauti na
zamani kulipokuwa na ubaguzi wa makabila,
siku hizi watu wanabaguana kwa vyama.
"Sijui kama tuna itikadi na Sera siku hizi,
tunategemea matukio na watu" alisema na
kuongeza: "Siku hizi wananchi hawajui
tunaelekea wapi, zamani kulikuwa na Sera na
itikadi, lakini hata ukiangalia vyombo vya habari
ni siasa tu." Amesema na kuongeza:
"Zamani kina Kahama (Sir George) walikuwa
wanahamasisha maendeleo, siku hizi viongozi
wetu wanakwenda kushitakiana kwa wananchi."
Mhadhara huo umehudhuriwa na Makamu wa
Rais mstaafu, Dk. Gharib Bilal, Waziri wa
zamani, Sir George Kahama na wasomi
mbalimbali.

Mahakama kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe.soma zaid

Mahakama kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe.soma zaid

Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC). Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali. Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo. Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria. Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandikia Msajili wa Mahakama barua kujua kama anatambulika, lakini alijibu kuwa haimtambui. Kutokana na majibu ya msajilihuyo kupitia barua yake ambayo wameiwasilisha mahakamani kama kielelezo, Kibatala alidai sheria na mchakato mzima uliotumika vilikuwa ni batili. Mawakili wa NHC, Ipilinga Panya na Aloyce Sekule walidai shirika hilo kabla ya kumtimua Mbowe lilimwandikia notisi ya siku 30 iliyokwisha kisha akaongezewa siku 30 zingine kama sheria inavyotaka ambazo ziliisha na kumpa tena siku 14, lakini hakulipa deni. Wakili wa kampuni ya Foster Auctioneers and General Traders, Aliko Mwamanenge alidai madai ya kuwa mteja wake ni dalali wa Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na siyo kampuni, hayana ukweli kwani upande wa mlalamikaji ulipoandika barua kuulizia uhalali wake ulipaswa kuuliza jina la mmiliki kampuni hiyo. Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji Kibatala alidai notisi zinazodaiwa kuandikwa na NHC zilipelekwa mahali pasipohusika kwa kampuni ya Free Media badala ya Mbowe Hotels ambayo ina mkataba na NHC. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sivangilwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Oktoba 18, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa maombi hayo ya mlalamikaji. Septemba Mosi, wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders walifika kwenye ofisi za kampuni ya Free Media na kuondoka vifaa mbalimbali vya kazi, zikiwamo kompyuta na viti kwa madai kwamba mmiliki wake, Mbowe anadaiwa na NHC fedha nyingi za kodi ya pango.chanzo mwanach

Waziri Profesa makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu kuchangamkia Fursa.soma zaid

Waziri Profesa makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu kuchangamkia Fursa.soma zaid


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa
sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara
kushirikiana na Serikali katika kuchangamkia
fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
sekta hiyo hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba wa
wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema
kwa sasa Serikali kupitia Rais wa Awamu ya
Tano inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi
nchini Uganda, ujenzi wa barabara ya kulipia wa
Dar es Salaam-Chalinze KM 144 (Dar-Chalinze
Express way) na ujenzi wa reli ya kati hivyo ni
muhimu kwa wadau hao kutumia mkutano huo
katika kuijadili miradi hiyo.
“Ni matumaini yangu katika mkutano huu
mtajadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na
Serikali katika kutekeleza fursa za ujenzi wa
miundombinu hapa nchini ikiwemo kuungana na
Serikali (Public Private Partnership) au kwa njia
nyingine yoyote”, amesema Waziri Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Aidha, Profesa Mbarawa amewataka wadau hao
kutumia mkutano huo wa siku mbili kujadili
namna bora ya kutunza na kuboresha
miundombinu ya reli na barabara ili kuweza
kudumu kwa muda mrefu.
Amesisitiza wadau hao kuja kwa wingi nchini na
kuwekeza katika sekta hiyo ili kupanua
ushindani wa kibiashara katika soko la kitaifa na
kimataifa.
Wazri Mbarawa amebainisha kuwa Serikali
inaendelea kutafuta pesa kutoka kwa wadau
mbalimbali na kushirikisha taasisi binafsi
kupitia mpango wa kushirikiana baina ya Serikali
na Taasisi hizo (Public Private Partnership ) ili
kutekeleza miradi ya miundombinu ya reli na
barabara nchini.
Mwenyekiti wa wadau wa barabara Tanzania Eng.
Abdul Awadhi akiongea na wadau wa miundombinu
ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa
wadau hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) Eng. Bruno Ching’andu amesema
kuwa licha ya TAZARA kuwa na treni za umma
zinazotoa huduma za usafiri nchini bado
inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo
uhaba wa fedha katika uendeshaji wa shirika
hilo ikiwemo gharama za ujenzi na ukararabati
wa mabehewa.
Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha
wadau wa miundombinu ya barabara na Reli
kutoka Taasisi za Serikali na wadau mbalimbali
wa sekta hiyo kutoka ndani na nje ya nchi lengo
likiwa ni kujadili kwa pamoja namna ya
kuboresha miundombinu hiyo.

Mvutano mkali watokea kwenye mdaholo kati ya Bi clinton na Trump.soma zaid.

Mvutano mkali watokea kwenye mdaholo kati ya Bi clinton na Trump.soma zaid.

Mdahalo wa wagombea urais wa Marekani Hillary Clinton wa Democratic na Donald Trump wa Republican ulikuwa kama pambano kati ya wakili na muuza bidhaa, wengi wanasema ni kama wakili aliibuka kidedea Nani bora kati ya wakili na muuza bidhaa Ni vigumu kukumbuka lakini kabla Bi Clinton ahudumu wadhifa wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, seneta au mama wa taifa , alikuwa ni wakili na wakili mwenye kipaji. Na kwa miaka hii yote bado anaendesha kampeni yake kama wakili, akiwa anachukua tahadhari na aliye mtulivu, tabia ambayo wakili anahitaji kuwa nayo mahakamani. Bwana Trump kwa upande mwingine ni muuza bidhaa. Udhaifu uliopo hapa ni kwamba muuza bidhaa huzungumza sana jambo ambalo linaweza kuwa tatizo kwa mda wote wa dakika 90 za mdahalo. Trump alidai kuwa licha ya kampeni za Clinton, amefanya vyema katika kura ya maoni Bi Clinton alionekana kung'aa aliposema kuwa Trump amekataa kuweka wazi kodi zake, akisema kuwa kuna jambo mihimu ambalo Trump hataki nchi ilijue au labda huenda likawa ni jambo baya ambalo anajaribu kulificha. Kabla ya Trump kuvutwa kwenda kwa suala la kodi, alitumia muda mrefu akijaribu kujieleza na mdahalo ulionekana kumwendea salama. Hata hivyo Bi Clinton alionekana kung'aa katika sehemu ya kwanza ya mdahalo, alipomhangaisha Trump kuhusu suala la kodi huku vilevile nayo sehemu ya pili ikionekana kuwa changamoto kubwa kwa Republican. Uhusiano kati ya watu wa rangi tofauti Suala lilikuwa ni uhusiano kati ya jami za rangi tofauti nchini Marekani, na ndio wakati huu Trump alihitajika kueleza ni kwa sababu gani alikuwa na shaka juu ya uraia wa Rais Obama. Mamilioni ya watu walitazama mdahalo huo kote duniani Trump kwa mara nyingine alijaribu kumlamu Bi Clinton kwa kuanzisha uvumi huo mwaka 2008 akisema kuwa anastahili shukran kutoka kwa Obama na wapiga kura weusi wa kwa kuchangia ufumbuzi wa suala hilo. Bi Clinton alitumia fursa hilo kumshambuli Trump akisema kuwa alionyesha ubaguzi ulio wazi aliposema kuwa rais mweusi wa marekani hakuwa raia wa nchi hiyo. Nani aliye na tajriba na kuongoza? Mdahalo ulipoelekea dakika zake za mwisho mwisho suala la ni nani aliye na uwezo wa kuongoza liliibuka. Clinton alijitetea akisema kuwa safari zake nchi za nje na jitihada za kutatua masuala kwa njia ya kidiplomasia vilionyesha kuwa ana uwezo wa kuwa rais. Image Majibizano makali yaliibuka kuhusu ni nani aliye na uwezo wa kuongoza nchi Alimlaumu Trump kwa kuwaita wanawake nguruwe na mbwa na kwa kudai kuwa wanawake hawastahili mishahara sawa ikiwa hawajafanya kazi sawa na wanaume. Hata hivyo Trump alijibu akisema kuwa matangazo ya Bi Clinton yanampiga vita, lakini badala yake anazidi kufanya vizuri katika kura ya maoni, jambo ambalo halikuridhisha.

Samweli sitta apelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu.soma zaid

Samweli sitta apelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu.soma zaid

Rais Dk. John Magufuli (kulia), alipokwenda
kumjulia hali Samuel Sitta hivi karibuni.
HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si
nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini
Ujerumani kwa matibabu zaidi.
Habari za uhakika ambazo MTANANIA imezipita
jijini Dar es Salaam jana, zinasema Sitta
alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada
ya afya yake kubadilika ghafla.
“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa
nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa
imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone
haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.
“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa
kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua
bado anampigania uhai wake…hii tabia ya
mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui
inafaidika nini.
“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu
natambua amekuwa asikumbuliwa mno na
tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake
siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.
Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John
Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini
alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha
kumwombea dua Mungu amsaidie.
Siku iliyofuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.
Sitta ameshika nyadhifa mbalimbali, zikiwamo
za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi
2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

Chama cha walimu (CWT)mkoani simiyu kimempinga Ndalichako.soma zaid

Chama cha walimu (CWT)mkoani simiyu kimempinga Ndalichako.soma zaid

Maswa. Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
wilayani hapa, Mkoa wa Simiyu, kimemjia juu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Joyce Ndalichako kuwa anaupotosha umma juu
ya madai yao.
Kimesema walimu wanadai madeni mengi, hivyo
kauli ya Ndalichako kwamba hawana
wanachodai inalenga kuleta uchonganishi kati
yao na Serikali.
Mwenyekiti wa CWT wilayani hapa, Onesmo
Makota amesema wao wanaidai Serikali zaidi ya
Sh500 milioni kutokana na malimbikizo na
mapunjo ya mishahara.

Serikali imetoa msaada ya sh.545 milion kutoka nchini India kwa ajilia Tetemeko iliyotokea Kagera.soma zaid

Serikali imetoa msaada ya sh.545 milion kutoka nchini India kwa ajilia Tetemeko iliyotokea Kagera.soma zaid

Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Balozi wa India hapa nchini
Sandeep Arya mara baada ya kupokea
mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi
za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar
es Salaam. Msaada huo umetolewa na
Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia
waathirika wa Tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera.

Monday, September 26, 2016
Watendaji 3 wa kijiji wasimamishwa kazi wilayani Singida.soma zaid

Watendaji 3 wa kijiji wasimamishwa kazi wilayani Singida.soma zaid

WATENDAJI watatu wa vijiji katika wilayani ya
Manyoni mkoa wa Singida, wamesimamishwa
kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi
iliyopo kwenye vijiji vyao na kusababisha
upotevu wa fedha za serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa
wilaya hiyo, Geofrey Mwambe, alisema amefikia
hatua hiyo baada ya kutembelea vijiji hivyo
mwezi huu na kukutana na upotevu wa fedha
kwenye miradi mbalimbali ikiwamo ya maji huku
wengine wakiwa hawajui wajibu wao katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Aliwataja kuwa ni mtendaji wa kijiji cha Chikuyu,
Msemembo na Rungwa na kwamba pia
ameivunja kamati ya maji ya kijiji cha Chikuyu.
Alisema baadhi ya miradi hiyo ni wa maji wa
kijiji cha Chikuyu ambao mitambo yake inatumia
sola, lakini kwenye akaunti una Shilindimilioni
moja wakati mradi wa maji Soliya
unaoendeshwa mitambo ya aina hiyo, lakini una
zaidi ya Sh. milioni 40 kwenye akaunti.
Alisema watendaji hao hawawajibiki ipasavyo
kuisimamia miradi ya aina hiyo na kusababisha
serikali kupoteza mamilioni huku wengine
wakiendeleza vitendo vya rushwa.
Alisema viongozi watendaji katika wilaya hiyo
wasioendana na kauli ya Rais John Magufuli ya
“hapa kazi tu” ni bora wajitoe wenyewe ili
kupisha viongozi wawajibikaji wanaoweza
kuwajali wananchi kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia kuhusu maeneo ya wazi
yaliyovamiwa, Mwambe alisema mpango alionao
ni kuhakikisha maeneo yote ya umma
yanajengewa uzio na kuwekewa alama kwa
ulinzi zaidi.
“Maeneo ya umma yalivamiwa kutokana na
kutokuwapo kwa bikoni zinazoonyesha kuwa ni
mali za umma,” alisema.
Alisisitiza kama kuna kiongozi aliuza maeneo
hayo ya umma kwa watu binafsi, atachukuliwa
hatua za kisheria na kuirudisha mali ya umma.

Majambazi yapora na kuua mtu mmoja mwanza.soma zaid

Majambazi yapora na kuua mtu mmoja mwanza.soma zaid

MTU mmoja amefariki dunia kwa kupigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
baada ya kuvamia na kupora kiasi cha fedha
ambacho hakijafahamika na simu nne za aina
mbalimbali katika duka la kuuza vifaa vya ujenzi
mtaa wa Nyakato Mecco Wilaya ya Ilemela
mkoani Mwanza.
Tukio hilo lilitokea jana saa 1:45 usiku ambapo
wavamizi hao ambao idadi yao haijajulikana
wakiwa na silaha aina ya SMG walivamia duka la
vifaa vya ujenzi mali ya Elikana Ngagaya na
kujaribu kupora maduka mengine ikiwa ni pamoja
na M-Pesa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed
Msangi, alimtaja aliyeuawa kuwa ni Grace Maega
(36) Mkazi wa Kangae ambaye alifariki muda
mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
“Inadaiwa wakati majambazi hao wanaondoka
eneo la tukio walifyatua risasi tatu zilizompata
kwenye bega la mkono wa kushoto wakati
akizima taa ndani ya duka lake lililopo jirani na
duka tajwa hapo juu kisha wakatokomea gizani.
“Majeruhi alikimbizwaHospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa matibabu lakini alifariki dunia
masaa machache baadae kwa kuvuja damu
nyingi,” alisema.
Katika tukio hilo la unyang’anyi wa kutumia
silaha hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa
kuhusiana na mauaji hayo huku Jeshi la Polisi
likiendelea na msako pamoja na uchunguzi
kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini
hapo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. “Tutafanya kila
tuwezalo kutumia ujuzi tulionao tukishirikiana na
wananchi kuhakikisha tunawakamata majambazi
hao.

Sunday, September 25, 2016
Unene  uwasababisha shirika la Ndege Emirates kutozwa faini.soma zaid

Unene uwasababisha shirika la Ndege Emirates kutozwa faini.soma zaid

Anaitwa Destro mwanasheria kitaaluma
anayehitaji kulipwa zaidi ya €2,000 kama
Gharama za usumbufu alioupata
(Damages) katika safari hiyo ya masaa
tisa
Kesi hiyo itakayosikilzwa Oktoba 20 huko
Padua inaibua maswali mazito kuhusu
huduma za usafiri duniani.
1.Je Kuna ulazima wa kuongeza kifungu
nyuma ya Tiketi kuwa utakabiliana na risk
ya kukaa na mtu aliye na Umbile kubwa
hivyo usidai kubadili siti au kurudishiwa
pesa
2.Je huu sio Ubaguzi? Kwamba Tutaanza
kuwabagua watu wanene katika vyombo
vya usafiri?
3.Mtandao wa Emirates una kauli mbiu
isemayo '' Sit back in comfortable seats
and enjoy the attention to detail that
makes our flights unique '' Je Kwa case
ya huyu jamaa watakuwa weemenda
kinyume? Kwa hapa Tanzania sheria
Inasemaje?
4.Kwenye Ticket taarifa za size ya mtu
zichukuliwe hata size ya Chura Kwa
wadada na kitambi ili kuondoa kadhia hii?
Nataka siku moja nipeleke kampuni moja
la mabasi kortini kama hii ikinitokea.
Unaweza panda na mama anakupa mtoto
umshike wakati yeye amelala...

Jarida la Forbose lasifu uwezo wa Ndege aina ya Bombardier.soma zaid

Jarida la Forbose lasifu uwezo wa Ndege aina ya Bombardier.soma zaid


WAKATI Serikali ya Tanzania ikiwa
imenunua ndege mbili za aina ya
Bombardier Dash8 Q400 kutoka Canada,
imebainika na kusisitizwa kuwa ndege
hizo zina usalama mkubwa, zinatumia
mafuta kidogo na kutabiriwa kuwa nguzo
muhimu kwa usafiri wa bei chee wa ndani
ya nchi mbalimbali.
Hayo yamo katika makala iliyoandikwa na
kuchapishwa na jarida mashuhuri duniani
la Forbes ikiwa na anuani “Can
Bombardier’s Q400 Save Regional  Air
Service in the US?” ambapo mwandishi
anafafanua faida za ndege hizo
ikilinganishwa na nyingine zinazofanya
usafiri wa ndani Marekani.
“Bombadia ina kasi nzuri na ya
kutosheleza mahitaji ya safari za ndani
kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi
kibiashara ikilinganishwa na ndege
nyingine za aina yake kama ATR,”
linaandika Forbes.
Faida nyingine inayotajwa ya Bombardier
ni matumizi ya mafuta. Forbes
wanaandika kuwa ndege hizo zina uwezo
wa kutumia mafuta kidogo sana kiasi
kwamba hata bei ya tiketi zake itakuwa
chini na kuwasaidia abiria wengi wa
ndani.
“Kutumia kwake mafuta kiasi kunaifanya
Bombardier kuwa na ufanisi wa asilimia
kati ya 48 mpaka 50 za kuwa bora zaidi ya
ndege nyingine za ukanda huu,”
linaandika Forbes.
Forbes wanasisitiza kuwa kutokana na
gharama za matengenezo kupanda, na
gharama nyingine za uendeshaji ikiwemo
mishahara mizuri kwa marubani, kuna
uwezekano mkubwa kwa Bombardier
kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza
tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege
nyingine.
“Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina
ya Bombardia ndio zitakuwa mbadala na
zitashika njia nyingi za ndani (Marekani)
kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na
zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa
(kutokana na gharama kubwa kwa ndege
nyingine) katika viwanja takribani 20,”
linaandika zaidi Forbes.
Akikaririwa katika makala hiyo,  Mike
Arcamone, Rais wa Masuala ya Biashara
wa Bombardier anasema wasiwasi wa
awali wa abiria kuhusu ndege hizo
kutumia mfumo wa turbo sasa umeondoka
kwa kuwa injini na dizaini ya kisasa ya
ndege hizo inaifanya isiwe na kelele kama
ilivyodhaniwa.
“Wanunuzi wengi wa ndege hizi
wamebaini kuwa hazina kelele na
watumiaji wengi wanaamini kuwa
zinaweza kuwa mbadala wa ndege
nyingine za bei nafuu,” anasema afisa
huyo kauli inayokubaliwa na wachambuzi
wa Forbes.
Tayari Serikali ya Tanzania imeahidi
kuleta ndege nyingine ya pili wiki hii
baada ya ile ya kwanza kuwasili nchini
wiki iliyopita ukiwa ni mkakati na
utekelezaji wa ahadi ya Rais John Pombe
Magufuli ya kulifufua Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL).
Kuwasili kwa ndege hizo kunaashiria
mengi lakini muhimu ni uthabiti wa ahadi
za Dkt. Magufuli akiwa ndani ya kipindi
cha mwaka mmoja wa uongozi wake,
ambapo mambo mengi makubwa ambayo
ameyaahidi ameanza kuyafanyiakazi na
kuwakuna wengi nchini na nje ya nchi.

Saturday, September 17, 2016
Wanazuoni wavutana kuhusu utafiti wa Twaweza.soma zaid

Wanazuoni wavutana kuhusu utafiti wa Twaweza.soma zaid

Dar es Salaam. Wanazuoni na wataalamu
mbalimbali wa uchumi nchini wamekuwa na
maoni tofauti kuhusu utafiti mpya wa Twaweza,
huku wakipishana kauli kuhusu hali ya
demokrasia inayoendelea nchini kwa sasa.
Baadhi wamekubalina na utafiti huo, lakini
wengine wanauona umekosa uhalisia katika
matokeo ya majibu ya waliohojiwa kuhusu hali ya
demokrasia nchini.
Profesa Benson Bana wa idara ya Sayansi ya
Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
alisema anakubaliana na matokeo ya utafiti huo
na kushangaa wanaohoji.
“Utafiti hukanushwa kwa utafiti, kwa kuhoji
mbinu zilizotumika kama maswali yaliyoulizwa
yalilenga majibu, au iwapo mwananchi alipewa
nafasi ya kufikiri, kutafakari kabla ya kutoa
majibu,” alisema mbobezi huyo.

Mlipuko wa bomu umejeluhi watu 29  jijini New York nchini Marekani.

Mlipuko wa bomu umejeluhi watu 29 jijini New York nchini Marekani.

Mlipuko umetokea jijini New York nchini
Marekani na kuacha watu 29
wamejeruhiwa na hamna taarifa za vifo.
Jeshi la Polisi limethibitisha mlipuko huo
ulikuwa ni wa makusudi na ulipangwa na
watu.
Vyombo vya Ulinzi vinaendelea na
uchunguzi ili kuwatia nguvuni wahusik

Auwawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasikara kisa ni mubakaji mkoani pwani.soma zaid

Auwawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasikara kisa ni mubakaji mkoani pwani.soma zaid

Kibaha. Mkazi wa Kibaha, Michael William
maarufu ‘Michael Dada’ ameuawa kwa kupigwa
na wananchi katika msitu wa Shirika la Elimu
Kibaha kutokana na tuhuma za kuteka watoto
wawili wa kike kwa lengo la kuwabaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniveture
Mushongi alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo
aliuawa Alhamisi saa 10:00 jioni.
Alisema Michael Dada anadaiwa kuwateka
watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la
nne wa Shule ya Msingi Kibaha na mwingine wa
Shule ya Awali ya Mama Kawili mchana wakati
wanacheza jirani na nyumbani kwao.

Neena yatangazwa kwa timu ya serengeti Boys.soma zaid

Neena yatangazwa kwa timu ya serengeti Boys.soma zaid

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na
waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kuhusu
mchezo kati ya Serengeti Boys na Congo-
Brazaville utakaofanyika Septemba 18 katika
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa
shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na
timu ya Serengeti Boys katika mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya
Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17
utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa
dhidi ya Congo-Brazzaville.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar
es Salaam Mhe.Nape amesema milango ipo
wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea
katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri
katika mechi hii ambayo ni muhimu sana
kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.
“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki,
tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri
na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa
timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.
Aidha aliongeza kuwa kesho asubuhi atakutana
na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno
ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na
kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi
uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa
kuwashangilia na kuwatia moyo.
Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi
kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki
zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa
kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ili
zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya
Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo
Fleva.
Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa
Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17
ambapo katika mchezo wa kesho watahitaji
ushindi na baadaye kufanya mechi ya
marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini
Congo-Brazzaville.

Wednesday, September 7, 2016
no image

Arusha. Sakata la posho za madiwani katika Jiji la Arusha limekuwa shubiri kwa madiwani baada ya kiwango walichokuwa wakipokea cha Sh60,000 kwa nauli za kuhudhuria vikao vya kisheria kupunguzwa hadi Sh10,000 na kuzusha mabishano. Pia wametakiwa kurejesha fedha walizolipwa kwa mawasiliano ya simu Sh150,000 kwa mwezi tangu Novemba mwaka 2015 hadi Agosti mwaka huu, ambazo ni sawa na Sh40.8 milioni lasivyo, Sh50,000 zitakatwa kila mwezi kutoka kwenye posho zao. Katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Arusha, hoja kuhusu posho ilitawala baada ya Meya wa jiji hilo, Kalist Lazaro kutoa ufafanuzi kuwa zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 2008 wakati wajumbe wengi wakiwa wa CCM, hivyo kushangazwa na ukubwa wake kwa sasa wakati baraza hilo likiongozwa na Chadema. Kikao hicho kilichoanza saa 4:30 asubuhi hadi saa 3:43 usiku kilivunja rekodi ya vikao kufanyika kwa muda mrefu zaidi kutokana na majibizano. Baadaye baraza hilo lilikaa kama kamati kutoa azimio dhidi ya mkurugenzi wa jiji baada ya kumtuhumu kukiuka kanuni naye akisisitiza anazifuta kikamilifu. Lazaro amesema hakutakuwa na mabadiliko ya nyongeza au punguzo kwa

Home » MAPENZI » Vitu 13 Akikuonyesha Mwanamke Ujue Amekuzimia Kwa Dhati Arusha. Sakata la posho za madiwani katika Jiji
la Arusha limekuwa shubiri kwa madiwani baada
ya kiwango walichokuwa wakipokea cha
Sh60,000 kwa nauli za kuhudhuria vikao vya
kisheria kupunguzwa hadi Sh10,000 na kuzusha
mabishano.
Pia wametakiwa kurejesha fedha walizolipwa
kwa mawasiliano ya simu Sh150,000 kwa mwezi
tangu Novemba mwaka 2015 hadi Agosti mwaka
huu, ambazo ni sawa na Sh40.8 milioni lasivyo,
Sh50,000 zitakatwa kila mwezi kutoka kwenye
posho zao.
Katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya
Msingi Arusha, hoja kuhusu posho ilitawala
baada ya Meya wa jiji hilo, Kalist Lazaro kutoa
ufafanuzi kuwa zimekuwa zikitolewa tangu
mwaka 2008 wakati wajumbe wengi wakiwa wa
CCM, hivyo kushangazwa na ukubwa wake kwa
sasa wakati baraza hilo likiongozwa na
Chadema.
Kikao hicho kilichoanza saa 4:30 asubuhi hadi
saa 3:43 usiku kilivunja rekodi ya vikao
kufanyika kwa muda mrefu zaidi kutokana na
majibizano. Baadaye baraza hilo lilikaa kama
kamati kutoa azimio dhidi ya mkurugenzi wa jiji
baada ya kumtuhumu kukiuka kanuni naye
akisisitiza anazifuta kikamilifu.
Lazaro amesema hakutakuwa na mabadiliko ya
nyongeza au punguzo kwa stahiki za madiwani
zilizoidhinishwa kisheria kuwawezesha kutimiza
wajibu wao.

Mswada wa mabadaliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari.soma zaid kujua.

Mswada wa mabadaliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari.soma zaid kujua.


Kutoka bungeni Dodoma
Mswada wa mabadiliko ya sheria ya
mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari. Fao
la kujitoa halipo kwenye mapendekezo
hayo, badala yake limeletwa fao la
kutokua na ajira
Inapendekezwa kuwa, mfanyakazi ambaye
amechangia zaidi ya miezi 18 atalipwa
30% ya mshahara wake wa mwisho baada
ya kupoteza ajira. Na atalipwa kwa miezi
6 mfululuzo, baaada ya hapo malipo hayo
yatasitishwa.
Mfanyakazi anayestahili malipo haya, ni
yule tu ambaye hakuacha kazi kwa hiari
yake (resignation)
Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa
fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa
hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha
michango yake kutoka kwenye mfuko wa
lazima (compulsory scheme), kwenda
mfuko wa hiari (supplementary scheme).
Hapo ataruhusiwa kuchukua 50% ya
michango yake.
Hapa ndio wafanyakazi na vyama vya
wafanyakazi tunatakiwa tuunganishe
nguvu kutetea maslahi ya wafanyakazi
ambao hawana ajira za kudumu.

Baraza la wazee wa chadema limesema kuna njama kukifuta chama cha CHADEMA.soma zaid

Baraza la wazee wa chadema limesema kuna njama kukifuta chama cha CHADEMA.soma zaid


Dar es Salaam. Baraza la Wazee wa Chadema
limesema kuna njama za kukifuta chama hicho
zinazopangwa kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Pia, baraza hilo ambalo limekemea vikali njama
hizo na limedai kuwa, Jaji Mutungi anafanya
hivyo ili kutimiza matakwa ya watawala kwa
kutumia mwavuli wa Baraza la Vyama vya Siasa
Tanzania.
Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka
amesema taarifa kuhusu njama hizo
zinathibitishwa na mtiririko wa matukio ya hivi
karibuni kupitia Kamati ya Uongozi ya Baraza la
Vyama vya Siasa.
“Taarifa zimeonyesha kuwa njama hizo zinalenga
kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego
haramu ya kisiasa ili yatolewe mapendekezo ya
kukifuta katika orodha ya vyama vya siasa,”
alisema Lutembeka.
Hata hivyo, Lutembeka amesema Chadema
haitegemei jambo hilo kutokea kwa sababu
inafanya shughuli zake kwa kufuata misingi ya
sheria na Katiba.
Lutembeka amesema miongoni mwa matukio
hayo ni kuahirishwa kwa baadhi ya vikao
vilivyopangwa kufanyika kati ya Jaji Mutungi na
Baraza la Vyama vya Siasa.
Miongoni mambo ambayo yamepangwa
kujadiliwa kwenye mkutano huo, ni changamoto
za mfumo wa demokrasia ya vyama vingi
hususan zuio la shughuli za vyama vya siasa.chanzo mwananch

Watumishi 34 wa mahakama wakiwemo mahakimu 11 wamefukuzwa kazi.soma zaid

Watumishi 34 wa mahakama wakiwemo mahakimu 11 wamefukuzwa kazi.soma zaid

WATUMISHI 34 wa mahakama wakiwemo
mahakimu 11, wamefukuzwa kazi kutokana na
makosa mbalimbali ya kinidhamu.
Aidha, Tume ya Utumishi wa Mahakama
inaendelea kujadili hatma ya mahakimu 30,
waliokuwa wanatuhumiwa kuhusika na rushwa
na kushinda zao mahakamani ili kuangalia kama
walifanya makosa ya kinidhamu.
Jaji Mkuu, Mohammed Chande Othman alisema
hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kupokea
taarifa za ukaguzi wa mahakama pamoja na
uendeshwaji wa mashauri.
Othman alisema watumishi hao, wamefukuzwa
kutokana na uamuzi wa kikao cha Tume ya
Mahakama, kilichofanyika Agosti 18, mwaka huu
baada ya kushughulikia masuala mbalimbali ya
kinidhamu.
“Tumewafukuza mahakimu wakazi wafawidhi,
mahakimu wa mahakama za Mwanzo za
Rombo, Temeke, Bahi na Chamwino na
watumishi wengine 23. Hii ni idadi ndogo
ambayo ni sawa na asilimia 0.005 ya
wafanyakazi wote lakini kwa mahakama ni doa
kubwa,” alisema Jaji Mkuu.
Alisema mahakimu hao wamefukuzwa kwa
makosa mbalimbali ya kinidhamu, ikiwemo
kutumia muhuri wa mahakama kinyume cha
taratibu, kuathiri utendaji wa haki kwa
kumsaidia mtu kufungua kesi moja katika
mahakama mbili pamoja na kufungua kesi ya
mirathi bila kuwa na hati ya kifo.
Aliongeza kuwa kuna makosa ya kisheria
ambayo jaji au hakimu akikosea kutumia kifungu
cha sheria hawajibishwi, lakini kuna makosa ya
kinidhamu ambayo yanaondoa sifa ya kuwa
hakimu au jaji.
Kuhusu mahakimu walioshinda kesi za rushwa
mahakamani, Jaji Chande alisema mahakama
inaweza isiwakute na hatia, lakini Tume
itaangalia kama walifanya vitendo vya ukosefu
wa nidhamu na kuwawajibisha.
Aidha, alisema mahakimu wengine 32 waliokuwa
wanakabiliwa na kesi za jinai na kushinda kesi
mahakamani, wanafunguliwa mashitaka ya
kinidhamu katika Kamati ya Maadili ya Maofisa
wa Mahakama kwa sababu inawezekana
hawajapatikana na hatia ya kosa la jinai, lakini
kama kuna vitendo vya ukosefu wa maadili
watawawajibisha kimaadili.
Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu
Katika hatua nyingine, Mahakama Maalumu ya
Ufisadi na Uhujumu Uchumi imeanza rasmi na
wiki ijayo Kanuni za Uendeshaji wa mahakama
hiyo, zinatarajiwa kuchapishwa. Jaji Mkuu
Othman alisema mahakama hiyo, imeanza rasmi
Julai 18 mwaka huu baada ya Rais John
Magufuli kusaini sheria ya uanzishwaji wa
mahakama hiyo.
“Wiki ijayo tutachapisha kanuni mbalimbali za
uendeshwaji wa mahakama hiyo, ikiwemo jinsi
ya kulinda mashahidi pamoja na taratibu za
ufunguaji wa kesi,” alisema Othman.
Alisema mahakama hiyo itakuwa na majaji wa
kutosha ili kufanya kazi kwa uadilifu na
kumaliza kesi kwa wakati, pia haitakuwa
ikiahirisha kesi mara kwa mara.
Kuhusu utendaji kazi wa mahakama, Jaji Mkuu
alisema mahakama haiwezi kutoa haki kama
itakuwa inajificha au kuendeshwa kwa siri, ndiyo
maana kwenye maboresho ya mahakama,
wameamua kuwapa fursa wananchi kutoa
mapendekezo au kero zao kupitia namba za
simu pamoja na barua pepe.
Kesi za uchaguzi Awali akiwasilisha taarifa za
utendaji wa Mahakama Kuu, Mahakama za
Hakimu Mkazi, Wilaya na za Mwanzo, Msajili wa
Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta alisema baada ya
uchaguzi, walipokea kesi 247 za uchaguzi, 53
za kupinga matokeo ya ubunge na 194 za
udiwani.
Mugeta alisema tayari wameshamaliza kesi 234,
zimebaki 13, lakini hadi kufikia Desemba mwaka
huu kesi zote zitakuwa zimemalizika.
Aidha, alisema tathmini waliyoifanya inaonesha
kesi zilizopo zinawiana na mahakimu, na kama
watawezeshwa kwa vifaa vya kutendea kazi
hadi Desemba mwaka huu watamaliza kesi zote
zilizofunguliwa mwaka huu.
Mahakama ya Rufaa Kwa upande wake, Msajili
wa Mahakama ya Rufaa, John Kahyoza alisema
kiwango cha kumaliza mashauri katika
Mahakama ya Rufaa kimeongezeka, pia wana
lengo la kuhakikisha nakala za hukumu
zinapatikana siku hukumu na ndani ya siku tatu
zitapatikana kwenye tovuti ya Mahakama ya
Tanzania.
Aidha, aliwaomba wananchi watoe ushirikiano ili
rufaa zisikilizwe na kuisha mapema, kwa sababu
kuna watu wanashindwa kufika mahakamani bila
sababu za msingi au kutoa visingizio jambo
linalosababisha rufaa zao kuchelewa.
Umuhimu wa mahakama Katika hotuba yake
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari
4, mwaka huu, Rais Magufuli alisema
anaitegemea sana Mahakama na aliwaambia
majaji na mahakimu nchini kuwa:
“Nawaomba waheshimiwa majaji na
waheshimiwa mahakimu, muitangulize Tanzania
kwanza. Mkiitanguliza Tanzania kwanza
tutaweza kufika mbali na tutaweza kuwasaidia
watanzania wengi. Nimeamua nchi iende, na
itaenda. Anayefikiri ataikwamisha, atakwama
yeye kwa sababu Mungu yuko pamoja na mimi.
Na watu ninaowategemea sana ni Mahakama.
Mahakama unafunga kila mmoja. Hata Rais
nikitaka kufungwa na Mahakama, nafungwa.
Mbunge anafungwa, nani anafungwa, nyinyi ndio
wenyewe”.

Kupunguzwa kwa nauli kumesababisha mabishano kwa madiwani Arusha.soma zaid

Kupunguzwa kwa nauli kumesababisha mabishano kwa madiwani Arusha.soma zaid

Arusha. Sakata la posho za madiwani katika Jiji
la Arusha limekuwa shubiri kwa madiwani baada
ya kiwango walichokuwa wakipokea cha
Sh60,000 kwa nauli za kuhudhuria vikao vya
kisheria kupunguzwa hadi Sh10,000 na kuzusha
mabishano.
Pia wametakiwa kurejesha fedha walizolipwa
kwa mawasiliano ya simu Sh150,000 kwa mwezi
tangu Novemba mwaka 2015 hadi Agosti mwaka
huu, ambazo ni sawa na Sh40.8 milioni lasivyo,
Sh50,000 zitakatwa kila mwezi kutoka kwenye
posho zao.
Katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya
Msingi Arusha, hoja kuhusu posho ilitawala
baada ya Meya wa jiji hilo, Kalist Lazaro kutoa
ufafanuzi kuwa zimekuwa zikitolewa tangu
mwaka 2008 wakati wajumbe wengi wakiwa wa
CCM, hivyo kushangazwa na ukubwa wake kwa
sasa wakati baraza hilo likiongozwa na
Chadema.
Kikao hicho kilichoanza saa 4:30 asubuhi hadi
saa 3:43 usiku kilivunja rekodi ya vikao
kufanyika kwa muda mrefu zaidi kutokana na
majibizano. Baadaye baraza hilo lilikaa kama
kamati kutoa azimio dhidi ya mkurugenzi wa jiji
baada ya kumtuhumu kukiuka kanuni naye
akisisitiza anazifuta kikamilifu.
Lazaro amesema hakutakuwa na mabadiliko ya
nyongeza au punguzo kwa stahiki za madiwani
zilizoidhinishwa kisheria kuwawezesha kutimiza
wajibu wao.

Sunday, September 4, 2016
TRA yakusanya sh.1.158 trillion kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.

TRA yakusanya sh.1.158 trillion kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.


Mamlaka ya mapato nchni TRA imekusanya
shilingi trilioni 1.158. Katika kipindi cha mwezi
agosti mwaka huu ikilinganishwa na lengo la
shilingi trilioni 1.152 ambayo ni sawa na asilimia
100.57 kuitokana na mikakati mizuri iliyowekwa
na uongozi wa TRA kwa kushirikiana na serikali
kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari,mkurugenzi
wa huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA Bwana
Richard Kayombo amesema mamlaka hiyo
imeweka mikakati endelevu ya kukusanya
mapato ikiwemo kulifanya eneo la Kariakoo kuwa
mkoa maalumu wa kodi kutokana na eneo hilo
kuwa kitovu cha biashara na kuhakikisha kila
mfanyabiashara anakuwa na mashine ya
kieletroniki ya kodi na kuitumia ipasavyo.
Aidha akielezea kuhusu mapato yatokayo na
Bandari Bwana Kayombo amesema licha ya
kupungua kidogo kwa bidhaa zinazotumika hapa
nchni ,mapato ya serikali yameongezeka
kutokana na idadi ya mizigo inayoingia kutozwa
kodi na kusisitiza toka kuanza kutozwa kodi hapa
nchni mizigo inayoenda nchi za jirani, mizigo ya
inayoenda jamhuri ya kidemokrais ya kongo
pekee ndio imepungua lakini nchni nyingine zote
ikiwemo Rwanda,Uganda,Burundi imezidi

G-20 Economic Summit Opens Amid Sluggish Gwowth.readmore.

G-20 Economic Summit Opens Amid Sluggish Gwowth.readmore.


HANGZHOU, China — Chinese President Xi
Jinping called Sunday for leaders of the United
States, Germany and other major economies to
resist pressure to raise trade barriers as they
opened a summit amid sluggish global growth
and disputes over China's steel exports and
Apple's Irish tax bill.
China made trade a theme of the Group of 20
meeting even as Beijing faces complaints it is
flooding world markets with low-cost steel,
fueling demands for trade curbs. The president
of the European Commission highlighted the
conflict by calling for the summit to take action.
Opening the two-day meeting in this lakeside city
southwest of Shanghai, Xi called for more
innovation to spur economic growth and reforms
to global financial and economic management.
He appealed for cooperation in taxes, anti-
corruption and measures to "improve the ability
of the world economy to resist risks."

TANESCO wameanza kazi ya uboreshaji wa miundo mbinu wa umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoaza umeme ubungo Dar.soma zaid

TANESCO wameanza kazi ya uboreshaji wa miundo mbinu wa umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoaza umeme ubungo Dar.soma zaid

Wahandisi na mafundi wa Shirika la Umeme
Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na
mafundi wa kampuni za Kijapani za Yachiyo
Engineering Co Limited, Takaoka na National
Construction Co. Limited, wameanza kazi y
uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo
kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha
Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha
laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme
mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine
muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze
kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.
“Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini
mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa
kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila
moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha
Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili
njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na
uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye
Megawati 220 kila moja,” alifafanua Meneja
Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika
hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa
kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia
Theodory Bayona.
Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii
itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa
kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na
jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili,
tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa
kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,”
alisema.
Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam,
watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio
bora, alifafanua Injinia Bayona.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la
Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila
Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya
juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika
wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake.
“Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi
katika mazingira salama, tutakuwa tukikata
umeme kuanzia leo hii Septemba, 3 na umeme
utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na
kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe
kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11,
Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.”
Alifafanua Leila, na kuwaomba wananchi kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki.
Mradi huu ulioanza Februari 2015 na
unaotarajiwa kukamilika Juni 2017
unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA)
.

Mwenyekiti wa mtaa anatuhumiwa kwa kumumwagia tindi kali katibu wa CCM tawi la Nyantorotoro mkoani Geita.soma zaid

Mwenyekiti wa mtaa anatuhumiwa kwa kumumwagia tindi kali katibu wa CCM tawi la Nyantorotoro mkoani Geita.soma zaid

Geita. Polisi mkoani Geita, inamshikilia
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorotoro A, Gervas
Kaiyelelo kwa tuhuma za kummwagia tindikali
Katibu wa CCM Tawi La Nyantorotoro, Kulwa
Kazinga kwa kile kinachodaiwa ni uhasama wa
kisiasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,
Herman Kapufi alisema tukio hilo lilitokea Agosti
31 usiku, wakati katibu huyo akielekea
nyumbani kwake. Kapufi alisema uchunguzi wa
awali unaonyesha chanzo cha tukio hilo ni
uhasama wa kisiasa baina ya mwenyekiti huyo
ambaye ni wa Chadema na katibu wa CCM.
Akizungumza kwa shida kutokana na majeraha
aliyoyapata ikiwamo kuungua maeneo ya uso na
kifuani, Kazinga alisema siku hiyo akiwa na
jirani yake aliyemtaja kwa jina la Selestine
Misungwi wakitokea makao makuu ya kata hiyo,
alitokea mtu msituni na kummwagia majimaji
ambayo yalianza kumuwasha na alihisi
maumivu makali.

Saturday, September 3, 2016
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametangaa hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametangaa hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14.


Rais wa Filipino Rodrigo Duterte ametangaza
hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14
yaliyotokea kwenye mlipuko wa bomu katika mji
wa Davao nchini humo.
Abu Sayyaf anayejiita mwenye msimamo mkali
amedai kuhusika na shambulio hilo. Licha
Sayyaf kutangaza kuhusika, mamlaka za
usalama nchini humo zimeahidi kuangalia
watuhumiwa wengine zaidi.
Mlipuko huo ulitokea majira ya usiku karibu na
maeneo ya soko, chuo kikuu na hoteli yenye
hadhi ya nyota, na kuua watu 14.
Chuo hicho kinachofahamika kwa jina la Ateneo
de Davao University na hoteli Marco Polo,
inadaiwa kutumiwa na rais Duterte kwenye ziara
zake nyingi na hoteli hiyo ilitumika kwa ajili ya
mikutano wakati wa kampeni za Uchaguzi wake
wa kitaifa.
Rais Duterte aliviambia vyombo vya habari
nchini humo kuwa, amelazimika kutangaza hali
ya vurugu kutokana na vitendo vya kihalifu
vilivyotokea nchini humo.
Duterte leo amewaambia waandishi wa habari
katika mji wa Davao kuwa ‘Ni tishio dhidi ya
watu na dhidi ya taifa nitachukua hatua kali
dhidi ya waliohusika na shambulio hilo, nina
wajibu huu ili kulinda nchi hii .’
Msemaji wa Abu Sayyif alisema walihusika na
mlipuko huo, na kudai kuwa Kundi
linaloongozwa na Sayyif limetishia kuanzisha
mashambulizi baada ya wapiganaji wake 30
kuuawa katika mashambulizi ya kijeshi
yaliyotokea wiki iliyopita.
Hata hivyo, Duterte amesema wakaguzi
wanaendelea kuangalia watuhumiwa wengine
zaidi ili kuthibitisha kama wahalifu wa dawa za
kulevya walihusika.
“Hizi ni nyakati za ajabu, na mimi nina mamlaka
ya kuruhusu vikosi vya usalama wa nchi hii
kufanya upekuzi, na tutakabiliana na mgogoro
uliopo sasa,”
Aliongeza. “Kuna mgogoro katika nchi na
washirika wa madawa ya kulevya, ambao
wanafanya mauaji yasiyo halali na inaonekana
kuwa bado kuna mazingira ya vurugu kutoka
kwa wahalifu.”
Tangu uzinduzi wake kama rais wa kupambana
na wafanyabiashara wa dawa za kulevya
mwishoni mwa mwezi Juni,2016, watu 2,000
wameuawa hadi sasa.

Pope Francis led prayer vigil for Mother Teresa ni St.Peter's Square.readmore.

Pope Francis led prayer vigil for Mother Teresa ni St.Peter's Square.readmore.

P ope Francis led a prayer vigil for Mother Teresa
in St. Peter's Square at the Vatican on Saturday,
attended by thousands of faithful.
The Pope is urged people to resist what "the
temptation to indifference" to suffering in a
speech on the eve of a ceremony to formally
proclaim Mother Teresa a saint.
Indian nuns of Missionaries of Charity gesture as
they sing rhymes standing beside a big potrait of
the late Mother Teresa while taking part in a
prayer to observe her 8th death anniversary, at
Mother House in Kolkata CREDIT: DESHAKALYAN
CHOWDHURY/AFP
Greeting thousands of lay volunteers from
around the world in St. Peter's Square, Francis
Saturday said that ignoring those suffering
hunger, sickness or exploitation is a "modern sin,
a sin of today."
The square hosts a ceremony Sunday expected
to draw hundreds of thousands of admirers of
Mother Teresa, a nun who before her death in
1997, cared for the destitute who were dying in
the streets of India.

Dhamira ya serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka 4.soma zaid

Dhamira ya serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka 4.soma zaid

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(mb) amesisitiza kuwa dhamira ya
Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale
ndani ya kipindi cha miaka minne hatua
kwa hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari
Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake
eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri
Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa
Dodoma, Waziri Mhagama alisema
“Watanzania wawe na amani, dhamira
yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais
alivyosema na tunawahakikishia
kwamba ndani ya kipindi hicho sisi
tumeshajipanga kuhamamia mkoani
Dodoma hatua kwa hatua”.
Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli
za maendeleo hazitosimama kwa
kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya
Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba
mipango yote ya maendeleo haitosimama
na shughuli zote za maendeleo
hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani
Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa
na tutaendelea kuyafanya hayo kwa
kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia
Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza
Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
ameahidi kutekeleza usimamizi wa
maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi
wa barabara kwa wakati “kwa upande
wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha
kuwa ujenzi wa barabara unakamilika
na tutakutana na Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji
Mji (CDA) na Manispaa ili kuona
shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza
maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya
majukumu ya mkoa.”
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri
Mhagama kwa kutembelea maeneo ya
makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na
Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri
Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote
ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na
kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi
wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri
Mkuu.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)
akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi
Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa
Kassim kutoka kwa Wataalam wa
maswala ya Ujenzi kulia kwake ni
Mhandisi Joseph Muhamba na wa
kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana
wakati wa Ziara yake katika makazi
hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.

Nzega# mwanamke moja Veronica Dala auwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika.soma zaid

Nzega# mwanamke moja Veronica Dala auwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika.soma zaid


Watu wasiofahamika wamemkata mapanga
mjane, Veronica Dala(46) na kisha
kuondoka na baadhi ya viungo vya mwili
wake.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kijiji
cha Ilagaja wilayani Nzega, Mkoa wa
Tabora.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, JUma Seleli
alisema jana kuwa tukio la kuvamiwa ni la
pili kumtokea Dala kwa aliwahi kuvamiwa
na kujeruhiwa.
Chanzo cha mauaji hayo bado
hakijafahamika.

Bodi ya mikopo kutoa fedha kwa waombaji chuo kikuu  waliokidhi vigezo.soma zaid

Bodi ya mikopo kutoa fedha kwa waombaji chuo kikuu waliokidhi vigezo.soma zaid


Bodi ya Mikopo kumwaga fedha kwa
waombaji wote
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo
mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq
Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa
hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano
waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa
mkupuo na kwa hiari.
Badru alisema idadi ya walioomba mkopo
mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi
itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo,
wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.
Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza
walionufaika na mikopo kulipa madeni yao,
alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa
ni 55,000.
Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya
kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA
Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa
mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh
15,115,200.
Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga
aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe
ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha
Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.
Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar
Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa
ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema
amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao
walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo
kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo
kukopesha wanafunzi wengine.
Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi
hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha
vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi
watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na
mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake,
Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge
wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.

Friday, September 2, 2016
MNADA# Kama uko Dar leo ijumamosi tareh 03.9.2016 kuna mnada wa magari na vitu mbalimbali.soma zaid

MNADA# Kama uko Dar leo ijumamosi tareh 03.9.2016 kuna mnada wa magari na vitu mbalimbali.soma zaid

Tunapenda kukujulisha mnada wa Magari
pamoja na Furniture mbalimbali za ofisi
na majumbani, mali kutoka Ubalozi
wa Canada, Sweden na Finland.Mnada
utafanyika Jumamosi ya wiki hii tarehe
03.09.2016 kuanzia saa 4 asubuhi.
Mahali: Golden Resort, Lion Street, Sinza
( Nyuma ya Lion Hotel) jijini Dar es
salaam.chanzo michuzi blog

Majambazi yaua walinzi na kuteketeza mabweni.

Majambazi yaua walinzi na kuteketeza mabweni.

Lushoto. Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele
Security ya Tanga, ameuawa kwa kupigwa risasi
na majambazi waliovamia Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu)
wilayani hapa usiku wa kuamkia jana.
Majambazi hao ambao idadi yao inakadiriwa
kuwa kati ya 10 hadi 15, walivamia mabweni
mawili waliyokuwa wakilala wanafunzi
wasichana kisha kumwaga petroli katika
mabweni hayo na kulipua kwa kiberiti bweni
moja ambalo halikuwa na watu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,
Benedict Wakulyamba alisema tukio hilo lilitokea
saa tano usiku wa kuamkia jana katika mabweni
yaliyo jirani na ofisi kuu ya chuo hicho. Mlinzi
aliyeuawa ni Yohana Shemzigwa (34) na
mwenzake, Abuu Rajab (33) alijeruhiwa.

no image

Mkurugenzi wa Yamoto bandi mkubwa Said Fella ameziweka hadharani nyumba tano za wasanii wake Yamoto Bandi.soma zaid

MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na
Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani
nyumba takribani tano za wasanii wake
wa kundi la Yamoto Band na kuwataka
wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji
nyumba na sio magari.
Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji
kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema
kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa
wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza
kuwazawadia nyumba wasanii wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa
ameamua kuziweka wazi hasa baada ya
kusikia maneno mengi kutoka kwa
wananchi wakidai kuwa Yamoto Band
hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.
Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka
sasa hajajua thamani yake ila
zitakapokamilika ataita watu wa tathmini
kwa ajili ya kuziangalia ili kujua
zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.
Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa
Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
kwa juhudi kubwa sana alizozifanya
katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua
wasanii. Na katika nyumba hizo
zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa
kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na
Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.
Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani
Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi
nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii
wenyewe wanazozipata kwenye shoo za
muziki wanazozifanya na sio kama hela
zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga
Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na
hatua hii kwani ni mara chache sana kwa
viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya
kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo
na amewataka wasanii kutokufanya
mzaha kwenye tasnia hii.

Taarifa ya Jeshi la kujenga (JWTZ) kuhusu chapicho la Gazet la Tanzania Daima septemba mosi.soma zaid

Taarifa ya Jeshi la kujenga (JWTZ) kuhusu chapicho la Gazet la Tanzania Daima septemba mosi.soma zaid

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na
gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari
4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha
shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika
maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa
kwake na shughuli za kisiasa.
Tunapenda kuwataarifu wananchi
kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na
kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya
nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa
kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na
sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya
juu, hivyo lisihusishwe na propaganda
zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye
maadili ya kitaasisi ya hali ya juu.
Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya
kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na
wanasiasa ni wakati linapotetea na
kulinda maslahi ya wananchi. Inaombwa
kuwa makini katika utoaji wa maelezo au
malalamiko, iachwe mara moja vyama
vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.
Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila
mwaka ni siku ya kuwakumbuka
Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili
kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta
mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa
mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi
kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita
vya Kagera.
Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji
wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo
Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera
ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku
ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria,
ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa
ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana
tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa
JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara
moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na
mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa
wekeni kumbukumbu zenu vizuri.
Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri
wakasoma vema historia ya nchi
wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza
ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno
yanayotolewa na viongozi wa kisiasa
wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli
za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na
kiungulia, awe makini kuongea vitu
ambavyo haelewi na kutokuwa makini
zaidi aelewe madhara yanayoweza
kutokea kutokana na upotoshaji.
Jeshi letu linafanya shughuli zake ki
weredi.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na
Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.chanzo michuzi blog

CUF yaondolewa kupisha mkutano wa Rais Magufuli Pemba.soma zaid

CUF yaondolewa kupisha mkutano wa Rais Magufuli Pemba.soma zaid

Jeshi la Polisi Wilaya ya Chakechake, Pemba
limezuia kufanyika mkutano na vyombo vya
habari wa Chama Cha Wananchi (CUF) uliokuwa
umepangwa kufanyika leo wilayani humo,
kupisha ziara ya Rais John Magufuli
itakayoanza leo.
Rais Magufuli anatarajia kuanza leo ziara yake
ya kwanza visiwani humo tangu achaguliwe
kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi
ya Ikulu, Rais Magufuli atazulu Pemba leo na
kesho atakuwa Unguja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba,
Shekhani Mohamed Shekhani amesema kuwa
zuio hilo la mkutano wa CUF ni kwa sababu
eneo wanalotarajia kutumia liko jirani na eneo la
uwanja atakaokuwa akihutubia Rais Magufuli.
Hata hivyo, Katibu wa CUF wilaya ya Chake
Chake, Saleh Nassor Juma alilalamikia maamuzi
hayo ya Jeshi la Polisi kwa madai kuwa wao
walitaka kufanya mkutano na vyombo vya habari
na sio mkutano wa hadhara. Alisema kuwa
tayari walishawaeleza Idara ya Habari Maelezo
na waliridhia.
Alisema mkutano huo na waandishi wa habari
ulilenga katika kutoa tamko lao kuunga mkono
uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la chama
hicho kumsimamisha uanachama aliyekuwa
Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba
pamoja na viongozi wengine 10.
“Niliwakatalia kwa hoja kwamba mkutano na
waandishi wa habari ni haki yetu ya kikatiba na
tulikwishawataarifu watu wa Idara ya Habari
Maelezo juu ya kikao hicho halali ambacho wao
pamoja na waandishi wa habari walithibitisha
kuwa watahudhuria,” alisema Nassor.
Idara ya Habari Maelezo ilithibitisha kuwa
walikubali kufanyika kwa mkutano huo wa CUF
na vyombo vya habari lakini baadae walipokea
taarifa ya kuahirisha kupisha ugeni wa Rais
Magufuli.

Ijue sifa ya Wilaya ya Muleba mkoani kagera

Ijue sifa ya Wilaya ya Muleba mkoani kagera

Picha unayoiona ni maeneo ya standi ya muleba mkoani Kagera nikiwa katika shughuli yangu ya kiza nilibahatika kufika katika standi ya muleba ambapo watu wake katika maeneo hayo kila mmoja wanateleza kauli mbiu ya hapa kazi tu ambapo kila mmoja anafanya kazi ilimradi aweze kiingiza kipato nilifurah kuona wananchi wafikifanya kazi muleba ni wilaya kubwa yenye Ardhi nzuri asilia kubwa ya watu wake ni wakulima na mazao makubwa nia Kahawa na Ndizi,lugha kubwa wanayoitumia katika mawasiliano ni kihaya.

Back To Top