Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Thursday, March 31, 2016
Habari kutoka ikulu  jumaa  bwando asimamishwa kazi.soma zaid.

Habari kutoka ikulu jumaa bwando asimamishwa kazi.soma zaid.


RAIS Dk. John Magufuli, amefanya mabadiliko
mengine Ikulu jijini Dar es Salaam kwa
kumwondoa aliyekuwa Mnikulu, Jumaa Bwando.
Vyanzo vya habari kutoka Ofisi ya Rais
vimesema Bwando, aliondolewa katika wadhifa
huo Machi 14, 2015, ambapo kwa sasa nafasi
hiyo inakaimiwa na mmoja wa maofisa wa juu
wa Ikulu.
Julai 10 mwaka jana, Bwando aliteuliwa kushika
wadhifa huo na Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete,
kuchukua nafasi ya Shaban Gurumo,
aliyeng’olewa baada ya kukiuka sheria ya maadili
ya viongozi wa umma inayokataza kiongozi wa
serikali kupokea zawadi zaidi ya zawadi
ndogondogo na ukarimu wa kawaida.
Kazi ya Mnikulu ni kusimamia majengo yote ya
Ikulu kwa maana ya shughuli za utawala. Yeye
ndiye anayehusika na usafi, samani na mapambo
yote katika ofisi hiyo kuu ya nchi.
Ni mtu anayeweza kuamua mwonekano wa Ikulu
uonekanaje, hata kupanga na kuamua aina ya
nguo, mashuka, mapazia yanayopaswa kutumiwa
na Rais. Kwa majukumu husika anapaswa amjue
vizuri Rais.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli ni mwendelezo wa
mabadiliko aliyoanza kuyafanya Ikulu siku chache
baada ya kuingia madarakani.
Tayari amezifumua na kuziunda upya baadhi ya
ofisi za Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam
pamoja na kuwaondoa baadhi ya watumishi
ambao hawana ulazima katika mfumo wa
utumishi wa Ikulu.
Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi
moja baada ya nyingine zilizopo Ikulu, huku
akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na
aina ya watendaji waliopo.
Katika ukaguzi huo, Rais Magufuli aliamuru
kufungwa mara moja kwa baadhi ya ofisi
alizobaini kuwa hazina tija na kwamba zina
watumishi ambao ni mizigo.
Baadhi ya ofisi zinazodaiwa kufungwa ni pamoja
na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha Rais na
ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni
binafsi wa Rais.
Wakati akifanya mabadiliko hayo, Ofisa mmoja
wa Ikulu alinukuliwa na gazeti hili akisema. “Rais
Magufuli alipoingia tu Ikulu alifanya ziara ya
kukagua ofisi zote zilizopo Ikulu, alitaka kujua
utendaji kazi wa ofisi hizo, lakini alipofika kwenye
kitengo maalumu cha lishe ya Rais, alisema
haoni umuhimu wa kuwepo kwa ofisi hiyo kwa
sababu suala la lishe yake siku zote
linasimamiwa na mkewe Janeth.
“Akaamuru ifungwe na watumishi wake
warejeshwe walikotoka. Ofisi nyingine aliyoamuru
ifungwe ni kupokea wageni binafsi wa Rais.
Alisema haoni tija ya kuwepo kwa ofisi hiyo kwa
sababu mgeni anatakiwa kufika Ikulu baada ya
kutoa taarifa, nayo aliamuru ifungwe,” alisema
ofisa huyo.
Taarifa zilisema aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha
Lishe Ikulu alirudishwa katika ajira yake ya awali
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, huku
watumishi wengine wakipelekwa Wizara ya Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
MTANZANIA ilipomtafuta Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, ili kupata
ufafanuzi wa suala hilo, alijibu kwa kifupi kuwa
“Nalifanyika kazi swali lako kisha nitakupatia
ufafanuzi baada ya muda,” alisema Msigwa,
ambapo baada ya muda alipopigiwa simu.

Migogoro ya aridhi kuisha hapa nchini.soma zaidi.

Migogoro ya aridhi kuisha hapa nchini.soma zaidi.

Serikali imesema urasimishaji wa hati za
ardhi za kimila ni moja ya hatua ya kuhakikisha
inamaliza migogoro ya ardhi nchini huku ikisema
imejipanga pia kuhakikisha inaweka utaratibu
mzuri wa ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa
wakulima na kwa wakati.chanzo itv.

Rwanda imemfunga jela askari aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha kumlinda Rais kagame miaka 21.

Rwanda imemfunga jela askari aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha kumlinda Rais kagame miaka 21.

Aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha ulinzi
wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba,
amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na
kuvuliwa cheo chake baada ya kupatikana na
hatia ya kuharibia sifa nchi hiyo na kuhamasisha
wananchi kupinga utawala.
Kesi hiyo ilimhusisha pia brigedia jenerali
mstaafu Frank Rusagara ambaye naye
amepatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 20
jela.
Maafisa hao wa jeshi wamepinga hukumu hiyo
wakisema mashtaka dhidi yao yalichochewa
kisiasa.
Mahakama imeunga mkono hoja za upande wa
mwendesha mashtaka kwamba mlinzi wa muda
mrefu wa Rais Kagame, Kanali Byabagamba,
alihusika na makosa matatu ambayo ni kueneza
kampeni za chuki dhidi ya utawala ambazo
zingesababisha wananchi kugoma dhidi ya
serikali ya nchi hiyo na kutoheshimu bendera ya
nchi hiyo.
Brigedia jenerali mstaafu Frank Rusagara naye
amepatikana na makosa kama hayo pamoja na
kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Awali alikiri kumiliki bastola mbili alizopewa kama
zawadi na nchi za Afrika Kusini na Israel, wakati
alipokuwa afisa mkuu anayehusika na ununuzi wa
silaha katika wizara ya ulinzi ya Rwanda.
Maafisa hao wamekata rufaa baada ya
mahakama kutangaza hukumu hiyo

Bado kunahitajika mikakati mizito kuhusu utoaji Elimu bure.soma zaid.

Bado kunahitajika mikakati mizito kuhusu utoaji Elimu bure.soma zaid.

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Zawa
wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wanalazamika
kusoma madarasa matatu katika chumba kimoja
kwa kupeana migongo na kutumia mbao mbili
tofauti wakati walimu wakifundisha kutokana na
changamoto ya vyumba vya madarasa ambapo
shule hiyo ina vyumba vitatu yenye wanafunzi
513.chanzo itv

Sababu 10 kwanini wanaume wanakuwa wenye furaha zaidi mda wote.soma zaid.

Sababu 10 kwanini wanaume wanakuwa wenye furaha zaidi mda wote.soma zaid.

SABABU 10 ZA KWA NINI WANAUME NI VIUMBE
WENYE
FURAHA ZAIDI
1. Majina yao ya ubini hubaki vivyo hivyo siku
zote za
maisha yao.
2. Maongezi yao kwenye simu huhitaji sekunde
30 tu
kulizungumza jambo lililowafanya kupiga simu.
3. Safari yao ya siku 5 huwahitaji kusafiri na
suruali
moja tu ya jinsi.
4. Endapo rafiki yao atasahau kuwaalika katika
tafrija
fulani, bado wataendelea kuwa marafiki.
5. Mtindo wao mmoja wa nywele hudumu
kichwani kwa
miaka mingi na pengine maisha yao yote na
bado
wakitokea mbele za watu huwa na amani kuwa
wamependeza.
6. Hata kama wanahitaji kuwafanyia shopping
ndugu 25
wao hutumia dakika 25 tu na shopping
ikamalizika kwa
mafanikio.
7. Huwa hawakasiriki wala kujisikia vibaya
wakienda
kwenye tafrija na kukutana na mwanaume
mwingine
aliyevaa shati kama yeye, zaidi hapo urafiki
huanza.
8. Wakisikia jambo hulimezea mate, hawahitaji
kuwasimulia watu wengi zaidi.
9. Wakiwa wanataka kwenda kwenye mtoko
mahali
hawahitaji kutumia saa nzima kabatini ili
kuchagua
nguo ya kuvaa.
10. Wakihitaji kuwa na uhusiano hawahitaji
kutumia
miezi mingi ili kufanya maamuzi juu ya nani wa
kuwa
naye.
MWISHO
Wakiambiwa ukweli juu ya vile walivyo
hawahitaji
kununa ili kuonesha hisia zao

Askari wa usalama wakiwa doria huku Rais kenyatta akiendelea kuhutubia bunge.

Askari wa usalama wakiwa doria huku Rais kenyatta akiendelea kuhutubia bunge.

Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru
Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada
ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi.
Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na
kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza
kuitoa.
Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge
ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi.
Hata hivyo utulivu ulirejea baada ya spika
kuwatupa nje wabunge waliokua wakizipuliza
hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba
yake kwa taifa.chanzo bbc.

Filimbi zimerindima bungeni kenya wakati Rais kenyatta akihutubia bunge.soma zaid.

Filimbi zimerindima bungeni kenya wakati Rais kenyatta akihutubia bunge.soma zaid.

Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru
Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada
ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi.
Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na
kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza
kuitoa.
Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge
ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi.
Hata hivyo utulivu ulirejea baada ya spika
kuwatupa nje wabunge waliokua wakizipuliza
hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba
yake kwa taifa.chanzo bbc swahil.

Baada ya MCC nchi 10 za magharibi  nazo zasitisha ufadhili wa misaada kwa Tanzania.soma zaid.

Baada ya MCC nchi 10 za magharibi nazo zasitisha ufadhili wa misaada kwa Tanzania.soma zaid.

March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la
Changamoto za Milenia ( MCC) ilisitisha msaada
wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa
Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni
kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya
malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria
mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la
Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika
ripoti ifuatayo >>> ‘kundi la watoa misaada 10
kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha
ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania,
hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada
la serikali ya Marekani kuondoa msaada
kutokana na uchaguzi wa Zanzibar
ulivyoendeshwa‘
‘ Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania
ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo
hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya
maendeleo ya serikali mpya ‘ – BBC SWAHILI

Rais jacobo zuma atishiwa kuvuliwa madaraka ya urais nchini Afrika kusini.

Rais jacobo zuma atishiwa kuvuliwa madaraka ya urais nchini Afrika kusini.

Chama cha Democtratic Alliance nchini Afrika
Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais
Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya
kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba.
Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa
kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha
mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe
pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba
yake ya kibinafsi.
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo
mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma
kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na
mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika
na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya
Nkandla.
Mamilioni ya madola yalitumika katika kile
kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa
usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha
ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe

Hii ndio mishahara ya vigogo wa mashirika ya umma.soma zaid.

Hii ndio mishahara ya vigogo wa mashirika ya umma.soma zaid.

Ni mashirika ya umma wanayolipana mishara
minono
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli,
kusema kwamba Serikali inafanya marekebisho
ya viwango vya mishahara kwa watendaji wa
mashirika ya umma, hatimaye
imebainika viwango mbalimbali vya mishahara
wanavyolipana vigogo katika mashirika hao.
Katika mashirika hayo, baadhi ya vigogo hulipana
viwango vikubwa vya mshahara, ambapo kigogo
mmoja hulipwa Sh Sh milioni 36 kwa mwezi na
wengine hufikia kiwango cha Sh milioni 40 kama
alivyoeleza Rais Magufuli juzi.
Akizungumza na wananchi wa Chato, Dk.
Magufuli alisema watu hao wanaolipwa kiwango
kikubwa cha mishahara wamekuwa wakiishi
kama malaika na sasa ni lazima washushwe ili
waishi kama shetani.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Serikali
kiliambia MTANZANIA kuwa, ulipwaji wa viwango
vikubwa kwa watendaji wa mashirika ya umma
umetengeneza tabaka kubwa la wenyenacho na
wasionacho.
Uamuzi huo wa Rais Magufuli, umetajwa kuwa
huwenda ukaleta heshima na utu kwa
Watanzania, kwani baadhi ya taasisi na mashirika
ya umma watendaji wake wa ngazi za juu
wameonekana kulipana mishahara ya kufuru.
“Kuna taasisi watendaji wa ngazi za juu
wamekuwa wakilipwa mishahara minono zaidi
ambapo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
hulipana Shilingi milioni 24 kwa mwezi pamoja na
marupurupu,” kilisema chanzo chetu.
Taasisi nyingine zinazolipwa kiwango kikubwa
kwa watendaji wake ni Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Sh milioni 36, Shirika la Umeme
nchini (Tanesco), Sh milioni 36.
Mashirika mengine ambayo yanaongoza kwa
kulipana kiwango kikubwa ni Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC), Sh milioni 36 na Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
ambapo watendaji wa juu hulipwa Sh milioni 36.
Mbali na taasisi hizo pia timu ya waatalamu ya
Rais Magufuli inaangalia taasisi kama za Mpango
wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), Mamlaka ya
Hifadhi za Taifa (Tanapa), Ngorongoro, Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA), Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH).
Taasisi nyingine ni Benki ya Rasilimali Tanzania
(TIB), Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC),
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Bodi
ya Bima ya Amana, Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Hatua ya Rais Magufuli kupitisha panga na
kuweka uwiyano wa mishahara kwa watendaji wa
taasisi hizo unaelezwa kuwa utaisaidia uwajibikaji
na usawa kwa watendaji.
“Kwa mfano kwa sasa zipo taasisi nyingine
hupandishiana mishara kila wakati, unakuta
mfagiaji analipwa hadi Shilingi milioni Moja,
wakati katika sekta nyingine kama walimu
wanaambulia Shilingi 400,000 kabla ya makato.
“Hatuwezi kujenga Taifa la wenye nacho na
wasio nacho kwa mfumu huu na ikiwa Serikali
italitekeleza hili kama Rais Magufuli alivyoamua
ni wazi sasa tutapiga hatua mbele zaidi,” alisema
mtoa habari huyo.
Azivaa bodi
Kiongozi huyo wa nchi, alishangazwa na baadhi
ya bodi za wakurugenzi kushindwa kufanyakazi
zao kwa mujibu wa sheria na badala yake
wamekuwa na kazi ya kupandisha mishahara kwa
viongozi.
Alisema kutokana na hali hiyo anashangazwa na
bodi hizo kila kukicha zimekuwa zikifanya kazi ya
kupandisha mishahara pamoja na kufanya vikao
nje ya nchi.
Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli ameunda
timu ya wataalamu ambayo imeanza kufanya
kazi ya upunguzaji wa mishahara mikubwa kwa
watendaji wakuu wa mashirika ya umma.
“Tena hawa wakurugenzi ndio wanaongoza kwa
kulipwa fedha nyingi na hata kwenda kufanya
vikao ulaya, ninasema hapa kwamba suala hili
litaanza kushughulikiwa katika bajeti ya hivi
karibuni,” alisema Rais Magufuli.
Juzi akiwa wilayani Chato, Rais Magufuli, alisema
wapo watendaji wanalipwa Sh milioni 40 kwa
mwezi na wengine wanalipwa Sh 300,000.
Alisema tayari ameunda timu ya wataalamu
ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara
hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili
asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya
kiwango hicho.
“Tunafanya hivi ili nyingine tuziteremshe kwa
watu wa chini na yule atakayeng’ang’ania
kwamba lazima alipwe Sh milioni 40 aache kazi
tuweke mtu mwingine,” alisema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli, alishangazwa na watu
namna wanavyolipana kile alichokiita mishahara
ya ajabu kwa kushirikiana na bodi ambazo wakati
mwingine huzihonga fedha ili zipandishe
mishahara yao.
“Kuna watu wanaishi kuliko hata malaika lazima
tuwashushe waishi kama shetani,” alisema Rais
Magufuli.
Pamoja na hali hiyo kiongozi huyo wa nchi
alianika madudu aliyoyakuta ndani ya Serikali
ikiwemo mmoja wa mfanyakazi wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), kulipwa mishahara ya
watu 17 na kuagiza mfanyakazi huyo afikishwe
mahakamani.
Pamoja na hali hiyo alisema wapo watumishi
wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia
hadi Sh milioni 40 kwa mwezi, ambayo sasa
itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha
mshahara usiozidi Sh milioni 15.
Dk. Magufuli alisema Serikali yake imejiandaa
kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa
kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi
asilimia 10 au 9 (single digit) kuanzia bajeti
ijayo.
“Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, uhakiki
mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini
wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa
shilingi bilioni 1 na milioni 800 na kwamba ni
matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima
utaisaidia Serikali kubaini wafanyakazi hewa
wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za
Watanzania.
Alisema anashangazwa na hatua ya baadhi ya
watu kuishi kama malaika huku wengine wakiishi
kama masheteni, jambo ambalo alisema halina
nafasi katika Serikali yake.
“Nyiye mliokuwa mnaishi kama malaika, sasa
zamu yenu kuishi kama mashetani,” alisema Dk.
Magufuli huku akishangiliwa na umati wa
wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.chanzo mtanzania

Uchumi wa Afrika umekuwa asilimia 4.5 lakin wananch wake ni masikini.

Uchumi wa Afrika umekuwa asilimia 4.5 lakin wananch wake ni masikini.

Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia
inaonesha kuwa Afrika ina wastani wa ukuaji wa
uchumi wa asilimia 4.5 kwa mwaka huku
ikikabiliwa na masuala ya umaskini.
Ripoti hiyo imesema,Afrika imepata maendeleo
makubwa katika sekta za afya, lishe, elimu na
mgawanyo wa madaraka, lakini maendeleo ya
uchumi wake hayajasaidia kwa ufanisi
maboresho ya maisha wa watu.chanzo radio one.

Hivi mbunge kupokea rushwa ni tamaa au nini?hawa ndio wabunge wanaotuhumiwa na waburuzwa na Takukuru mahakamani.soma zaid.

Hivi mbunge kupokea rushwa ni tamaa au nini?hawa ndio wabunge wanaotuhumiwa na waburuzwa na Takukuru mahakamani.soma zaid.

Baadhi ya wabunge ambao uchunguzi
umeshakamilika wanapelekwa
Mahakamani leo hii.
Ni wabunge wa Kamati za kudumu za
Bunge wanaotuhumiwa kushawishi na
kupokea rushwa kwa Taasisi za Kiserikali
ili kuweza kusaidia taarifa zao ambazo
zinamapungufu zipitishwe bila kupingwa
Watapelekwa kwa mafungu (yaani si wote
kwa pamoja) bali in groups.
Taarifa zaidi itawajia soon
===========
UPDATES:
===========
Wabunge waliopandishwa Mahakama ya
Kisutu ni Victor Mwambalaswa, Sadiq
Murad na Kangi Lugola Mbunge wa
Mwibara.

Wednesday, March 30, 2016
Tanzania yapania kuimarisha usafiri wa anga baada kuahidi ndani ya miezi 2 ijayo wanunua ndege mpya 2 kutoka canada.soma zaid.

Tanzania yapania kuimarisha usafiri wa anga baada kuahidi ndani ya miezi 2 ijayo wanunua ndege mpya 2 kutoka canada.soma zaid.


Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano
ya ushirikiano wa anga na Serikali ya
Quwait.
Makubaliano hayo yatawezesha mashirika
ya ndege ya nchi zote mbili kufanya safari
za moja kwa moja na kukuza sekta ya
utalii.
Wakati hayo yakijiri, Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi imethibitisha
kwamba imeagiza ndege za kisasa kutoka
nchini Canada ambazo zinatarajiwa
kuwasili nchini ndani ya siku 60 (miezi
miwili ijayo).
Kwa kuanzia, awamu ya kwanza ya ndege
hizo zitafanya safari za ndani bara na
visiwani kabla ya kujitanua ndani na nje
ya Afrika.
Shime watanzania, tusimame kidete na
serikali yetu kuhakikisha kwamba
tunaachana na unyonge wa kutumia
ndege za mashirika ya nchi jirani. Hii ni
fursa nzuri ya uwekezaji katika sekta ya
chakula, nishati, vinywaji n.k.
Prof Mbarawa hinted that plans were
underway to purchase two brand-new
aircrafts as part of a strategy to
strengthen the ATC’s fleet in capturing
the local market.
“Last week we had a meeting and
received presentations from officials of
three global airplane manufacturers
and they took us on a number of
options we can consider when we
want to acquire the aircrafts.
“The companies include Canada’s
Bombardier, France’s Airbus as well
as Embraer of Brazil. In the meantime
we have decided to purchase two
planes from Bombardier which will
arrive after two months,” he explained.
Prof Mbarawa noted further that the
national carrier will first establish and
strengthen its footprints in the
domestic market and thereafter
consider regional expansion to
neighouring countries before it
ventures into international flight.chanzo jamii forums.

Kupitia umaarufu na hutuba zake watumika kuingiza mkwanja.

Kupitia umaarufu na hutuba zake watumika kuingiza mkwanja.

Wazalishaji wa filamu moja nchini Mexico
kuhusu wahamiaji wanaojaribu kuingia nchini
Marekani wametoa kipande kidogo cha filamu
hiyo ambacho kinatumia hotuba ya bwana
Donald Trump kupitisha ujumbe wa filamu hiyo
kwamba maneno ni hatari kama risasi.
Sauti iliowekwa katika filamu hiyo ya Kihispania,
Desierto ,inemuonyesha bwana Trump akiitaka
Mexico kusitisha kuwaingiza Marekani walanguzi
wa dawa za kulevya pamoja na walanguzi wa
binaadamu haraka iwezekanavyo.
Kipande hicho cha filamu kinaisha na mlinzi
mmoja akiwawinda wahamiaji jangwani.Filamu
hiyo inaigizwa na Garcia Gael Bernal na
inaelekezwa na Jonas Cuaron ,mwanawe
mwelekezi aliyeshinda tuzo za Oscar Alfonso
Cuaron.chanzo bnc.

Hali ya joto Inayaonzengeza hapa nchini yasababisha ndoa nyingi kutetereka ''nani kasema" ? soma zaid.

Hali ya joto Inayaonzengeza hapa nchini yasababisha ndoa nyingi kutetereka ''nani kasema" ? soma zaid.

Kutokana na hali ya joto iliyopo jijini Dar es
Salaam, Askofu wa Huduma ya Good News for
All, Charles Gadi amefanya maombi kuomba
mvua katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo
mara baada ya kuzungumza na waandishi wa
habari.
Maombi hayo yaliyofanyika kwa nusu saa,
yaliwashirikisha waandishi wa habari na
wachungaji mbalimbali wa huduma hiyo. Katika
maombi hayo yaliyofanyika jana, jijini humo,
Askofu Gadi alisema hali ya hewa imekuwa ya
joto kubwa kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Alisema hali hiyo imesababisha familia na ndoa
kukosa raha na kushindwa kuzaliana kama
ilivyoelezwa katika Biblia kwamba wazae waijaze
dunia.
‘’Wanandoa wanakosa raha, watu wanalala nje
kwa sababu ya joto kali lililokuwepo. Mwaka jana
katika kipindi hiki cha Pasaka kulikuwa na mvua
kubwa zilizosababisha mafuriko lakini ni tofauti
na mwaka huu, hivyo tuombee mvua,’’ alisema.
Alisema inapaswa kuendelea kuomba ili watu
waweze kuishi kwa amani na kwamba endapo
watu hawataomba, inawezekana kusiwe na mvua
za masika kama walivyozoea.
Askofu Gadi aliongeza kuwa ni lazima kuomba ili
kuwe na mvua za kutosha nchi iweze
kujitegemea kwa chakula kwa muda wote wa
utawala wa Rais Dk John Magufuli.
‘’Tuombe ili fedha ambazo Rais Magufuli
angetakiwa kuzitumia kwa ajili ya kuagiza
vyakula, zitumike kwenye kuleta maendeleo
mengine ya muhimu kwa Taifa letu. Pia itasaidia
kuimarika kwa mbuga za wanyama katika
kuendeleza na kuinua sekta ya utalii nchini,’’
alifafanua Askofu Gadi.chanzo time fm.

Tuesday, March 29, 2016
Askari kikosi za zimamoto wanusurika kuchapwa kipigo kutoka kwa wananchi mkoani shinyanga.

Askari kikosi za zimamoto wanusurika kuchapwa kipigo kutoka kwa wananchi mkoani shinyanga.


Askari wa Kikosi cha Zimamoto, Manispaa ya
Shinyanga wamenusurika kipigo kutoka kwa
wananchi wa mtaa wa Banduka, kata ya Ndala
mjini hapa, baada ya kuchelewa kufika kwenye
tukio la nyumba kuungua moto ikiwa na watoto
ndani yake.
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa moto huo
ulianza kuwaka kwenye nyumba ya Azizi
Abdallah, saa 2:00 asubuhi na uliunguza baadhi
ya vitu kwenye nyumba hiyo ambayo wanaishi
wapangaji pekee kwa kile kinachosadikiwa kuwa
ni hitilafu ya umeme ambayo imekuwa ikijitokeza
mara kwa mara.Mmoja wa walioshuhudia,
Onesmo Shija, alisema wapangaji wote walikuwa
wamekwenda makazini na kubaki watoto ambapo
saa 2:00 aliona moshi ukifuka kwenye madirisha
huku watoto wakipiga kelele, ndipo
walipokusanyika na kuanza kuuzima na
kuwanusuru kifo watoto hao.Shija alisema baada
ya wananchi kutoa taarifa mapema kwa kikosi
hicho, walichelewa kufika na walipofika tayari
moto ulikuwa umeshazimwa ndipo wananchi
walipopandwa hasira na kuanza kuokota mawe
na kuwashambulia lakini mwenyekiti wa mtaa
aliwazuia.Mwenyekiti wa mtaa huo, Terege
Nyankangara alisikitishwa na kikosi cha
Zimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio na
kueleza uchelewaji huo ulitaka kuhatarisha
amani. Hata hivyo, Nyankangara aliwaasa
wananchi wake kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi.

Kama unania ya kuwa mkulima ya kilimo cha mapapi soma hii itakusaidia.

Kama unania ya kuwa mkulima ya kilimo cha mapapi soma hii itakusaidia.

SOMA HII INAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA
KUFIKIA MALENGO YAKO
HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE
HESABU..!!
Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza
miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia
mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche
1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza
kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. Tufanye
umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya
shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya
Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi
Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80
unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja).
Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000
unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). Gharama
za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili.
Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua
miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii
milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata
nenda kapande tena papai ekari 20! Kama
kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh.
Milioni mia nane (800,000,000/=). Hapo
nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa
raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini
unatumbua pesa nyingi namna hiyo? Mwambie
Sanga kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza
tena shambani, halafu milioni 500 weka benki.
Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia
mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani
ya miaka mitano. Tuache hayo. Najua utaniuliza,
maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo,
mbegu na mengine. Tafadhali hayo maswali
tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home
work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu).
Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini
kuna nchi nahitaji sana kama vile Comoro na
Madagascar. Kama umeungana na waliokariri
kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua
majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe
laivu!
Kwa haya na mengine mengi usisahau Ku like
page hii.
Sunday at 3:31am · Public · in Tim

Madudu tena yagunduliwa PTA(bandarini).soma zaidi.

Madudu tena yagunduliwa PTA(bandarini).soma zaidi.

Wajumbe wa Kamati hiyo, mbunge wa Mbeya
Vijijini Bw. Oran Njeza pamoja na mwenzake wa
Tunduma wamesema taarifa ya fedha ya
mamlaka hiyo inaonesha uwepo wa mapungufu
makubwa ambayo yasiporekebishwa, mchango
wa sekta ya bandari katika uchumi utaendelea
kudidimia siku hadi siku.
Aidha, mbunge wa Mtwara Mjini Bw. Maftah
Abdallah Nachuma amehoji, dhana ya mradi wa
ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo, wakati
ambapo mamlaka hiyo imekuwa ikihaha kutafuta
pesa kwa ajili ya kuboresha bandari zake
ikiwemo ya Mtwara ambayo inahitaji ukarabati
mkubwa chini ya mradi wa ukanda wa kiuchumi
wa Mtwara.
Kwa upande wake, Mbunge wa Bunda Mjini Bi.
Easter Bulaya amehoji ni kwanini TPA imekuwa
haishughulikii tatizo la bandari bubu zilizozagaa
maeneo mengi ya ukanda wa bahari ya Hindi,
hasa katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam,
huku mizigo inayopitia katika bandari ya Dar es
Salaam ikiwa inapungua.chanzo east africa television.

Tanzania yapata pigo kubwa.soma zaidi.

Tanzania yapata pigo kubwa.soma zaidi.

Waziri wa mambo ya nje mh. Mahiga
amesema serikali imesikitishwa na
kusitishwa kwa mgao wa fedha za MCC
kwani itaathiri sana suala la nishati
hususani umeme vijijini.
Akaongeza kwamba haya ni matokeo ya
nchi kuwa tegemezi.
Chanzo: ITV habari saa mbili usiku, tar

Hivi nchi hii ya tanzania ni masikini kama mtumishi wa umma analipwa mshahara million 40 kwa mwezi?

Hivi nchi hii ya tanzania ni masikini kama mtumishi wa umma analipwa mshahara million 40 kwa mwezi?

Rais wa Tanzania John Magufuli ameahidi
kwamba kuanzia bajeti ijayo kodi katika
mishahara kwa wafanyakazi itapungua kutoka
asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9.
Aidha, pis alisema ataweka kiwango cha kima cha
juu na kwamba wale wote wanaopokea
mishahara ya hadi shilingi milioni 40, itapunguwa
na haitazidi milioni 15
Rais Magufuli aliyasema  hayo hapo jana alipokuwa
akizungumza katika mkutano wa hadhara
Kaskazini Magharibi mwa Tanzania (Wilaya ya
Chato, Mkoa wa Geita) ambapo aliwataka
wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kuondokana
na tabia ya utegemezi wa misaada ya nje.
Magufuli apiga simu kituo cha runinga
"Ni lazima tujisimamie sisi wenyewe. Na
tukijisimamia sisi wenyewe kwa kila mmoja
kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi
afanye kazi kwelikweli. Kama ni mkulima afanye
ukulima kweli kweli, kama ni mfanyabiashara
afanye biashara kweli kweli, kama ni mfugaji
afuge kweli kweli, kama ki mvuvi avue kweli
kweli, Tanzania hii tutavuka," amesema Magufuli.
Awali, Dkt Magufuli, aliagiza kufunguliwa kwa
barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza-Igombe
hadi Kayenze yenye urefu wa kilomita 7.
Barabara hiyo ilifungwa kupisha upanuzi wa
uwanja huo tangu mwaka 2014.
"Nafahamu suala linalowaumiza wananchi la
kufungwa kwa barabara ya Airport-Igombe yenye
urefu wa kilomita 7, sasa naagiza kuanzia sasa
kufunguliwa kwa barabara hiyo ili wananchi
watumie kupita ili kuondoa usumbufu wa
kuzunguka kule maeneo ya Nyakato hadi maeneo
ya TX Kata ya Bugogwa, Kata ya
Sangabuye,”alisema.chanzo(BBC).

Rais magufuli atua kwao chato kwa kishindo na kuongea yafuatayo.sima zaidi.

Rais magufuli atua kwao chato kwa kishindo na kuongea yafuatayo.sima zaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
wananchi wa Chato mara baada ya kumaliza
kuwahutubia katika mkutano wa hadhara jana
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya
sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania
kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na
utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo
huambatana na masharti.
Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo
mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana
na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja
ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi
mahali pake pa kazi.
"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na
tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja
kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi
afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye
ukulima wake kwelikweli, kama ni
mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli,
kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi
avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema
Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli alisema serikali yake
imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu
serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua
watumishi wa umma wanaolisababishia taifa
upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa
hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua
Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo
likomeshwe.
Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote
wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,
Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza
wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa
mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi,
kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa
hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.
Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini
kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya
changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi
waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini
ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana
na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze
kufanya vizuri katika masomo yao.
"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima,
kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi
shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia
kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila
siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni
sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu
Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.
Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli
amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni,
umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa
wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na
kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa
nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi
hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi
za watanzania.
Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye
alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na
kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa
mahakamani.
Pia Rais Magufuli amesema serikali yake
imejiandaa kuboresha maslai ya wafanyakazi kwa
kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi
asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini
amesema kwa wale wanaolipwa mishahara
mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40,
itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha
mshahara usiozidi shilingi milioni 15.

Uchaguzi wa zanzibar waikosesha Tanzania msaada wa trillion 1.

Uchaguzi wa zanzibar waikosesha Tanzania msaada wa trillion 1.

Sheria ya matumizi ya mitandao 'Cyber Crime
Act ya mwaka 2015' pamoja na kurudiwa kwa
uchaguzi wa Zanzibar kumefanya Marekani
kupitia kwa shirika lake la ufadhili kutangaza
kuzuia misaada yake ya kimaendeleo nchini
yenye thamani ya dola 472.8 milioni
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Shirika la
Changamoto za Milenia (MCC) imesema
Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili
kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo.
Mambo yanayolalamikiwa na shirika hilo ni
pamoja na serikali kutochukua hatua za
kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na uguru
wa kujieleza pamoja na utekelezwaji wa sheria
ya uhalifu wa mitandao.
Aidha MCC imesema huwa inazingatia na kutilia
mkazo demokrasia na kujitolea kwa nchi ili
kufanikisha uchaguzi uwe huru na wa haki.
Fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na MCC
zimekuwa zikisaidia miradi mbalimbali ya
kimaendeleo maji, umeme na barabara hasa
maeneo ya vijijini ambapo kwa awamu ya kwanza
serikali ilipokea Dola 698.
Chanzo BBC.

Mfanyakazi mmoja TRA Dar analipwa mishahara  17 kwa mwezi. soma zaid.

Mfanyakazi mmoja TRA Dar analipwa mishahara 17 kwa mwezi. soma zaid.

una baaadhi ya wafanyakazi nchi hii wanapata
mishahara hadi mil. 40 kwa mwezi Hakika
nawaambia mishahara hiyo nitaifuta. Nataka
mshahara wa juu uwe mil.15, Nitaishusha ili
iende kwa hao wadogo wanaoteseka. Kuna watu
wanaishi kama malaika nataka niwashushe
waishi kama shetani. Ambaye hawezi aende
anakotaka. Mwanafunzi unasoma bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne bure halafu
mtihani wa mwisho unapata 0 wewe ni wa
kufungwa(JPM-CHATO) Matatizo ndani ya
serikali ni mengI tu. Nashindwa hadi nianzie wapi
Kuna mfanyakazi mmoja TRA Dar alikuwa
analipwa mishahara 17 kwenye akaunti tofauti
huyu tunampeleka mahakamani.(JPM-CHATO)

Mkurugenzi wa halmashauri ya Itilima mkoan simiyu atumbuliwa jipu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Itilima mkoan simiyu atumbuliwa jipu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony
Mtaka amemsimamisha kazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Itilima, John Aloyce.
Sababu iliyotolewa ya kusimamishwa
kwake ni kushindwa kuisimamia
Halmashauri kama inavyotakiwa.
sijui mamlaka hayo anayatoa wapi. Mtaka
kijana huyu ambaye Mzumbe penyewe
alimaliza kwa kuibia na kuigilizia kwa
watu. Kamwe siwezi kuwa mkazi wa
SIMIYU kuongozwa na RC aliyenusurika
kudisco Mzumbe.chanzo jamii forums.

Kilimanjaro imebaini watumishi hewa 111 soma zaid.

Kilimanjaro imebaini watumishi hewa 111 soma zaid.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said
Meck Sadick amesema wamebaini watumishi
hewa 111 kati ya watumishi 20,964 ambao wapo
katika utumishi wa umma mkoani humo na
kwamba uchunguzi unaendelea kuwabaini
wahusika wa utumishi huo hewa ili waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.chanzo itv.

Watu 10 wamenusurika kufa kwa moto kata ya ndala shinyanga.soma zaid.

Watu 10 wamenusurika kufa kwa moto kata ya ndala shinyanga.soma zaid.

Watu 10 wamenusurika kufa kwa
kuungua moto baada ya nyumba yao iliyoko
katika kata ya Ndala halmashauri ya manispaa
ya Shinyanga mjini kuungua moto unaodhaniwa
kusababishwa na shoti ya umeme leo majira ya
saa tatu asubuhi na kusababisha hasara ya vitu
vya ndani vikiwemo Vitanda,Makochi na Makabati
ya nguo.chanzo itv.

Raisi john magufuli adhihilisha leo huko mwanza kwamba hana utofauti na mwal.nyerere.soma zaid.

Raisi john magufuli adhihilisha leo huko mwanza kwamba hana utofauti na mwal.nyerere.soma zaid.

:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na
Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na
viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia
chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria
uliopo nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza
alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea
nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa
mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni
Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga,
Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James
Bwire,Mkuu wa Mkoa wa MWanza Mhe John
Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg
Anthony Diallo.

Burundi kuiburuza mahakani Rwanda.

Burundi kuiburuza mahakani Rwanda.

In an exclusive interview, Burundi's
foreign affairs minister, Alain Aime
Nyamitwe, said his government plans to
take Rwanda to court for backing the
rebel insurgency in his country.
Burundi's ruling CNDD-FDD party has
accused Rwandan President Paul Kagame
of seeking to "export" genocide to their
country as relations between the two
neighbors deteriorate further.
The head of the CNDD-FDD party Pascal
Nyabenda said in a statement that
Kagame had previously "experimented"
with genocide, referring to the 1994
Rwandan genocide in which around
800,000 people were killed, mostly ethnic
Tutsis.

Monday, March 28, 2016
Makaya awataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais magufuli.

Makaya awataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais magufuli.

Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya
Western Tanganyika Kigoma Sadock Makaya
amewataka watanzania kuunga mkono jitihada za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Dk John Magufuli katika kukabiliana na
uzembe,wizi na matumizi mabaya ya madaraka
yanayosababishia hasara kwa nchi.
Akihubiri katika ibada ya Pasaka kukumbuka
kufufuka kwa yesu kristu katika kijiji cha
Nyumbigwa wilayani Kasulu,Askofu Makaya
amesema uwepo wa wafanyakazi hewa
wanaolipwa na serikali,ufisadi,rushwa
,kutowajibika na matumizi mabaya ya madaraka
miongoni mwa vitu ambavyo Rais Magufuli
anapambana navyo vinakwamisha maendeleo ya
nchi na watu wake, ambapo wamewataka
watanzania kubadilika na kufuata mafundisho ya
mungu.
Aidha katika ibada hiyo kanisa la Anglikana
Nyumbigwa lilitoa msaada wa vyakula na nguo
kwa watu wasiojiweza na wenye ulemavu
mbalimbali,ambapo Askofu Makaya ameeleza nia
ya kanisa hilo Dayosisi ya Western Tanganyika
pamoja na kuhubiri injili ni kusaidia jamii hasa
wahitaji kimwili huku mchungaji Richard Shumbu
wa kanisa hilo akieleza kuwa zaidi ya wahitaji
mia moja wamenufaika na msaada huu.

Sunday, March 27, 2016
Japani yaendelea kubuni njia mpya ya kukuza uchumi baada ya kuanzisha mradi mpya wa treni ya iendayo kasi chini ya bahari.soma zaid.

Japani yaendelea kubuni njia mpya ya kukuza uchumi baada ya kuanzisha mradi mpya wa treni ya iendayo kasi chini ya bahari.soma zaid.

Japan wamefungua mradi wao mpya wa
treni ya kasi zaidi (Bullet train) unaopita
chini ya bahari (Seikan Tunnel) na
kuunganisha sehemu kaskazini ya kisiwa
chake cha Hokkaido. Kwa hivi sasa kisiwa
hicho kimeunganiswa na jiji la Tokyo na
treni ya kasi zaidi. Mradi huo umegharibu
takribani dola za kimarekani bilioni tano
($5 billion).
Kutoka Tokyo hadi Hokkaido kwa treni hii
inachukua dakika 53 ikiwa inachukua
dakika 90 kusafiri kutoka Tokyo hadi mji
wa Shin-Hakodate ulioko Hokkaido
inachukua dakika 90, ukijumla muda wa
ukaguzi wa kiusalama yaweza chukua
zaidi ya masaa 3. kwasasa kuna
ushindani kati ya usafiri huo na ndege.
Seikan Tunnel ni njia kubwa kuliko zote
za chini ya bahari inaurefu wa mile 33.4
(53.8 km).chanzo jamii forums.

Basi super shem mwanza kwenda mbeya limeanguka mlima Ruaha iringa waliofariki ni wanne.

Basi super shem mwanza kwenda mbeya limeanguka mlima Ruaha iringa waliofariki ni wanne.

Kuna basi la Super Shem limeanguka
mlima wa Ruaha Iringa. Inasemekana hali
za abiria ni mbaya.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza
kwenda mbeya.
Waliofariki ni wanne. Wanaume wawili na
wanawake wawili.
Majeruhi ni 38, wako hospitali ya mkoa,
Iringa. Basi hili lilikuwa la kuishia Iringa
ila kuna abiria waliokuwa wakipelekwa
Ipogolo kufaulishwa kwenye gari la Mbeya
na wakati linashusha ule mlima ndio
likafeli breki na kugonga kingo za
barabara na kuanguka.
Majeruhi wengi wamevunjika viungo

Mkuu wa wilaya ya uvinza ampa jukumu nzito mkurugenzi.soma zaid

Mkuu wa wilaya ya uvinza ampa jukumu nzito mkurugenzi.soma zaid

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mrisho
Gambo amemuagiza mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya hiyo kuwachukulia hatua haraka
Maafisa utumishi waliofanya uzembe wa
kushindwa kuwapokea watumishi sitini wa kada
mbalimbali waliopangiwa kufanya kazi wilayani
humo Mwaka jana na kusababisha waondoke
huku wilaya ikiwa na upungufu wa asilimia 77 ya
watumishi.

serikali imeandaa mikakati ya kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.soma zais.

serikali imeandaa mikakati ya kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.soma zais.

Mkurugenzi msaidizi Taasisi ya soko la ajira
Ofisi ya Waziri mkuu kazi, Vijana, Ajira na
wenye ulemavu Ahmed Makbel
Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa
Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel
wakati akizungumza na henura blog.spot.com kuhusu
mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza
kuchukuliwa ili kuhakikisha inawainua vijana
kiuchumi.
Makble amezitaka taasisi zisizo za kiserikali
kushirikiana na Serikali ili waweze kutekeleza
maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na
kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha
na kipato kizuri pamoja na mazingira mazuri ya
kazi.
Mkurugenzi huyo amesema serikali imeanza
kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau
wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia
kwenye vipato vyao vya kila siku sambamba na
kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na
serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.
Makbel ameongeza kuwa wahusika wakuu wa
serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe mazingira
rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa
yakuchangia pato la taifa na serikali kuu
wameanza vikao vya pamoja ili waone
wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa
vijana.

Hivi serikali kukataa kutekeza meno ya tembo ina nia ya kukomesha ujangili nchini? soma zaid.

Hivi serikali kukataa kutekeza meno ya tembo ina nia ya kukomesha ujangili nchini? soma zaid.

mko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe
akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini
Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi
huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta
ya Maliasili nchini.
Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo
wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa
Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya
tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito
duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha
biashara hiyo haramu.
"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo
tayari kuteketeza meno haya, tunaweza
kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo
kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo
mahakamani na nyingine ambazo bado
zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof.
Maghembe.
Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua
hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo
yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na
Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni
njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu
kukomesha biashara hii haramu ya meno ya
tembo.
Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China,
India, Marekani na Ureno.
Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo
sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi
meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya
Kusini, Botswana na Zimbabwe.
Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya
Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba
Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji
mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza
Tanzania pamoja na kusaidia kwenye
mapambano dhidi ya Ujangili.
Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi
ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo
hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza
vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.
Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa
misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani
ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo
wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs)
kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za
Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi
kupitia bandari na viwanja vya ndege.
Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina
ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe
na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark
Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani
imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake
ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika
kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.
Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na
Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof.
maghembe kuwa Serikali ya Marekani
itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya
nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi
imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo
tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili
ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya
ujangili.chanzo east africa television.

Rais john pombe maguful awataka watanzania wote kuwa wamoja.

Rais john pombe maguful awataka watanzania wote kuwa wamoja.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika
wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako
amesali ibada ya Pasaka pamoja na waumini wa
kanisa hilo.
Amesema Mwenyezi Mungu alimtoa mwanaye
wa pekee Yesu Kristo kuja kuikomboa dunia bila
kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi
binadamu tunapaswa kutobaguana, iwe kwa dini
zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na hata
rangi zetu.
Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha
watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu
vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi,
na amebainisha kuwa Tanzania yenye neema
inawezekana endapo kila mtu atazingatia
kufanya kazi.
“Tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka
nje, nchi hii ina neema nyingi. Kwa kweli
tukifanya kazi kwa bidi nchi yetu inapaswa kuwa
inatoa misaada kwa nchi nyingine na sio kuomba
misaada kutoka nchi nyingine” Amesisitiza Dkt.
Magufuli.
Rais Magufuli ambaye amesali kwenye kanisa
hilo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
lakini ikiwa ni mara yake ya nne kusali katika
kanisa hilo hata kabla ya kuwa Rais, amewaomba
watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia
kumuombea yeye ili afanikiwe kutekeleza jukumu
kubwa na zito la kuiongoza nchi.
Pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea
Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli
waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mkuu wa KKKT
Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex
Malasusa amempongeza Rais Magufuli kwa tabia
yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi
viongozi wengine kupenda ibada.
Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa Yesu
Kristo kuwa jambo la kuleta matumaini, na hivyo
amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa, huku
akisema Kanisa linaona matumaini kwa Taifa.

Saturday, March 26, 2016
no image

Tangazo la ajira secta mbalimbli.

EMERGENCY RESPONSE MANAGER
Save the Children Management & Executive,
Deadline: Apr 6, 2016 Chief of Party Creative
Associates International Sales and Marketing,
Deadline: Apr 22, 2016 Physics Teacher The
School of St. Jude Education, Deadline: Apr 15,
2016 Mathematics Teacher The School of St. Jude
Education, Deadline: Apr 15, 2016 Biology Teacher
The School of St. Jude Education, Deadline: Apr
15, 2016 WASH Coordinator OXFAM NGO,
Deadline: Apr 1, 2016 Sub Grants Officer THPS
Administration & Office Management, Deadline: Apr
8, 2016 Internal Compliance Manager THPS
Accounting & Finance, Deadline: Apr 8, 2016
Procurement & Logistics Manager THPS Logistics /
Supply Chain, Deadline: Apr 8, 2016 HALL
JANITOR/ RECEPTIONIST (1 POSITION)
MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL Administration &
Office Management, Deadline: Apr 6, 2016
AUDIOMETRIST (2 POSITIONS) MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL Health, Deadline: Apr 6, 2016
SPEECH THERAPIST (2 POSITIONS) MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL Health, Deadline: Apr 6, 2016
ARTISAN (REFRIGERATION) (1 POSITION)
MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL Health, Deadline:
Apr 6, 2016 DHOBI II (5 POSITIONS) MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL Health, Deadline: Apr 6, 2016
PERSONAL SECRETARY II (1POSITION) MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL Administration & Office
Management, Deadline: Apr 6, 2016
ENVIRONMENTAL HEALTH OFFICER II (1
POSITION) MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL
Health, Deadline: Apr 6, 2016 HEALTH
ATTENDANT II (13 POSITIONS) MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL Health, Deadline: Apr 6, 2016
ACCOUNTS ASSISTANT II (1 POSITION)
MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL Accounting &
Finance, Deadline: Apr 6, 2016 NURSE II (5
POSITIONS) MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL
Health, Deadline: Apr 6, 2016 SUPPLIES
ASSISTANT II (1 POSITION) MUHIMBILI NATIONAL
HOSPITAL Logistics / Supply Chain, Deadline: Apr
6, 2016

Friday, March 25, 2016
Kukithiri kwa ujangili hapa nchini TANAPA sasa kuimarisha kujiimarisha kijeshi.soma zaid.

Kukithiri kwa ujangili hapa nchini TANAPA sasa kuimarisha kujiimarisha kijeshi.soma zaid.

Wahifadhi na Watendaji wa Shirika la Hifadhi ya
Taifa la TANAPA,wameonywa kuwa mafunzo ya
kijeshi yanayoendelea hivi sasa kama hayataenda
sambamba na uadilifu na nidhamu,yatakuwa
hayana tija katika mapambano dhidi ya vitendo
vya ujangili vilivyoshamiri katika hifadhi zote za
taifa nchini,na kutishia kuiuwa sekta ya utalii.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Naibu
Kamishna wa Polisi Paul Chagonja,ameyasema
hayo kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake
na Mshauri wa Mgambo wa Mkoa huo Kanali
Alex Ntazi,wakati wa ufungaji wa mafunzo ya
kijeshi kwa wahifadhi na waekolojia kwenye pori
la akiba la Mlele mkoani humo,na kwamba
TANAPA izingatie kutoa mafunzo hayo kwa
watendaji wake ili kuweza kufikia malengo ya
kulinda hifadhi hizo wakiwa na jeshi usu (para
military
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa
mafunzo hayo yaliyozingatia matumizi bora ya
silaha, ukakamavu na sheria,wamesema mafunzo
yamewatia hali kubwa ya kwenda kupambana na
majangili,ambao hawana nia njema na raslimali
za Nchi hii,ambazo ni kivutio kikubwa cha watalii
na hivyo kuliingizia Taifa mapato makubwa.

Ufisadi Spika wa Bunge job ndugai atajwa Ngorongoro soma zaid.

Ufisadi Spika wa Bunge job ndugai atajwa Ngorongoro soma zaid.

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametajwa katika
kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na
kuisababishia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA), upotevu wa Dola za Marekani 66,890
sawa na Sh. Milioni 133.7
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mhifadhi Mkuu
wa zamani wa NCAA, Benard Murunya ambaye
pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA), Meneja wa Utalii wa NCAA Veronica
Funguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Cosmas
ya Uwakala wa Usafirishaji Salha Issa.
Kesi hiyo iliendelea jana mahakamani hapa kwa
shahidi wa kwanza wa Serikali ambaye ni Kaimu
Mhasibu Mkuu wa NCAA,Sezari Semfukwe
kuhojiwa na Wakili wa utetezi Joseph Boniface
mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi.
Akihojiwa na Wakili Boniface, Shahidi alidai
mbele ya Hakimu ya Patricia Kisinda wa
Mahakama ya wilaya ya Arusha, kwa mujibu wa
nyaraka Murunya aliithinisha malipo ya Dola za
Marekani 66,890 kwa Kampuni ya Uwakala ya
Cosmos ambayo haikufanya kazi husika.
Alidai kuwa malipo hayo yalikuwa kwa ajili ya
Safari ya Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige, Murunya na Msaidizi wa Waziri
Egidius Muyungi ambao hawakutumia tiketi za
Kampuni ya Uwakala ya Cosmos.
Badala yake Aalidai malipo mengine kupitia hundi
namba 310/0379 ya Oktoba 29, Mwaka 2011 na
Tranformer Invoice namba 5609 ya Septemba 7,
Mwaka 2011 yenye Dola za Marekani 66,890
yalilipwa kwa Antelope Tours& Traveling kwa
tiketi ya Waziri Maige, Murunya, Muyungi na
kusafiri kwenda Marekani.
“Baada ya kupata taarifa kuwa huduma
haikutolewa Mhifadhi Mkuu aliandika barua ya
kutaka kujiridhisha kama huduma ilitolewa na
Kampuni ya Cosmas au haikutolewa,” alidai
shahidi huyo wa Serikali ambaye ofisi yake
inahusika na malipo na kumbukumbu zote za
fedha.
Hata hivyo Wakili wa Utetezi Boniface alimpatia
kusoma barua ya Mhifadhi Mkuu kwenda
Kampuni ya Cosmas iliyokuwa ikionyesha malipo
yalivyofanywa kwa kampuni hiyo lakini huduma
haitolewa.
Katika hatua hiyo hiyo Wakili Bonaface alimpatia
tena shahidi barua yenye majibu kutoka Kampuni
ya Cosmas kwenda kwa Mhifadhi Mkuu ambapo
shahidi aliisoma na kueleza kuwa, Kampuni ya
Cosmas ilikiri kupokea fedha lakini haikutoa
huduma.
Alidai kwa mujibu wa barua ya Kampuni ya
Cosmas waliahidi kutoa tiketi nyingine kwa ajili
ya safari Murunya, Naibu Spika Job Ndugai, Peter
Makutiani, Machumu na Kamamba.
“Hawa walisafirishwa na Kampuni ya Uwakala ya
Cosmas na hawana uhusiano na malipo ya
awali,” alidai Shahidi aliyemaliza kutoa ushahidi
wake jana akiongozwa na Wakili wa Hamidu
Sembano anayesaidiana na Wakili Mwandamizi
Rehema Mteta.
Awali mahakamani hapo Wakili wa Utetezi
Boniface aliwasilisha ombi la kujitoa kumtetea
mshitakiwa wa kwanza Murunya kutokana na kile
alichodai kuwapo kwa mawasiliano hafifu baina
yao.chanzo mtanzani.co.tz

Zitto na Hussein Bashe wahojiwa na Takukuru kwa tuhuma za Rusha kwenye kamati yao.soma zaid.

Zitto na Hussein Bashe wahojiwa na Takukuru kwa tuhuma za Rusha kwenye kamati yao.soma zaid.

Muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo
kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa Nzega Mjini,
Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya
Huduma za Jamii, walimuandikia barua Spika wa
Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao
ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
By Julius Mathias, Mwananchi jmathias@
mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Siku tatu baada ya kuibuka kwa
kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuita
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo
kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa Nzega Mjini,
Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya
Huduma za Jamii, walimuandikia barua Spika wa
Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao
ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto alithibitisha kupata wito kutoka makao
makuu ya Takukuru ili kuhojiwa juu ya sakata hilo
na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali
vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote
zinazoelekezwa kwa wanasiasa na watumishi
wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji
na kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nimepata wito huo kupitia Ofisi ya Bunge.
Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi wito wetu
wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito
unaostahili na tutatoa ushirikiano wote kwa
vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa
haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
Alipotafutwa Bashe ili kupata ukweli wa kuitwa
kwake, ingawa hakutimiza ahadi yake, alisema:
“Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza hivi
sasa.”
Mpaka jana, wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji
wanasiasa na watendaji wa mashirika yaliyotajwa
kuhusika kutoa rushwa ili kubadili maoni ya
wajumbe juu ya utendaji wao, wabunge wawili
walithibitika kuitwa na Takukuru.
Tuhuma hizo zimekwenda sambamba na Ndugai
kuwaondoa wenyeviti wa kamati za Ardhi,
Maliasili na Utalii; Nishati na Madini; Uwekezaji
na Mitaji ya Umma huku ile ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC) na Huduma na
Maendeleo ya Jamii lakini akisema ni uhamisho
wa kawaida.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino
Mlowola, bila kuingilia uchunguzi unaoendelea,
alithibitisha kuwaita wabunge hao na watendaji
wa mashirika waliohojiwa.
“Hili ni suala la uchunguzi. Bado linaendelea
hivyo si wakati muafaka kutaja watu waliohojiwa
mpaka sasa ingawa mahojiano yanaendelea. Kazi
ikikamilika utapata taarifa kamili,” alisema
Mlowola.

Thursday, March 24, 2016
Watumish hewa 169 wagundulika mkoani kigoma ni baada ya agizo la Raisi.soma zaidi.

Watumish hewa 169 wagundulika mkoani kigoma ni baada ya agizo la Raisi.soma zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga amewataka
wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote
waliopo katika halmashauri zote kutaja
kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa
mishahara watumishi hewa 169 kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akiongea na waandishi wa habari,
Brigedia Jenerali Emanuel Maganga
alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo
la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa
watumishi katika halmashauri zote ili
kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa
mishahara kinyume na utaratibu za
utumishi.
Alisema katika hao watumishi hewa 169
waliowabainika wapo ambao
walishafukuzwa kazi, wapo ambao
wameshafariki na wengine hawana sifa za
kuwa watumishi wa umma.
Mhe. Maganga alisema kuwa suala la
kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao
hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia
wanyonge hauwezi kuvumilika.
"Hakuna anayeweza kuvumilia wizi wa
waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi
ya watumishi wasiowaaminifu, wale wote
watakaobainika wajiandae kwani hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema
Maganga.
Alisema kuwa fedha walizokuwa wakilipwa
watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara
zinatakiwa kurudi zote, pia wakurugenzi
wawafute watumishi hao hewa kwenye
orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa
hivi katika serekali hii ya awamu ya tano
hakuna kufanya kazi kwa mazoea.
Alizitaja halmashauri zenye watumishi
hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu
watumishi 78,halmashauri ya Kigoma
23,Manispaa ya Kigoma Ujiji
29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza
19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4 na
halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi
hewa.

Serikal ya kongo imeomba umoja wa maifa kuondoa nusu ya askali wake DRC.soma zaid.

Serikal ya kongo imeomba umoja wa maifa kuondoa nusu ya askali wake DRC.soma zaid.


Serikali ya Kongo imeomba Umoja wa mataifa
iondoe nusu ya wanajeshi wake nchini
DRC.Kwenye kikao maalumu kwa ajili ya
kuchunguza hali ya kiusalama nchini humo,waziri
wa mambo ya nje wa kongo ameliambia baraza
la usalama la umoja wa mataifa kwamba,serikali
yake inasubiri kuona ifikapo mwishoni mwa
mwaka huu wanajeshi wapatao elfu kumi wa
umoja wa mataifa wameondoka.Hata hivyo
katibu mkuu wa umoja wa mataifa ameelezea
wasiwasi wake kuhusu hali ya kiusalama ambayo
huenda ikazorota kutokana na hali ya kisiasa
ilioko hivi sasa kabla ya uchaguzi. Je, unafikiri ni
bora kupunguzwa kwa wanajeshi au waongezwe
wanajeshi zaidi?chanzo dw swahil.

BASATA yapiga marufuku Disko toto.soma zaidi.

BASATA yapiga marufuku Disko toto.soma zaidi.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa
na burudani nchini linawakumbusha
wamiliki na waendeshaji wa kumbi za
burudani kufuata sheria, kanuni na
taratibu walizopewa kwenye vibali vyao
vya uendeshaji wa kumbi.
Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na
vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao,
kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi,
kuepuka kelele zinazosumbua kwenye
maeneo maalum hasa makazi ya watu na
kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha
ya watu na mali zao.
Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki
wote wa kumbi za sherehe na burudani
kwamba ni marufuku kukusanya watoto
katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa
‘Disko Toto’ katika msimu huu wa
Sikukuu ya Pasaka ili kuepuka maafa
yanayoweza kujitokeza.
Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za
sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi
wamekuwa wakijisahau na kuendekeza
faida katika biashara zao kiasi cha
kuandaa madisko ya watoto hali mbayo
imekuwa ikisababisha maafa ambayo
yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni
na taratibu.
Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji
wa kumbi kwa msingi huohuo wa
kuendekeza faida pasi na kujali
maelekezo ya vibali vyao wamekuwa
wakijaza watu kupita viwango vya
madaraja waliyopangiwa na BASATA.
BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi
za sherehe na burudani linasisistiza
kwamba halitafumbia macho ukumbi
wowote utakaokiuka maelekezo haya
sambamba na kuruhusu maonesho
machafu yenye kudhalilisha utu wa
binadamu hasa yale yanayoonesha
maungo ya ndani. Hatua kali na za
kisheria zitachukuliwa kwa yeyote
atakayekiuka maagizo haya.
BASATA linawatakia wasanii na wadau
wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye
furaha tele.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA
KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

no image

Halmashauli ya Bariadi mkoani simiyu imewasimamisha watumishi watatu

Serikali wilayani Bariadi Mkoani Simiyu
imewasimamisha kazi Watumishi watatu wa
Halmashauri ya Bariadi kwa tuhuma mbalimbali
ikiwemo ya walimu kuuziwa vitambulisho vya
kazi,fomu ya (OPRAS) na walimu 22
waliosimamishwa na kurudishwa kazini na
kushindwa kulipwa madai yao ya miaka mitatu
kiasi cha milioni 150 baada ya kuagizwa na Tume
ya walimu TSD na kukaidi kufanya hivyo.
Uamuzi wa kuwasimamisha kazi Watumishi hao
umekuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa
kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo
Ponsiano Nyami na waalimu zaidi ya elfu moja
wa Wilaya ya Bariadi kilichofanyika katika Ukumbi
wa Bariadi Motel ambapo walipomueleza mkuu
huyo namna wanavyonyanyasika na watumishi
hao kiasi cha kukata tamaa,ya kufundisha
kutokana na madai yao yakiwemo malimbikizo ya
mishahara.
Mara baada ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya
akaitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi
na Usalama,ambapo akatoa kauli ya Serikali ya
kuwasiamamisha Watumishi hao mbele ya
waandishi wa habari.
Sambamba na kuwasimamisha Watumishi hao pia
ameviagiza Vyombo Dola ikiwemo Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU
kuhakikisha wanachunguza tuhuma zote
zinazowakabili,huku akimuagiza Mkuu wa Polisi
wa Wilaya kuwakamata na kuwafikisha
ahakamani wale wenye maduka ya vifaa vya
shule ambao wamekuwa wakiuza za fomu za
OPRAS ambazo ni za serikali katika maduka yao

Tanzania na Saud Arabia wasaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara.soma zaid.

Tanzania na Saud Arabia wasaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara.soma zaid.

:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili
wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu
Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia hapo jana
katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji,
Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa
Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga
(kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa
na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.

Wilaya ya maswa mkoani shinyanga imepoteza milion500 kwa kumlipa mkandarasi hewa.

Wilaya ya maswa mkoani shinyanga imepoteza milion500 kwa kumlipa mkandarasi hewa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa
Mkoani Simiyu,imebaini kuwepo kwa matumizi
hewa ya zaidi ya shilingi Milioni 500,yaliyofanywa
na Meneja wa Mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira Wilayani humo Mhandisi Jeremiah
Lema kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Pett
Cooperation Ltd,anayejenga mradi wa chujio la
maji wa Zanzui bila kibali cha Bodi ya maji
Wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Maswa Rosemary
Kirigini,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
amesema kuwa meneja huyo pia anadaiwa
kuidanganya kamati hiyo ya ulinzi na usalama
kuhusu ununuzi wa Krasha iliyodaiwa kuagizwa
toka nchini china
Mkurugenzi wa kampuni ya Petty Coopertion Ltd
inayotekeleza ujenzi wa mradi huo wa chujio la
maji wa Zanzui kwa ushirikiano na kampuni ya
Josam and Company Ltd Tryphon Elias,akatoa
ahadi ya kukamilisha mradi huo tarehe 30 mwezi
Mei.
Lugha gongana kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya
maji wilayani Maswa Aloys Kimisha na Meneja
wake Mhandisi Jeremiah Lema kuhusu wananchi
kunyweshwa maji ambayo hayajatiwa
dawa,ikaibuka mbele ya Mkuu mpya wa Mkoa wa
Simiyu Antony Mtakaje, mkuu huyo wa Mkoa wa
Simiyu Antony Mtaka yuko tayari kuwajibika
iwapo wananchi wa Maswa watakunywa maji
yasiyotibiwa na kuugua magonjwa ya mlipuko
kikiwemo kipindupindu.chanzo itv tanzania.

Wafanyakazi 100 wa mgodi wa tanzanite waandamana kupinga kufukuzwa bila kulipwa mishahara yao.

Wafanyakazi 100 wa mgodi wa tanzanite waandamana kupinga kufukuzwa bila kulipwa mishahara yao.

Zaidi ya wafanyakazi mia moja wa mgodi wa
uchimbaji wa madini ya Tanzanite ya G and M
uliyopo katika Mji mdogo wa Mererani wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara waliandamana hapo jana
kupinga hatua ya kampuni hiyo kuwaachisha kazi
bila kuwapa stahiki zao kwa kazi waliofanya kwa
zaidi ya miaka mitatu huku wakilazimishwa
kusaini mikataba mipya.
Wakizungumza kwa jazba wafanyakazi 
hao wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka
mitatu na sasa wameachishwa ghafla kwani
walifika kwenye lango kuu la kuingia mgodini
wamekuta pamefungwa na kutakiwa wasiingie
ndani,wameiomba serikali iwasaidie kwakuwa
tayari wamiliki wameajiri wafanyakazi wengine na
wao kulazimishwa kusaini mikataba mipya.
Mwenyekiti wa wafanyakazi hao Adam Mosha
amesema hatua iliyo chukuliwa na uongozi wa
mgodi huo siyo ya kibinadamu na kamwe
hawatakubali kuacha haki yao.
ITV ilimtafuta Meneja wa Mgodi huo Elisante
Forcet ambaye amedai kuwa kampuni hiyo
haijawahi kuajiri wafanyakazi lakini huwa
wanawachukua kama vibarua na hivyo hakuna
mwenye haki ya kudai na kwa sasa kampuni
haina pesa za kuendelea kuwa na wafanyakazi
wengi kiasi hicho.chanzo itv.

Wakala wa pembejeo wilaya ya ulanga mkoani morogoro kutiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa.soma zaid.

Wakala wa pembejeo wilaya ya ulanga mkoani morogoro kutiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa.soma zaid.

Serikali wilayani Ulanga mkoani Morogoro
imeamuru kutiwa mbaroni kwa wakala wa
usambazaji wa Pembejeo,Novatus Naningwa na
wasaidizi wake pamoja na Afisa mtendaji wa
kata ya Kichangani na wa kijiji cha Kichangani
wilayani humo,wakituhumiwa kuwarubuni
wananchi kuchukua fedha badala ya vocha za
Pembejeo.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Christina Mndeme
amekiri kufikia uamuzi huo,baada ya wakala
huyo,wasaidizi wake na kiongozi wa kata ya
Kichangani na kijiji cha Kichangani kubainika
walikuwa wakiwarubuni wananchi kuchukua kiasi
cha shilingi 5000 ili wasaini wamepokea vocha
hizo za serikali ambazo nusu ya Gharama yake
imekuwa ikilipiwa na Serikali.
Amesema wakala huyo alipewa dhamana ya
kusambaza vocha hizo za Pembejeo katika kata
tatu za Kichangani,Lupiro na Milola,lakini yeye na
wasaidizi wake,Kuchungi Mussa, Ponsiasi
Chanja,Christopher Ponela na Rashid
Msasa,walishirikiana na mtendaji wa kata na wa
kijiji na kuwarubuni wananchi Wachukue
vocha,badala yake walisaini vocha Hizo na
kupewa shilingi 5,000 kwa kila mmoja.
Hata hivyo Amesema baada ya Uongozi wa
Wilaya kupata taarifa kutoka kwa raia Wema na
Diwani walimuandikia wakala huyo barua ya
kumsimamisha kuendelea na Huduma ingawa
aliendelea na zoezi hilo hivyo kuamuru
watuhumiwa hao watiwe mbaroni ili kufikishwa
mahakamani,huku Mtendaji wa kata na mtendaji
wa kijiji cha Kichangani wakikimbia na
wanaendelea kutafutwa.chanzo itv.

Tumbili 61 wakamatwa uwanja ndege KIA.soma zaid

Tumbili 61 wakamatwa uwanja ndege KIA.soma zaid


Raia wa Uholanzi wakamatwa KIA na tumbili 61
Raia wawili wa Uholanzi wamekamatwa katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
kwa kutaka kusafirisha jumla ya tumbili hai 61
Walikuwa wanataka kuwasafirisha kuelekea
nchini Albania.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwakamata raia
hao

Wabunge wanaotuhumiwa kupokea Rushwa sasa kuchunguzwa na Takukuru.soma zaid.

Wabunge wanaotuhumiwa kupokea Rushwa sasa kuchunguzwa na Takukuru.soma zaid.

Wabunge wamevitaka vyombo vya kuichunguzi
kuhakikisha vinazifanyia kazi tuhuma za rushwa
zinazowakabili baadhi ya wabunge kwani ni
dhahiri zinashusha hadhi ya Bunge na kuwafanya
wananchi kutokuwa na imani na wawakilishi wao.
Katika mahojiano maalum na ITV kwa nyakati
tofauti jijini Dar es Salaam wabunge hao kutoka
majimbo ya Mtera,Nyamagana,Magomeni
Visiwani Zanzibar wamesema uwepo wa tuhuma
hizo kwa wabunge waliopewa dhamana kubwa ni
fedheha kwa Bunge, huku wakitaka hatua stahiki
kuchukuliwa kama tuhuma hizo zitabainika.
Maafisa wa Bunge wanasema moja ya hatua za
awali waliokwisha kuzichukua ni pamoja na
kuwavua uwenyeviti wa kamati za kudumu za
bunge wanaotajwa katika tuhuma hizo pamoja na
kuwahamisha baadhi ya wabunge kutoka kamati
moja hadi nyingine,nakuahidi hatua nyingine zaidi
zitafuata.
Miongoni mwa hatua zilizokwisha kuchukuliwa na
Spika wa Bunge chini ya kanuni ya 116(3) cha
kanuni za kudumu za Bunge,ni pamoja na
kufanya mabadiliko katika kamati 5 za Bunge
pamoja na kufanya mabadiliko ya wajumbe katika
kamati hizo.

Licha ya Rais magufuli kuagiza mashine ya EFD's kutolewa bura kwa wafanya biashara hapa nchini mkuu wa kitengo cha machine ya lielekitroniki amemuweka ngumu.soma zaid.

Licha ya Rais magufuli kuagiza mashine ya EFD's kutolewa bura kwa wafanya biashara hapa nchini mkuu wa kitengo cha machine ya lielekitroniki amemuweka ngumu.soma zaid.


Wakati wafanyabiashara wakisubiri kupewa bure
mashine za kieletroniki (EFD’s) kama Rais John
Magufuli, alivyosema, Mamlaka ya Mapato (TRA)
imesema kauli ya Rais ilikuwa ni mtazamo wake
na siyo agizo kama linavyopotoshwa na baadhi
ya wafanyabiashara.Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Mashine za Kieletroniki na Kodi
Mkoa wa Kodi Temeke, Kennedy Sawaya,
aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Chemba ya Wafanyabiashara,
Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA).
Alisema mashine za bure zitatolewa kwa baadhi
ya sekta na hazitawahusu wafanyabiashara
wasajiliwa wa Vat na wale wanaotegemea
kusajiliwa humo.Sawaya alitoa maelezo hayo
baada ya mmoja wa washiriki wa mkutano huo
kutaka kujua kwa nini TRA inachelewa kutoa
mashine hizo ambazo Rais Magufuli aliagiza
zigawiwe bure kwa wafanyabiashara nchini.
Akijibu swali hilo alisema: “Ulikuwa ni mtizamo
wa Rais kama TRA inaweza kufanya hivyo,
hakuna bajeti iliyoelekezwa kuzinunua mashine
hizi hata zikitolewa bure ni kwa baadhi ya sekta,”
alisema.

Back To Top