Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Sunday, February 28, 2016
Rais magufuli amewasili Arusha kwa mkutano unatakaofanyika 2/03/2016 wa Marais wa Afrika mashariki.

Rais magufuli amewasili Arusha kwa mkutano unatakaofanyika 2/03/2016 wa Marais wa Afrika mashariki.

Rais Magufuli akiwasili uwanja wa Ndege
wa KIA kwa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa
Nchi za Afrika Mashariki unaotarajiwa
kufanyika Machi 2, 2016.
Pichani, Rais Magufuli akisalimiana na
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mhe.
Joshua Nassari(CHADEMA) aliyekuwa
mmoja wa viongozi na wananchi
waliojitokeza kwa wingi kumpokea
alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza
Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
utofanyika jijini Arusha.chanzo jamii forum.

Saturday, February 27, 2016
Au wapeleka wanajeshi 100 kurinda amani burundi.soma zaid.

Au wapeleka wanajeshi 100 kurinda amani burundi.soma zaid.

Umoja wa Afrika umetangaza kwamba
utawapeleka waangalizi 100 wa haki za
kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100
wa kijeshi nchini Burundi.
Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre
Nkurunziza ameunga mkono mpango huo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza
ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika
ziara ya siku mbili wiki hii.
Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi
wawili wa upinzani ambao wamesalia nchini
humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi
Aprili baada ya Nkurunziza kutangaza kuwa
atawania muhula wa tatu.
Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais
Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo
hivi karibuni.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.chanzo bbc swahili.

Friday, February 26, 2016
Majambazi wavamia benk la Access tawi la mbagala rangi tatu.

Majambazi wavamia benk la Access tawi la mbagala rangi tatu.

Benki ya Access Tawi la Mbagala Rangi
Tatu kuna tukio la Ujambazi limetokea
muda huu!
Chanzo: CloudsFm
============
Kwa mujibu wa polisi kanda maalum,
majambazi watatu wameuawa baada ya
kupambana na polisi na kuzidiwa nguvu.

Nyota wa filamu ya rocky tony Burton afariki dunia.soma zaid.

Nyota wa filamu ya rocky tony Burton afariki dunia.soma zaid.

atsApp
News Sport Weather Radio
Masharti ya matumizi Kuhusu BBC
Sera ya Faragha Cookies
Accessibility Help Parental Guidance
Wasiliana na BBC Jitangaze na BBC
Chaguo
Viunganishi
Uongozaji BBC
Swahili navigation
Yaliyomo
Mwigizaji wa filamu ya Rocky Tony Burton
afariki
26 Februari 2016
Mshirikishe mwenzako
T.chanzo bbc swahili.

AU waamua kukamilisha mgogoro wa amani Burundi.

AU waamua kukamilisha mgogoro wa amani Burundi.


Viongozi wa mataifa matano ya Afrika
wanaokwamua mgogoro wa kisiasa nchini
Burundi wanakamilisha mazungumzo yao katika
mji mkuu wa taifa hilo Bujumbura.
Usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa,viongozi hao
walikutana na wanasiasa,wanaharakati na
makundi ya kidini.
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge
amesema kuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma
aliwaambia wanasiasa hao kwamba lengo lao kuu
ni kuunga mkono juhudi za kuleta amani nchini
humo.
Bwana Zuma na rais Pierre Nkurunziza
wanatarajiwa kutoa taarifa mwishoni mwa ziara
hiyo.chanzo bbc swahili.

Mawazir 4 na naibu wazir mmoja wapewa masaa 12 kujaza na kurudisha form za maadili.

Mawazir 4 na naibu wazir mmoja wapewa masaa 12 kujaza na kurudisha form za maadili.

Rais John Pombe Magufuli ametoa muda
mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na
Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu
kwa Sekretarieti ya maadili kwa ajili ya
kuanisha mali na madeni wanayodaiwa
ambapo wamepewa muda mpaka saa 12
wawe wamesharejesha fomu hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja
majina mawaziri hao kuwa ni
Agustine Mahiga
Charles Kitwanga,
January Makamba,
Joyce Ndali Chako na
Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.
=======
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa leo Jumanne
Februari 26, 2016 ameongea na
waandishi wa habari kuhusu kadhia ya
baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu
ya tano kushindwa kuresha fomu za hati
ya mali ya wanazomiliki. Kwanza alielezea
sekretarieti ya maadili na nini wajibu wake
ikiwemo kufatilia maadali ya viongozi wa
umma na sheria inayowataka viongozi
husika kutoa tamko la mali ndani ya siku
thelathini tangu uteuzi wao.
Majawaliwa: Viongozi wanaoshindwa
kutoa tamko katika kipindi kilichowekwa
kwa mujibu wa sheria wanawajibika kutoa
maelezo ya sababu za msingi za
kushindwa kwao kuwasilisha fomu hizo
za tamko la rasilimali na madeni
waliyonayo.
Endapo maelezo hayo hayatakuwa na
sababu za msingi, hatua zaidi za kisheria
huwa zinachukuliwa. Aidha viongozi wa
umma wanawajibika kusaini hati za
maadili, ahadi ya uadilifu kwa viongozi
wote wa umma. Zoezi hili lilianza mwaka
2015 na ni endelevu na lilikuwa na lengo
la commitment ya kiongozi juu ya uadilifu
wake wakati wote anapokuwa kiongozi wa
umma na tayari watumishi wengi wa
umma wanaendelea kuzijaza fomu hizo na
ndio msingi wa uwajibikaji katika sekta ya
umma.
Kwa misingi hiyo, mawaziri bado
wanaendelea na zoezi hilo lakini pia mtu
toka alipoteuliwa. Fomu hizo
walishakabidhiwa na wanawajibika
kurudisha tume.
Jana nilikabidhiwa majina ya mawaziri na
manaibu mawaziri ambao hawakuweza
kurudisha fomu zote mbili au fomu moja.
Na alikuwa analikuwa anatakiwa pia watoe
tamko la rasilimali walizonazo na madeni
waliyonayo na fomu hizo walitakiwa
kurejesha kwa kamishna.
Mhashimiwa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania ameelekeza
kwamba waziri na manaibu waziri wote
ambao hawajajaza tamko la rasilimali na
madeni, ifikapo leo Ijumaa saa kumi na
mbili jioni wawe wameshajaza na
kurejesha fomu hizo ofisi ya tume ya
maadili hapa Dar es Salaam.
Kwa waziri yeyote ambae atashindwa
kutekeleza agizo hilo atakua amejiondoa
mwenyewe kwa majukumu aliyonayo ya
uwaziri au unaibu waziri. Na mheshimiwa
Rais ameelekeza lazima wasomwe ili
popote walipo warudi na watekeleze hivyo
na ofisi yangu itasimamia kwa ukaribu
kuona kwamba fomu hizo zinapatikana
ifikapo saa 12.
Nao ni wafuatao, kundi la mawaziri
1. Charles Kitwanga(Waziri wa
mambo ya ndani, yeye hajarejesha
fomu zote mbili)
2. January Makmba (Hajarejesha
fomu zote mbili)
3. Dr Augustine Mahiga (Waziri wa
mambo ya nje, Fomu moja ya
maadili)
4. Prof Ndalichako (Fomu moja ya
tamko)
Manaibu
1. Luhaga Mpina (Mazingira na
muungano, hajajaza fomu zote
mbili)
===================
Update
Agizo la Rais Magufuli laanza
kutekelezwa, Waziri Mahiga arudisha
Fomu wengine wang'aka
Baada ya Waziri Mkuu kutaja majina ya
mawaziri wanne na Naibu waziri mmoja
ambao hawajarudhisha fomu za
Sekretariati ya maadili ya umma na
kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo
mpaka saa kumi na mbili jioni ijumaa ya
leo mpaka sasa ni waziri mmoja aliyetii
agizo hilo.
Aliyerudisha fomu hizo ni waziri wa
mambo ya nje,ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe.
Balozi dkt. Augustine Mahiga ambapo
amekiri kuwa ni kweli alikuwa hajarudisha
fomu hizo kutokana na majukumu ya kazi
yaliyokuwa yamembana.
ITV pia imefanikiwa kuongea na waziri wa
mambo ya ndani Charles Kitwanga
ambaye naye ametajwa kutorudisha fomu
hizo ambapo ameshangaa jina lake
likitajwa wakati ameshazirudisha na kwa
sasa ameelekea ofisi za Sektretariati ya
maadili kuwasilisha malalamiko yake.
Naibu waziri wa ofisi ya makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
ambapo amesema kuwa atawahisha
kurudisha fomu hizo kabla ya saa kumi
na mbili jioni.

Mawaziri 4 na naibu waziri mmoja wapewa masaa 12 wawe amejaza na kurudisha form za maadiri.soma zaid.

Mawaziri 4 na naibu waziri mmoja wapewa masaa 12 wawe amejaza na kurudisha form za maadiri.soma zaid.

Rais John Pombe Magufuli ametoa
muda mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na
Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu kwa
Sekrtariati ya maadili kwa ajili ya kuanisha mali
na madeni wanayodaiwa ambapo wamepewa
muda mpaka saa 12 wawe wamesharejesha fomu
hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja majina
mawaziri hao kuwa ni Agustine Mahiga( # Pichani)
, Charles Kitwanga,January Makamba,Joyce Ndali
Chako na Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.

Habari ya hivi bunde ccm yakimbilia mahakani kupinga uchaguzi wa meya wa jiji la Dar hapo kesho.soma zaid

Habari ya hivi bunde ccm yakimbilia mahakani kupinga uchaguzi wa meya wa jiji la Dar hapo kesho.soma zaid

CCM wakimbilia mahakamani kuzuia uchaguzi wa
Meya kesho
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba CCM
wako mahakamani muda huu wakitafuta hati ya
kimahakama kuzuia uchaguzi wa kumpata Meya
wa Jiji la Dar es salaam usifanyike kama
ilivyokuwa imetangazwa hapo awali, na kama
barua za mialiko kwa wajumbe wa kikao hivyo
zinavyoelekeza.
Aidha sababu kubwa inayotajwa CCM kukimbilia
mahamakani kutafuta zuio la uchaguzi wa Meya
wa Jiji inatajwa kuwa ni wao (CCM) kuendelea
kutafuta mbinu ya kushinda uchaguzi huo bila
kujali idadi ya wajumbe wao ni ndogo kuliko ya
Ukawa.
Awali moja ya mbinu tegemeo waliyojua itawapa
ushindi ni kuongeza wabunge wa viti maalum
kutoka nchi jirani ya Zanzibar na wengine kutoka
mikoa ya Tanzania bara, ambao kwa bahati
mbaya baada ya kufuatilia hao wanaotoka mikoa
mingine ilibainika michakato yao ya kusaka
ubunge wa viti maalum ulianzia huko mikoani
kinyume na ukweli kwamba makazi yao yako Dar
es salaam. Na kwa maana hiyo wakaonekana si
wajumbe halali kujumuishwa kwenye uchaguzi
huu.
Kwa wale wabunge wa viti maalum kutoka nchi
jirani ya Zanzibar wao ilibainika kwamba
hawatakiwi kujihusisha na uchaguzi huu wa
kumpata Meya, kwa kuwa wajumbe wote
wataingia kama madiwani na hivyo wao
hawaruhusiwi kwa kuwa suala la madiwani liko
chini ya TAMISEMI, Na suala hilo si la Muungano.
Kwa kuwa mbinu hiyo chafu iliyotaka kutumiwa
na CCM imekwama ,Imekwama, na kwa kuwa
uchaguzi ni kesho tu kama ilivyotangazwa, basi
wameona njia pekee ni kukimbilia mahakamani
tena, kuzuia uchaguzi huo wa kesho usifanyike.
Kwa maoni yangu. Nawaomba CCM wakubali tu
kwamba jiji liko chini ya Ukawa, ni watanzania
hawa, tofauti ni itikadi tu, na kwa kuwa Tanzania
iliridhia kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi
sioni sababu ya msingi kuendelea kulazimisha
wakati mchakato huu ulianzia kwa wananchi
kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa kuwachagua
madiwani wengi wa ukawa.
Ni bora waachane na figisufigisu hizi za
kulazimisha kuongoza jiji. ...sidhani kama mbinu
hii ya kuendelea kuzuia uchaguzi kwa njia ya
mahakama utawasaidia. ..labda kama wanahitaji
kwenda hatua nyingine mbaya zaidi ya kumwaga
damu ya watanzania kwa kutaka kuongoza jiji,
labda kama wanajipanga kupata umeya kwa
umafia, kwa vurugu na support ya vyombo vya
dola. ...Lakini uchaguzi wa haki na huru, kwa
uchaguzi wa kidemokrasia sioni CCM watashinda
vipi uchaguzi na meya wa Jiji kwa kuwa
uchaguzi ni namba na namba haziongopi.
..Ukawa wana wajumbe takribani 11 zaidi ya
wajumbe wa ccm.
hii ya ccm kukimbilia mahakamani, nawashauri
waachane na mpango huo waache demokrasia
itamalaki.chanzo Dodluck peter mtema .breaking new tz.

Morogoro sasa kupimwa na kutolewa hati za kimila.soma zaid.

Morogoro sasa kupimwa na kutolewa hati za kimila.soma zaid.

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Wiliam Lukuvi ameagiza kupimwa na kutolewa
kwa hati za kimila kwa wananchi wa wilaya ya
Mvomero sambamba na kuheshimiwa na
kutambuliwa kwa hati hizo na taasisi mbalimbali
za kifedha ikiwemo mabenki.
Waziri Lukuvi amesema hayo baada ya kufika
wilayani Kilosa na kupokea taarifa ya usuluhishi
wa migogoro ya ardhi katika kijiji cha Mabwegere
wilayani Kilosa,kazi ambayo awali alimwagiza
aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro
Steven Mashishanga kuifanya,ambapo pia
ametembelea wilaya ya Mvomero akiwa na timu
ya wataalamu wa kuhakiki mipaka ya vijiji sita
vya wilaya hiyo na kupima,ambapo amekuwa ni
waziri wa tatu kutembelea wilaya hiyo ndani ya
kipindi kisichozidi wiki moja,na ametumia fursa
hiyo kuzungumza na baadhi ya makundi ya
wakulima na wafugaji pamoja na viongozi,na
kutoa hati milki za kimila zaidi ya elfu
saba,akitaka zitambuliwe.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Rajab Rutengwe
amevitaka vyombo vya usalama kutogeuka
sababu ya migogoro ya ardhi katika wilaya za
mkoa huo,sambamba na kuahidi kubadili viongozi
wa jeshi la polisi hususani wilayani Mvomero ili
kubadili utendaji,ambapo mkuu wa wilaya ya
Mvomero Elizabety Mkwasa akabainisha wapo
baadhi ya wafugaji wanaoshiriki katika kukuza
migogoro wilayani humo ikiwemo kwa kuruhusu
uingizaji wa mifugo kiholela na kutumia watoto
kuchunga bila tahadhari.chanzo itv tz.

Wednesday, February 24, 2016
Naibu waziri wa ardh asitisha mkataba na mwenyekit wabaraza la ardhi nyumba na makazi geita.

Naibu waziri wa ardh asitisha mkataba na mwenyekit wabaraza la ardhi nyumba na makazi geita.

Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya
makazi,Angeline Mabula amesitisha mkataba wa
kazi wa Emmanuel Mogasa ambaye Mwenyekiti
wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya chato
iliyoko mkoani Geita mkoa ili apishe uchunguzi
wa tuhuma zinazochunguzwa juu yake za
kujihusisha na vitendo vya rushwa katika kutoa
maamuzi ya mashauri yanayofikishwa katika
baraza hilo.
Naibu waziri huyo ametoa maamuzi hayo baada
ya kupokea taarifa toka kwa mwenyeti huyo
ambayo ilikuwa inaelezea mwenendo mzima wa
utendaji wa kazi wa baraza hilo.
Amesema amesitisha mkataba wa kazi wa
Mogasa na hivyo atakuwa nje ya ofisi hadi
uchunguzi wa tuhuma zinazomhusu
utakapokamilika na pia ametoa onyo kwa
watendaji idara ya ardhi wa halmashauri ya
wilaya ya chato na kutaka wampe taarifa juu ya
matumizi ya shilingi zaidi milioni 32 zilizotolewa
na wizara kama mkopo kwa ajili ya upimaji wa
viwanja wilayani humo ambao hadi sasa
haurejeshwa wizarani kulingana na makubalino.
Katika hatua nyingine naibu waziri huyo
ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa
kuhakikisha zinatenga viwanja vitakaloliwezesha
shirika la nyumba la taifa kujenga bora kwa
gharama nafuu ili nyumba zinazijengwa
zinazojengwa na ziwe na unafuu kodi, ametoa
agizo hilo baada ya kukagua nyumba zilizojengwa
na shirika hilo wilayani chato na muleba mkoani
kagera.
Naye,Deogratias Batakanwa ambaye ni meneja
wa shirika la nyumba mkoani Kagera na wilaya
ya chato ambayo zamani ilikuwa mkoani humo
kabla ya kuundwa kwa mkoa wa Geita,ameelezea
idadi ya nyumba ambazo shirika hilo limezijenga
mkoani Kagera na wilaya changamoto inayokabili
ujenzi wa nyumba hizo

Waziri wa awamu ya kikwete atajwa kuwa fisadi ngorongoro.soma zaidi

Waziri wa awamu ya kikwete atajwa kuwa fisadi ngorongoro.soma zaidi

Ezekiel Maige Atajwa Ufisadi Ngorongoro
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika
serikali ya awamu ya nne, Ezekiel Maige, jana
alitajwa katika kesi inayomkabili aliyekuwa
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro, Bernard Murunya* ambaye
ameshitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi.
Katika kesi hiyo, Maige anadaiwa kulipiwa nauli
ya safari ya nje na mamlaka hiyo kwa idhini ya
Murunya, ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika
Mashariki.*
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Sezari
Semfukwe, alidai kuwa Murunya na aliyekuwa
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mamlaka
hiyo, Shad Kiambile, waliidhinisha malipo ya dola
66,890. Alidai kuwa fedha hizo zilikuwa kwa ajili
ya safari ya Maige na msaidizi wake aliyetajwa
kwa jina la E. Muyungi na Murunya mwenyewe.
Semfukwe, ambaye ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa
mamlaka hiyo, alidai kuwa Murunya na Kiambile,
ndio walioidhinisha madokezo kwa ajili ya malipo
hayo.*
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Hamidu
Sembano, akisaidiana na Rehema Mteta, mbele
ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha,
Patricia Kisinda, Semfukwe alidai kuwa utaratibu
wa maombi ya safari, unatokana na maelekezo
ya mkuu wa idara na kujaza fomu inayoonyesha
anakwenda wapi na kwa muda gani.
Sambamba na hilo, alidai kuwa aina zingine za
safari zinahusisha watu wa nje ambao, si
waajiriwa wa NCAA kwa dokezo la mkuu wa
idara au shirika.
Alidai kuwa alitoa hundi ya malipo namba
309/0238 ya Septemba 9/2011, ambayo ilikuwa
na dokezo la safari kutoka kwa Murunya kwenda
kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha. Pia *alitoa
hundi ya malipo nyingine iliyokuwa ikionyesha
imelipwa dola zaMarekani *66,890 kwa kampuni
ya Wakala wa Usafirishaji ya Cosmas.
Aliendelea kudai kuwa hundi za malipo namba
310/0379 ya Oktoba 29, 2011 na ankara namba
5609 ya Septemba 7, *2011 zililipwa kwa
Antelope Tours & Traveling kwa ajili ya tiketi za
Murunya, Muyungi na Maige kwa malipo ya dola
za Marekani 66,890 (zaidi ya Sh. milioni 133).
Shahidi hiyo alidai kuwa kumbukumbu ya kitabu
cha malipo ya hundi inaonyesha hundi namba
002758 na 002755 za Septemba 9, *2011
zililipwa kwa kampuni ya Cosmas Travelling
Agent na zilitiwa saini na Kiambile na Murunya.
Hata hivyo, wakati shahidi huyo akitoa vielelezo
hivyo mahakamani hapo ili vitumike kama
ushahidi, malumbano ya kisheria yaliibuka baina
ya mawakili wa pande zote.
Malumbano hayo yaliibuka baada ya upande wa
washtakiwa, ukiongozwa na wakili Amani
Mirambo, kutaka kujua ni vielelezo vingapi au vya
aina gani ambavyo upande wa mashtaka
unavileta.
Hatua hiyo ilisababisha malumbano ya kisheria
hivyo kumfanya hakimu kuahirisha kesi kwa
dakika 10. Baada ya muda huo, alirejea
mahakamani baada ya dakika hizo na kuwahoji.
Baada ya kuhoji pande zote mbili, kutokana na
malumbano ya kisheria, Hakimu alikatizwa na
Wakili wa Serikali Hamidu Simbano,
aliyemwomba *kuahirisha kesi hiyo na kutaja
tarehe nyingine ya *washtakiwa kusomewa
maelezo yao ya awali.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
Rehema Mteta, aliwasomea maelezo ya awali juu
ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka
yaliyosababisha mamlaka hiyo kupoteza dola
66,890 (Sh. 133,780,000).
Mteta aliwataja washitakiwa, mbali na Murunya
na Kiambile, kuwa ni Meneja Utalii wa mamlaka
hiyo, Veronica Funguo na Salha Issa ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Cosmas Travelling
Agent.chanzo godluck peter breaking newz tz.

Tuesday, February 23, 2016
Chama cha CUF kimeitaka tume ya uchaguzi ZEC kutotumia jina alama au picha ya mgombea kutoka cuf.

Chama cha CUF kimeitaka tume ya uchaguzi ZEC kutotumia jina alama au picha ya mgombea kutoka cuf.


Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuhakikisha haitumii
jina, alama wala picha ya mgombea yeyote wa
chama hicho katika karatasi za kura za uchaguzi
mkuu wa marudio utakaofanyika March 20,
mwaka huu visiwani humo.Akizungumza na
waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma
wa chama hicho, Hamad Masoud, alidai CUF
inatambua kwamba Mwenyekiti wa ZEC, Jecha
Salim Jecha, anatekeleza maagizo ya chama
chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema CUF inawataka wananchi wote wa
Zanzibar, Tanzania na jumuiya ya kimataifa
kutambua kwamba Jecha ametoa taarifa ya
uongo ili kuendeleza upotoshaji alioanzisha kwa
tamko lake la kufuta uchaguzi wa Oktoba 25,
mwaka jana na kuamuru kurudiwa uchaguzi
huo.Alisema CUF haitashiriki katika uchaguzi huo
wa Machi 20, mwaka huu na kuichia CCM
iendelee kujitangazia ushindi wa urais, viti vyote
54 vya uwakilishi na viti vyote 111 vya udiwani.

Waziri simba chawene aagiza maafisa ardhi na watendaji wanaosababisha migogoro ya ardhi mvomero wafukuzwe kazi.

Waziri simba chawene aagiza maafisa ardhi na watendaji wanaosababisha migogoro ya ardhi mvomero wafukuzwe kazi.

Waziri wa nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na
serikali za mitaa, Tamisemi, George
Simbachawene ameagiza mamlaka mbalimbali
kuwafukuzwa kazi ndani ya siku 14 watendaji na
wenyeviti wa vijiji watakaobainika kuhusika na
uchochezi wa migogoro ya ardhi wilayani
Mvomero, sambamba na kuhamishwa kwa
watumishi waliokaa muda mrefu katika wilaya
hiyo.
Waziri Simbachawene amesema hayo wakati
akizungumza na viongozi na watumishi wa
halmashauri ya wilaya ya Mvomero na mkoa wa
Morogoro, ambapo amepokea taarifa
inayohusiana na changamoto za wilaya hiyo
ikiwemo juu ya migogoro ya ardhi, huku lawama
zikielekezwa na viongozi kwa baadhi ya
watendaji na viongozi wa serikali katika kuhusika
na kukuza na kuendeleza migogoro hiyo pamoja
na ukosefu wa baraza la ardhi katika wilaya hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe
katika kikao hicho, ameiomba mamlaka ya kuzuia
na kupambana na rushwa Takukuru kuwaongeza
wataalamu ili kukabiliana na maswala ya rushwa
ambayo yameonekana kushika kasi katika baadhi
ya wilaya na kusababisha migogoro ya ardhi
kuzidi kukua, ambapo waziri Simbachawene
akaagiza kuchunguzwa na kufukuzwa kwa
watendaji wote watakaobainika kuchangia kukua
kwa migogoro hiyo ya ardhi na kwamba serikali
haitamvumilia yeyote atakayebainika kuwa
chanzo cha migogoro hiyo.
Katika siku ya pili ziara yake mkoani Morogoro,
waziri huyo wa Tamisemi ameweza kuembelea
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na
kueleza kuridhishwa na utendaji kazi na jitihada
zinazofanywa na watumishi, wakiongozwa na
mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Ritta
Lyamuya, pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa
kisasa wa kituo kikuu cha mabasi Msamvu,
pamoja na kuzungumza na viongozi wa mkoa,
wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri
za wilaya.chanzo Itv.

Monday, February 22, 2016
no image

TAMISENI yawataka watumishi mkoan Arusha kutofanya kazi kwa mazoea.soma zaidi.

Tamisemi yawataka watendaji mkoani Arusha
kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu waziri wa Tamisemi Bw.Suleimani Jaffo
amemtaka katibu tawala wa mkoa wa Arusha
kumpatia orodha ya watendaji wanaoendelea
kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha
wananchi kuteseka bila sababu za msingi ili
hatua zikiwemo za kuwafukuza kazi zichukuliwe
haraka kwani wakati wa kubembelezana
umekwisha.
Mh.Jaffo ameyasema hayo baada ya kupewa
taarifa inayopingana na hali halisi ya utekelezaji
wa majukumu mbalimbali likiwemo la
kushughulikia maafa yanayowapata wananchi
iliyosababisha baadhi ya watendaji kushindwa
kujieleza na wengine kutupiana lawama na
kuikana maelezo yao wenyewe.
Mkanganyiko wa watendaji hao ulikuja baada ya
naibu waziri Mh.Jaffo kutaka kupata maelezo ya
watendaji hao wanavyoshughulikia majanga
mbalimbali yanayowapata wananchi likiwemo la
kuezuliwa kwa shule ya msingi isimani lililotokea
Desemba mwaka jana ambalo hadi sasa hatua
hazijachukuliwa licha ya kuwa ndani ya uwezo.
Katika sakata hilo kadiri viongozi na watendaji
hao walivyojaribu kutoa maelezo yaliendelea
kutofautiana jambo ambalo Mh.Waziri.Jaffo
amesema linalodhihirisha wazi kuwa lipo tatizo
ambalo serikali haiwezi kuendelea kulifumbiwa
macho.
Mh.Naibu waziri Suleiman Jaffo alifanya ziara ya
kushtukiza mkoani Arusha ambayo inadaiwa
kuwa ni matokeo ya malalamiko ya wannachi
wakiwemo wanaopatwa na maafa ama majanga
mbali mbali ya kuchelewa kupata msaada wa
serikali licha ya kupewa ahadi kila janga
linapotokea.
wana mkomoa lema na chadema.

Muungano kwanza na mapinduzi mengine yatasuri asema Dk.shein.soma zaid.

Muungano kwanza na mapinduzi mengine yatasuri asema Dk.shein.soma zaid.

DR SHENI ASEMA MUUNGANO NA MAPINDUZI
KWANZA MENGINE YATASUBIRI.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein akizungumza na Jumuiya ya
Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mjini kichama
leo katika ukumbi wa CCM Amani Mjini Unguja na
kuwataka Vijana kulinda Muungano na Mapinduzi
ya Zanzibar,ikiwa ni katika hatua za uimarishaji
wa Chama cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa
marudio wa Machi 20, 2016.chanzo goodluck peter mtenga breaking news tanzania.

Sarafu ya uingereza yaporomoka soma zaid.

Sarafu ya uingereza yaporomoka soma zaid.


BBC Dira TV: Sarafu ya Uingereza - pauni-
imeporomoka kufuatia mjadala kuhusu Uingereza
kujitoa au kutojitoa katika Umoja wa Ulaya, EU.
Kura ya maoni itapigwa mwezi Juni mwaka huu
kuamua. Nini mtazamo wako kuhusu nchi
kuwepo au kutokuwepo kwenye jumuiya au
muungano wa mataifa?chanzo bbc tv.

Serikalai ya uingereza yaridhishwa na utendaji wa serikal ya awamu ya tano.

Serikalai ya uingereza yaridhishwa na utendaji wa serikal ya awamu ya tano.

erikali ya Uingereza imeeleza kuridhishwa na
utendaji kazi wa rais wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli katika kubana matumizi pia
kupambana na rushwa na kwamba nchi yake iko
tayari kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika
kuliimarisha jeshi la polisi na idara ya
mahakama.
Hayo yamesemwa na balozi wa Uingereza hapa
nchini Dianna Melrose alipokutana na kufanya
mazungumzo na rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini
Dar es Salaam na kuongeza kuwa waziri mkuu
wa Uingereza David Cameroon anaridhishwa na
hatua zinazochukuliwa na rais John Pombe
Magufuli katika kupambana na rushwa hapa
nchini.
Mbali na balozi huyo wa uingereza hapa nchini
pia rais Dkt John Pombe Magufuli pia amekutana
na kufanya mazungumzo na balozi wa Afrika
Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku, na kisha
Mh Mohamed Yasserel Shawaf balozi wa Misri
hapa nchini mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Katika tukio jingine rais Dkt John Pombe
Magufuli amepokea hati za utambulisho za
mabalozi ambapo balozi wa kwanza kuwasili
Ikulu na kukabidhi hati zake ni balozi wa jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo DRC Mh Jean Pierre
tshampanga na kisha kufuatiwa na balozi wa
Namibia Mh Theresia Samaria matukio
yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na rais mstaafu wa awamu ya nne
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es
Salaam.chanzo itv.

Sunday, February 21, 2016
Tayari hadharani kikosi cha kwanza cha fc.barcelona zidi ya arsenal.tareh23/02.2016.soma zaidi

Tayari hadharani kikosi cha kwanza cha fc.barcelona zidi ya arsenal.tareh23/02.2016.soma zaidi

Ter Stegen, Claudio Bravo, Masip, Piqué,
I.Rakitic, Sergio, Dani Alves, A.Iniesta, Suárez,
Messi, Neymar Jr, Mascherano, Munir, Jordi Alba,
S.Roberto, Adriano, Aleix Vidal, Vermalen &
Mathieu.

Miundombinu ya muwekezaji wa shamba la TPC kilimanjaro rahalibiwa na wananchi.soma zaidi.

Miundombinu ya muwekezaji wa shamba la TPC kilimanjaro rahalibiwa na wananchi.soma zaidi.

Wakulima wa mpunga katika skimu ya
umwagiliaji Mawala kata ya Kahe wilaya ya
Moshi mkoani Kilimanjaro wamevamia na
kuharibu miundombinu ya ugawaji maji kupeleka
katika mashamba ya miwa ya mwekezaji wa
kiwanda cha sukari TPC.
Wakulima hao wamesema wamelazimika kufanya
uharibifu huo na kuelekeza maji katika mfereji wa
mashamba ya wakulima kwa madai ya
mwekezaji huyo kukausha maji yote mferejini na
kuelekeza kwenye mashamba ya miwa hali
ambayo imesababisha kusababisha mpunga
uliopandwa kukauka kwa kukosa maji.
Wamesema wanasikitishwa na hatua ya
mwekezaji huyo kukiuka makubaliano ya
kugawana maji hayo kwa wiki siku tatu badala
yake anatumia mashine ya kuvuta maji yote
mferejini na kueleleza kwenye mashamba ya
miwa hali ambayo imesababisha mashamba ya
mpunga kukauka kwa kukosa maji.
Diwani wa kata ya Kahe mashariki Bw. Rodrick
Mmanyi amelazimika kufika katika eneo la tukio
na kuwataka wakulima kuacha kufanya vurugu na
kuahidi kushirikiana na viongozi wa umoja wa
wakulima hao ili kufanya mazungumzo na
uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kumaliza
mgogoro huo ambao unahatarisha amani.
Hata hivyo juhudi za kumpata afisa utawala wa
kiwanda cha sukari TPC Japhary Ally
kuzungumzia mgogoro huo hazikufanikiwa baada
ya kusema yuko kwenye kikao ambapo kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhani Mungi
amesema amepata taarifa hizo na kwamba yuko
safarini atatoa taarifa hizo kesho.chanzo ITV TZ.

Tatizo la afya nchini bado ni changamoto kitanda kimoja walala watu 2.sma zaid.

Tatizo la afya nchini bado ni changamoto kitanda kimoja walala watu 2.sma zaid.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete
iliyoanzishwa mwaka 1906, inakabiliwa na
changamoto ya akinamama wazazi na
wanaojifungua kulala zaidi ya wawili katika
kitanda kimoja, hali ambayo imedaiwa kuwa,
naweza kusababishia watoto wanaozaliwa
kuondoka na maambukizi katika kile
kinachodaiwa kuwa ni miundomninu ya zamani
ya majengo kutofanyiwa marekebisho.
Hayo yamebainishwa na katibu tawala msaidizi
huduma za afya mkoa wa Tabora ambaye pia ni
mganga mkuu wa mkoa Dkt Gunini Kamba,
wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa viti maalum
Chadema aliyekwenda hospitalini hapo kwa lengo
la kutambua changamoto na kutafuta ni jinsi gani
anaweza kushiriki katika kuzitatua.
Kwa upande wake mbunge huyo wa viti maalum
mkoa wa Tabora Chadema Mhe. Hawa
Mwaifunga amesema kuwa, kwa pamoja
wabunge kumi na nne wa mkoa wa Tabora kila
mmoja akitoa sehemu ya kipato kinachotokana
na nafasi zao, wanaweza kutatua changamoto
hizo na kuisaidia serikali kutekeleza majukumu
yake.chanzo radio one stereo.

Wauza simu waomba waonzewe mda wa kuzima simu feki..soma zaidi.

Wauza simu waomba waonzewe mda wa kuzima simu feki..soma zaidi.

Wakati tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu
zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya
wafanyabiashara za simu za mikononi katika
soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam walalamikia
kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa
kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki
huku watuamiaji nao wakilalamikia kuwa
watakosa mawasiliano kutokana na simu origino
kuwa ghali.
Siku chache baada ya mamalaka ya mawasiliano
nchini TCRA kuonesha msimamo wake wa
kuzifungia simu hizo baadhi ya wafanyabiashara
katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam
wameelezea kuwa katika wakati mgumu
kutokana na kukosa wateja na hivyo kusababisha
hata simu ambazo sio feki kukosa wateja na
kubaini kupata hasara kubwa kutokana na azimio
hilo ambapo wameziomba mamlaka husika
kuongeza muda ili kuwapa nafasi ya kujipanga ili
kutafuta mtaji wa kuingiza simu zinazotakiwa.
Baadhi ya watumiaji waliozungumza na ITV nao
wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la
kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo
kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika
kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei
elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa
wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.
Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia
walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya
kuzima simu feki na walikuwa na haya ya
kusema.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayri
imeonesha msimamo na kutangaza kuwa tarehe
kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki
zitazimwa ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa
kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika
Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari
wameshazifungia kabisa simu feki.

Trump aibuka mshindi south carolina.soma zaid.

Trump aibuka mshindi south carolina.soma zaid.

Mgombea kiti wa chama cha Republican katika
uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani Donald
Trump ameshinda kura ya mashinani katika
jimbo la Carolina Kusini.
Bwana Trump ambaye awali mwezi huu,
alishinda katika jimbo la New Hampshire,
amepata kura nyingi huko Carolina Kusini huku
wapinzani wake Ted Cruz na Marco Rubio
wakimfuatia kwa karibu.
Kutokana na matokeo mabaya ya gavana wa
zamani wa Florida, Jeb Bush, kakake aliyekuwa
Rais wa Marekani George W. Bush, amejiondoa
katika kinyanganyiro hicho.
Awali mgombea kiti hicho kwa chama cha
Democrats Bi Hillary Clinton ameibuka mshindi
katika kura ya mashinani eneo la Nevada, na
kubwaga mpinzani wake Bernie Sanders.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.

Saturday, February 20, 2016
no image

Polisi wamsaka mshambuliaji michigani.soma zaid.


Polisi nchini Marekani wanamsaka mtu mwenye
silaha ambaye amefyatua risasi na kuwaua watu
kadha katika mji wa Kalamazoo, jiombo la
Michigan.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema watu
sita wameuawa.
Watu wanne waliuawa katika mgahawa mmoja na
wengine wawili katika duka la kuuza magari.
Maafisa wanasema mwanamume huyo
anazunguka eneo hilo akiwafyatulia risasi watu
kiholela.
Mashambulio hayo yanadaiwa kuwa na uhusiano
na kisa cha awali cha ufyatuaji wa risasi katika
maegesho ya magari, ambapo mwanamke mmoja
alijeruhiwa vibaya.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako

Mtoto albino wa miaka mitano akatwa mikono na kuuwawa nchini Burundi.soma zaid.

Mtoto albino wa miaka mitano akatwa mikono na kuuwawa nchini Burundi.soma zaid.


Mtoto wa kike wa miaka mitano mwenye
ulemavu wa ngozi(Albino) ametekwa kisha
kuuawa kwa kukatwa viungo na watu
wenye silaha.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi
wake na kuwashambulia wazazi na
kutokomea kusikojulikana na mtoto huyo
mlemavu.
Walifuatiliwa na majirani wa familia hiyo
na kuukuta mwili wa mtoto ukiwa
umetupwa bila kuwa na mkono mo.chanzo jamii forums.

Oparation ya utumbuaji majibu kwa wasio lipa kodi sio uonevu.asema waziri mkuu.

Oparation ya utumbuaji majibu kwa wasio lipa kodi sio uonevu.asema waziri mkuu.

Waziri Mkuu Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA
amesema oparesheni ambayo inafanyika sasa
kuhakikisha kila mtu analipa kodi na kudumisha
nidhamu kwa watumishi wa umma haina nia ya
kuwaadhibu watu.
Amesema hatua hiyo ni kuhakikisha kila mtu
anatekeleza wajibu wake wa kulipa kodi ili
serikali iweze kutekeleza mipango yake
iliyojiwekea na hivyo amewaomba wananchi
kuisaidia serikali kutekeleza oparesheni hiyo.
Mheshimiwa MAJALIWA ameyasema hayo katika
mkutano wa Jumuiya ya Wanarukwa na Katavi
waishio jijini Dar es Salaam ambapo amesema
serikali haitamuonea mtu wala huruma mtu
yoyote ambaye anakwenda kinyume na sheria za
nchi.
Aidha mkuu huyo amewataka Watanzania
kutumia fursa zinazowazunguka kama madini,
kilimo, mifugo na nyingine za kujiletea
maendeleo.
Naye Waziri Mkuu Mstahafu MIZENGO PINDA
amesema kwa sasa kila mtu anapaswa kujua
kuwa ni jukumu lake kujiletea maendeleo kwani
haitakuwa na faida yoyote kama mtu amebaki
kuikosoa serikali bila ya kutoa njia mbayala ya
kurekebisha hicho ambacho anaona hakijawa
sawa.chanzo itv tz.

Al Qaida wateka mji wa Ahwar,Yemeni.

Al Qaida wateka mji wa Ahwar,Yemeni.

Inaarifiwa kuwa wapiganaji kadha wa al-Qaeda
nchini Yemen, wameuteka mji wa Ahwar, Kusini
mwa Yemen.
Duru za huko zinanukuliwa kusema kwamba,
wakati wapiganaji walipoingia mjini humo,
walipambana na kikosi kilichokuwa kikilinda mji
huo na watatu waliuwawa.
Vilevile wapiganaji waliweka vizuizi vya
barabarani na kupandisha bendera yao katika
majengo ya serikali.
Wadadisi wanasema, kwa kuteka mji wa Ahwar,
itaisaidia al-Qaeda kujizatiti katika mwambao wa
jimbo la Abyan, ambako tayari inadhibiti miji
mengine miwili.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako

Msimamo wa Cuf zanzibar waendelea.

Msimamo wa Cuf zanzibar waendelea.

Mshindo wa CUF Z’bar
KIMYA cha viongozi wa Chama cha Wananchi
(CUF) kina mshindo visiwani Zanzibar, hata hivyo
chama hicho kinasema kinapambana na sera za
kibabe za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM),
Kinaeleza kuwa, umoja na mshikamano wa
wapenda haki hasa katika kipindi hiki cha
mgogoro wa kisiasa ndio njia pekee ya
kuhakikisha sera haramu na za kibabe zinazikwa
visiwani humo.
Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Mipango,
Uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Taifa
amesema, CUF na Watanzania sasa wanaelewa
kwamba, kwa Serikali ya CCM hoja si haki
isipokuwa kupata kile wanachokitaka.
Akizungumza na mtandao huu leo kwenye Ofisi
Kuu ya CUF amesema, CCM haifuati sheria na
imejikita katika kukandamiza uhuru na
demokrasia huku utafutaji wa suluhu ukiwa ni wa
mabavu.
“Mambo mengi yanayofanywa na serikali
hayafuati sheria na misingi ya demokrasia,
hufanya mambo kwa kulinda maslahi ya chama
tawala hata kama wanajua wanavunja sheria,”
amesema Mketo.
Ametaja baadhi ya mambo ambayo yanaviashiria
vya uvunjwaji wa sheria na ukandamizaji wa
demokrasia kuwa ni pamoja na kulazimisha
vyama vya siasa kufuata matakwa yao pia Jeshi
la Polisi kutotendea haki vyama vya upinzani.
“Kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi visiwani
Zanzibar bila ya sababu za msingi ni
kuikandamiza demokrasia na kukiuka sheria,
kama uchaguzi haukuwa wa haki, nani
aliyeipoteza haki?” amehoji Mketo na kuongeza;
“Hata siku moja chama cha upinzani
hakitafanikiwa kuiba kura, sababu Tume na
watendaji wake huchaguliwa na Rais ambaye
anatoka chama tawala.
“Ili wapinzani waibe kura inabidi washirikiane na
Tume ambao ni Mwenyekiti, Wakurugenzi na
Makamishina, wote wamechaguliwa na Rais, kwa
hiyo si rahisi kuwarubuni,” amesema.
Mketo amedai kuwa, chaguzi nyingi zilizopita
mgombea wa CUF alikuwa ni mshindi lakini
waliminya demokrasia kwa Tume kumpitisha
wanayemtaka, pia ametoa mfano wa uchaguzi
uliofanyika mwaka 1995.
“Uchaguzi wa mwaka 1995, mgombea wa
upinzani alipita, kituo cha televisheni cha DTV
ambacho sasa ni Chanel Ten, kilifungiwa baada
ya kutangaza kuwa Maalim Seif aongoza
Zanzibar,” amesema.
Mketo amesema, wagombea wote wa CUF
wameiandikia barua tume ya ZEC na viapo ili
kuwaeleza kwamba, hawatashiriki katika
uchaguzi wa marudio.
“Hata kama ZEC ikilazimisha kuweka jina la
Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF na
ikaonekana ameshinda, Maalim Seif hatokubali
kuichukua nchi, sababu ameshakataa kurudiwa
kwa uchaguzi,” amesema na kuongeza;
“Wananchi wengi wa Zanzibar hawakubali
kurudia uchaguzi, wanaijua demokrasi na haki
yao, hawatapiga kura sababu viongozi
wanaowataka, wameshawachagua.”
Kuhusu kuzuiliwa kwa maandamano ya Jumuiya
ya Wanawake CUF-Taifa amesema, kitendo cha
polisi kuwanyima kibali ni kinyume cha sheria na
walikifanya hivyo ili kulinda masilahi ya serikali.
“Kwa mujibu wa sheria namba 5 ya vyama vya
siasa ya 1992, imetoa haki kwa vyama vya siasa
kuandamana na inasema vyama vinatakiwa kutoa
taarifa ya maandamano kabla ya siku mbili,”
amesema Mketo.

Beaking news.Yoweli  kaguta mseveni ashinda urais.soma zaid.

Beaking news.Yoweli kaguta mseveni ashinda urais.soma zaid.

mage copyright
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza
Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi
wa urais uliofanyika Alhamisi.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na
asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu
wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru
Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata
kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia
35.37%.
Wasifu wa Yoweri Museveni
Besigye na Muntu waachiliwa huru Uganda
Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na
Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa
uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro
nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa
upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao
ya kijamii.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.

Kasi ya Rais magufuri

Kasi ya Rais magufuri

WAFANYABIASHARA wa Rwanda
wamepongeza hatua zinazochukuliwa na
Rais John Magufuli katika Bandari ya Dar
es Salaam, kwa kuimarisha ufanisi wa
bandari, kukuza biashara baina ya
Tanzania na nchi jirani.
Aidha wamesema tangu Rais Magufuli
aanze kuchukua hatua hizo, mizigo yao
imekuwa salama zaidi na wamefanikiwa
kuipata kwa urahisi tofauti na zamani
ambapo mingi ilikuwa ikipotea.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Mambo
ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Mahiga wakati akizungumza na waandishi
wa habari katika Ukumbi wa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA).
Akizungumza baada ya kutua nchini
akitokea Kigali, Rwanda, Balozi Mahiga
alisema pia Rais wa nchi hiyo, Paul
Kagame amemhakikishia kuwa ataendelea
kushawishi wafanyabiashara wake
kutumia Bandari ya Dar es Salaam, ili
kukuza uhusiano wa kibiashara uliopo.
“Nilipata bahati ya kuzungumza na
wafanyabiashara wa kule... wamepongeza
sana hatua zinazochukuliwa na Rais
Magufuli pale bandarini kwa sababu
wanasema sasa hivi itawasaidia sana
kuhakikisha usalama wa mizigo yao,”
alisema Blozi Mahiga.
Alisema wafanyabiashara hao pia
wameomba mkutano wa pamoja na
wenzao wa Tanzania, ili kujadili masuala
mbalimbali, ikiwemo fursa za uwekezaji
ndani ya Rwanda na Tanzania.
Alisema Rais Kagame anaunga mkono
ujenzi wa reli itakayotumika kusafarisha
mizigo kwa kuwa ni njia mojawapo ya
kukuza uchumi wa nchi hizo mbili rafiki.
Akizungumzia safari yake hiyo, Balozi
Mahiga alisema, alienda nchini humo
kujadiliana masuala mbalimbali
aliyoagizwa na Rais Magufuli kwa Rais wa
nchi hiyo, ambapo walijadili masuala
matatu, ikiwemo machafuko
yanayoendelea Burundi.
Alisema kuhusu machafuko ya Burundi,
Rais Kagame alikanusha tuhuma
zinazotolewa na nchi hiyo pamoja na
jumuiya za kimataifa kuwa anahusika
katika kuchochea machafuko hayo.
Kwa mujibu wa Balozi Mahiga,
maandamano ya nchi nzima yaliyofanyika
wiki iliyopita nchini Burundi ya
kuishutumu Rwanda kuhusika na
machafuko nchini mwao, yalishitua nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
kutokana na baadhi ya maneno ya chuki
yaliyokuwa yakitolewa na wananchi hao
dhidi ya nchi hiyo.
Alisema hali hiyo, ilihofiwa kwamba
ingeweza kuvunja mazungumzo ya
kutafuta suluhu yanayoendelea.
“Nilimuuliza Rais Kagame kuhusu hili
suala, akasema hatachukua hatua yoyote
licha ya kwamba wananchi wake
wamemlazimisha kufanya kitu. Lakini
alisema atashiriki katika majadiliano ya
kutafuta suluhu ya Burundi. “Sisi tulikuwa
tunahofia kuwa huenda akachukua hatua
ambazo zingeweza kuleta matatizo na
hata mazungumzo yanayoendelea
kuvunjika, lakini ameniambia hatachukua
hatua yoyote inayoweza kusababisha
kuvunjika kwa uhusiano,” alisema Balozi
Mahiga.
Hata hivyo, alisema Rais Kagame
alilalamikia nchi yake kushutumiwa kwa
kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi
wa Burundi, ili kuipindua Serikali ya nchi
hiyo na kutaka Jumuiya za Kimataifa,
kuwaondoa wakimbizi zaidi ya 70,000 na
kuwahamishia nchi nyingine za jirani.
“Aliniambia kuwa kuendelea kuwa na
hawa wakimbizi katika nchi yake,
kunaweza kumletea matatizo makubwa,
kwa sababu amekuwa akilaumiwa sana.
Hivyo kuliko lawama, ni bora hizi Jumuiya
za Kimataifa zikawaondoa wakimbizi,”
alisema.
Alisema kwa mujibu wa Rais Kagame,
Rwanda itaendelea kushiriki katika
mijadala mbalimbali ya kutafuta suluhu ya
Burundi na itahakikisha Burundi inakuwa
salama.
Jambo lingine walilozungumza na Rais
Kagame ni mkutano wa marais wa Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotarajiwa
kufanyika mwisho wa mwezi nchini
Tanzania, ambapo pia alikuwa katika
hatua ya mwisho katika kukamilisha
ajenda na watakaoshiriki mkutano huo.

Thursday, February 18, 2016
Kwa mara ya kwanza tangue aingie madarakani.Rais azungumza na wasanii.

Kwa mara ya kwanza tangue aingie madarakani.Rais azungumza na wasanii.

Rais Magufuli akiambatana na makamu wa Rais
Mh. Samia Suluhu Hassani, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi
Abdalah Bulembo pamoja na mawaziri kadhaa wa
serikali yake amekutana na makundi hayo ikulu
jijini Dar es salaam kwa nia ya kuwashukuru na
kutoa agizo la katazo la utoaji wa vibali vya
kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.
Aidha Dkt Magufuli ameiagiza mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) kufanya operesheni
maalum ya kukamata kazi zote za wasanii zisizo
na alama maalum ya mamlaka ya mapato nchini
kufuatia malalamiko ya wasanii kushindwa
kumudu ushindani katika soko kutokana na kazi
nyingi kuingizwa nchini bila ya kulipia ushuru.
Pia amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa Na Michezo Mh. Nape Nnauye kuangalia
utaratibu wa chama cha haki miliki Tanzania
(COSOTA) kuwa chini ya wizara yake tofauti na
ilivyo sasa ambapo chama hicho kiko chini ya
wizara ya viwanda na biashara.
Kwa upande wake makamu wa Rais Mh. Samia
Suluhu hassani amewashukuru wasanii hao kwa
mchango wao uliokiwezesha Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 na kuwataka kuendelea kushirikiana
na serikali katika masuala mbalimbali ya
kuhamasisha maendeleo huku waziri mkuu Mh
Kassim Majaliwa akiwaahidi kusimamia kwa
vitendo maagizo yote yaliyotolewa na Rais.
Kwa upande wasanii hao wamemshukuru Rais
kwa uamuzi wake wa kuwaita na kuzungumza
nao ikiwa ni jitihada za kutambua mchango wao
katika uchumi na maendeleo ya nchi na miongoni
mwa makundi yaliyofanikisha chama cha
mapinduzi kushinda katika uchaguzi mkuu wa
2015..

Wakazi 150 gongolamboto walazimika kulala inje baada ya nyumba kubomolewa.soma zaidi.

Wakazi 150 gongolamboto walazimika kulala inje baada ya nyumba kubomolewa.soma zaidi.

Wakazi zaidi 150 wa Guluka kwalala
Gongolamboto jijini Dar es Salaam ambao
nyumba zao 25 zimebolewa wamesema kwa sasa
watalazimika kulala nje kwa kukosa nyumba za
kuishi baada ya zoezo la bomoabomoa kufanywa
na uongozi wa kiwanda cha kampuni ya NAMERA
huku wakazi hao wakisema zoezi zima la
ubomoaji limefanyika wakati kesi kuendelea
kusikilizwa katika mahakama ya ardhi.
Wakiongea na ITV mara baada ya kufika katika
eneo hilo la Guluka kwalala na kushuhudia
mabaki ya nyumba ambazo zimebomolewa
wananchi hao wamelalamikia zoezi zima la
ubomoaji wa nyumba hizo baada ya idadi kubwa
ya wakazo hao kushindwa kutoa samani zao
ndani wakati zoezi la ubomoaji likifanyika na
kusimamiwa na askari wa jeshi la polisi.
Bwana Fitiri Juma ambaye ni mjumbe wa seikali
ya mtaa wa Guluka Kwalala akiongea na ITV
amelalamikia viongozi wote wa eneo hilo kutofika
wakati zoezi la ubomoaji likendelea na
kusababisha wananchi hao kupata hasara ya mali
zao.
Katika kutaka kujua juu ya uhalali wa zoezi zima
la ubomoaji kama limezingatia misingi ya sheria
ITV iliutafuta uongozi wa kiwanda cha NAMERA
ambapo uongozi umekiri kutelezela zoezi hilo na
kulipa fidia wananchi wote waliojenga eneo hilo
wanalodai ni la kiwanda.chanzo itv.

Uturuki yaapa kulipiza kisasi shambulio.

Uturuki yaapa kulipiza kisasi shambulio.

Uturuki imeapa kulipiza kisasi dhidi ya
washambuliaji wa mlipuko mkubwa wa bomu
katika mji mkuu wa Ankara,ambao umewawacha
watu 28 wakiwa wamefariki na wengine 61
wakijeruhiwa.
''Uturuki haitaogopa kutumia uwezo wake wa
kujilinda,rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
Maafisa wamesema kuwa gari lililojaa vilipuzi
lililipuliwa wakati ambapo mabasi ya jeshi
yalikuwa yakipita siku ya jumatano.Mazishi
yanatarajiwa kufanyika siku ya Alamisi.
Hakuna kundi lolote kufikia sasa lililodai
kutekeleza shambulio hilo.
Marekani ilishtumu mlipuko huo ,huku msemaji
wa baraza la usalama wa kitaifa Ned Price
akisema,tunasimama pamoja na Uturuki ,mshirika
wa Nato na mshirika wetu mkuu.
Mlipuko huo ulitokea katika eneo la karibu na
bunge na makao makuu ya jeshi.
Moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka eneo
hilo na mashahidi wanasema mlipuko huo
ulisikika mji mzima.chanzo bbc.com.

Watumishi watatu TCRA wasimamishwa kazi.soma zaidi

Watumishi watatu TCRA wasimamishwa kazi.soma zaidi


# Habari:Waziri wa ujenzi, uchukuzi na
mawasiliano Prof Makame Mbarawa
amewasimamisha na kuwastaafisha kazi
watendaji watatu wa mamlaka ya mawasiliano
nchini TCRA kwa kuhujumu kifaa cha kuhakiki
ubora wa mawasiliano ya ndani na nje TTMS.chanzo radio one sterio.

Tatizo la ajira afrika na kati chanzo ni rushwa asema makamu wa rais tz.soma zaid.

Tatizo la ajira afrika na kati chanzo ni rushwa asema makamu wa rais tz.soma zaid.

Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassani
amesema nchni za Afrika Mashariki na kati
zitaweza kuongeza ajira zaidi iwapo zitapunguza
rushwa, urasimu na kuhamisha uwekezaji toka
nje ya nchi kwa kuweka sera nzuri na masharti
nafuu.
Akizungumza na vyombo vya habari katika
ufunguzi wa mkutano wa nane wa kimataifa wa
jumuiya ya shirikisho la mifuko ya hifadhi ya
jamii ya nchi za Afrika Mashariki na kati, Mhe
Samia amelitaka shirikisho hilo kuzisaidia nchi za
Afrika Mashariki na kati kuzalisha ajira na
kusisitiza lengo la Tanzania ni kuingiza sekta
isiyorasmi katika mifumo ya hifadhi ya jamii ili
kuboresha maisha ya watanzania.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera bunge,
kazi, ajira, vijana na walemavu Mhe. Jenista
Mhagama amesema kupitia mpango wa kukuza
ajira kwa vijana kwa kushirikisha mifuko ya
hifadhi ya jamii kutaweza kufikiwa lengo la
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ambapo
pia amewataka watanzania kutokuwa na hofu ya
kufirisika kwa mifuko hiyo kutokana na kujiingiza
katika biashara ya uwekezaji.

RATIBA FA CUP ENGLAND TAR 20--21

RATIBA FA CUP ENGLAND TAR 20--21

RATIBA FA CUP:
Tarehe 20feb:
Arsenal & hullcity 15:45pm
Reading & westbrom 18:00pm
Watford & leeds utd 18:00pm
Bournemouth & everton 20:15
_
Tarehe 21
Blackburn & westham 17:00pm
Tottenham & crystal palace 18:00pm
Chelsea & man city 19:

Maajabu mfungwa wa kike nchini vietnam ashika mimba akiwa jela.

Maajabu mfungwa wa kike nchini vietnam ashika mimba akiwa jela.

wa kiume, ili kukwepa hukumu ya kifo.
Askari jela wanne nchini Vietnam
wamesimamishwa kazi kwa kosa la kuzembea
kazini baada ya mfungwa wa kike
aliyehukumiwa kunyongwa kushika mimba.
Kwa mujibu wa sheria ya Vietnam inasema
mwanamke mjamzito au mwenye mtoto wa chini
ya umri wa miaka mitatu hawezi kunyongwa na
badala yake hukumu yake inafaa kubadilishwa
na kuwa kifungo cha maisha jela.
Hivyo kwa Sasa inatarajiwa kwamba hukumu
yake itapunguzwa kutoka kifo hadi maisha jela
kwa sababu atakuwa na mtoto wa chini ya
miaka mitatu.
Aidha maafisa wanasema mfungwa huyo
alinunua mbegu kutoka kwa mfungwa wa kiume
wa umri wa miaka 27 kwa $2,300.chanzo jamii forums

Southampton kumuuza sadio mane.soma zaid.

Southampton kumuuza sadio mane.soma zaid.

OUTHAMPTON ipo tayari kumuuza winga wake
wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane lakini
imepanga dau la Pauni 30 milioni kwa timu
yoyote ambayo inamtaka Mane anayetarajiwa
kuzusha vurugu wakati wa dirisha kubwa la
uhamisho.
Manchester City na Manchester United zinadaiwa
zinamtaka staa huyo hatari uwanjani ambaye
amekuwa aking’ara na Southampton iliyomnunua
kutoka Red Bull Salzburg ya Austria katika dirisha
la majira ya joto 2014 kwa Pauni 11 milioni. —

 Habari zilizo tufikia hivi punde Vurugu yazuka jijin mwanza kati ya waendesha pikipiki na polisi.soma zaid.

Habari zilizo tufikia hivi punde Vurugu yazuka jijin mwanza kati ya waendesha pikipiki na polisi.soma zaid.

Jeshi la polisi jijini mwanza limelazimika kutumia mabomu kuwatawanya waendesha pikipiki baada ya kufunga barabara ya Tx igoma kuelekea  uwanja wa ndege.

Wednesday, February 17, 2016
Lori lasababisha taharuki mlima UYOLE mbeya.soma zaid.

Lori lasababisha taharuki mlima UYOLE mbeya.soma zaid.

Zaid ya mabasi 15 na magari mengine 100 yamekwama na kushindwa kupanda mlima UYOLE mkoani mbeya na kuanza kurudi nyuma na kukatisha njiabna hivyo kuzuia magari mengine kupita na kusababisha foleni kubwa .chanzo redio one stereo.

Wimbi la utumbuaji wa majipu watawala wakurugenzi wanne wasimamishwa.soma zaidi.

Wimbi la utumbuaji wa majipu watawala wakurugenzi wanne wasimamishwa.soma zaidi.

Waziri wa nchi ya Rais TAMISEMI mh.George simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzibwa halmashuri nne nchini kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa maofisa wa ofsi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kubatilisha hati chafu zilizopata halmashauri zao. Walikurugenzi hao ni wa halmashauri ya manispaa ya misenyi kagera Elizabeth kitundu, halmashauli ya nanyumbu mtwara mohammed kasega.halmashauri ya kilolo iringa Lukson  mkurugeni wa halmashauri yavmbogwe mkoani geita Abdallah mfaume. Pia amemsimamisha mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa tunduma Halima mpita. Chanzo east africa television.

Monday, February 8, 2016
Mke wa pinda anusurika kifo baada ya kupata ajali.soma zaid.

Mke wa pinda anusurika kifo baada ya kupata ajali.soma zaid.

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu msitaafu maam tunu pinda baada ya ajali walilokuwa wakisafiri kumgonga mwendesha pipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la mkundi manispaa ya morogoro ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la mkundi ikuhusisha gari lenye namba za usajili STK9242 gari la mke wa wazir mkuu mstaafu .mageruhi wengine ni dereva wa gari Bwana Anjelo Gudensi.Tembo nakijana wa familia ya mama tunu pinda Bwana Gilbet sampa.

Mkurugenzi na maofisa wawili wafikishwa mahakamani kwa ufsadi huko mbeya.soma zaidi.

Mkurugenzi na maofisa wawili wafikishwa mahakamani kwa ufsadi huko mbeya.soma zaidi.

Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa takukuru imewafikisha mahakani watumishi watatu wa halimashauri ya wilaya ya mbeya akiwemo mkurugenzi mtendaji, upendo sanga kwa madai ya kuhujumi uchumi .Awali sanga alifika mahakamanibhapo kisikiliza hukumu ya kesi yake iliyofungiliwa na takukuru mwaka 2014.Baada ya hakimu kuwaachia huru, Takukuru walimzunguka na kumkamata tena na maofisa wake ambao walipandishwa tena kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita.maofisa wengine ni mweka hazina Hafidhi mgagi na mhasibu Gershom Bwire na Sanga.chanzo mwananch.

Sunday, February 7, 2016
Makamishina wawili wa ZEC wamsaliti mwenyekiti wa tume jecha.soma zaidi.

Makamishina wawili wa ZEC wamsaliti mwenyekiti wa tume jecha.soma zaidi.

Wakati wanahalakati wa kisiasa mbalimbali wakipinga kufutwa uchaguzi zanzibar wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi wa zanzibar ZEC ndugu NASSOR KHAMIS MOHAMED na AYUBU HAMADI wameibuka jijini Dar es salaam leo na kupinga marudio ya uchaguzi unaotalajia kufanyika mwishobi mwa mwezi uchao kwa madai uchaguzi huo sio wa halalivkulingana na matukio yaliyotokea tangu kufanyika kwa uchaguzi halali wa october2015 mwaka jana.chanzo jamii forums.

Walimu watatu watishiwa kuuwala na wanafunzi wao sumbawanga.soma zaid.

Walimu watatu watishiwa kuuwala na wanafunzi wao sumbawanga.soma zaid.

Wanafunzu wa shule ya sekondari kantalamba ya wavulana manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa wameanza mgomo usiokuwa na kikomo na kutishia kuwauwa walimu watatu shulen hapo iwapo hawatohamishwa.chanzo east africa television.

Wednesday, February 3, 2016
LHRC yamkataka mwenyekiti wa uchaguzi zanzibar azijuzuru.soma zaid.

LHRC yamkataka mwenyekiti wa uchaguzi zanzibar azijuzuru.soma zaid.

LHRC kimemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa zanzibar jecha salum jecha ajiuzuru wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi nakutangaza tareh ya marudio bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.tamko hilo limetolewa jijini Dar es salaam na kaim mkurugenzi mtendaji wa LHRC Bi imelda urrio.

Kiyama cha mafisadi tanzania chaja.soma zaid.

Kiyama cha mafisadi tanzania chaja.soma zaid.

Jaji mkuu asema mahakama ya ufisadi ni kipaombele. Jaji Mkuu othumani chande amesema suala la  uanziswaji wa mahakama maalumu yakushughulikia makosa makubwa ya ufisafi,rushwa na uhujumu uchumi ndicho kipaumbele kikuu inchini kwanza kwa mhimili huo wa dola Mwaka huu.jaji Mkuu alisema hayo Jana alipozungumza na mwananchi kuchakato wa uanziswaji wa mahakama hiyo ambao unatokana na ahadi za Rais maguful aliyoitoa wakati wa kampeni zake katika uchaguzi mkuu2015.

Tuesday, February 2, 2016
Virusi vya  ugonjwa  wa "ZiKA" sasa kwisha.soma zaidi.

Virusi vya ugonjwa wa "ZiKA" sasa kwisha.soma zaidi.

Shirika la Afya  Duniani WHO limesema limeanzisha kitengo maalumu cha kimataifa cha kukabiliana na mripuko wa virusi vya zika huku likielezea wasiwasi wake kuhusu ugonjwa huo unasababisha watoto wa Amerika ya kusini kuzaliwa wakiwa wakiwa na vichwa vidogo pamoja na ubongo ulioathirika, kwamba unaweza ukaenea dadi barani Afrika na Asia.chanzo DW Swahili.

Raia 83 wa Ethopia wahukumiwa kwenda jela miaka mitatu iringa.soma zaid.

Raia 83 wa Ethopia wahukumiwa kwenda jela miaka mitatu iringa.soma zaid.

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa iringa imewahukumu kwenda jela miaka mitatu wahamiaji 83raia wa Ethiopia walipingia nchini bila kibali huku pia ikiwahukumu jela miaka mitano dereva na utingo wa Lori waliowasafirisha wahamiaji hao kutoka jijini Dar es salaam kuelekea nchini Malawi. Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa iringa my.Edrew scout amesema mahakama imezingatia maombi yote ya wahusika lakni kwa kuwa biashara ya usafirishaji binadam imezidi kushamili nchini.

Mwenyekiti wa NEC atua ikulu kwa kishindo.soma zaid.

Mwenyekiti wa NEC atua ikulu kwa kishindo.soma zaid.

Mwenyekiti wa NEC mh.Damian Lubuva amemuhakishia Rais magufulu kuwa tume ipo huru na haijawahi kuingiliwa kimaamzi na Rais au kiongozi yeyote. Lubuva aliyasema hayo Jana baada kumtembelea Rais ikulu.

Monday, February 1, 2016
Mvua zasababisha 6000 kukosa huduma za kijamii malinyi.

Mvua zasababisha 6000 kukosa huduma za kijamii malinyi.

Mvua zinazo endelea kunyesha inchi zimeendelea kuharibu miundombinu.hiyo ni baada ya mvua iliyonyesha jana na kuharibu mawasiliano ya Barabara hapa malinyi mkoani morogoro na kufanya zaidi ya watu 6000 kukosa huduma ya kijamii

Umoja wa Africa AU watishia kujitoa mahakama ya kimataifa ICC.soma zaid.

Umoja wa Africa AU watishia kujitoa mahakama ya kimataifa ICC.soma zaid.

Umoja wa Africa umekubaliana " kuandaa mpango" ambao utafanikisha kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC.hayo yamezungumzwa kwenye mkutano wa siku mbili mjini Addis Ababa Ethiopia . mwenyekiti mpya wa Au Rais  wa chadi Idriss Deby amesema ICC inawalenga viongozi wa Africa. Au inasubiri ICC kutathini wasiwasi ulioneshwa na umoja huo.Raisi wa Kenya Uhuru kinyatta ambaye aliwakilisha pendekezo hilo alisema yeye pamoja na naibu wake William Ruto wamekuwa wakikabiliwa na kesi zenye msingi dhaifu wa uchunguzi na wenye kuchochewa kisiasa kutoka kwa ICC.ICC unasema inasaka haki na usawa kwa waafrika walioathiriwa na mizozo.chanzo salim kikeke.

Jaji mkuu othumani chande awapa mahakimu  siku saba tu(7) soma zaid.

Jaji mkuu othumani chande awapa mahakimu siku saba tu(7) soma zaid.

Mahakimu 508 walioshindwa kumaliza kutoa hukumu kwa mashauri yaliyopangwa hadi Mwaka Jana watakiwa kuyamaliza ndani ya siku7.Alisema kiwango cha kesi kwa kila hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi na mahakama ya wilaya ni 250, ambapo mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 Mwaka Jana.

Back To Top