Jambazi sugu akamatwa Dar.soma zaid
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es
Salaam, limefanikiwa kumkamata mtu
mmoja anayedaiwa kuwa jambazi sugu
Abdallah Said (45) kwa makosa ya
ujambazi wa kutumia silaha na uvamizi
kwenye vituo vya Polisi ikiwemo kituo cha
Stakishari na taasisi mbalimbali za fedha
zikiwemo benki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari ,
Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar
es Salaam, Simon Sirro, amesema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo
la Kariakoo baada ya askari kufanya
upelelezi wa kuwasaka watuhumiwa sugu
wanaojihusisha na makosa yakiwemo
ujambazi wa kutumia silaha.
Amesema katika uchunguzi wa
wamebaini kuwa mtuhumiwa huyo
alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa
makosa ya ujambazi wa kutumia silaha
ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji ya
kutumia silaha.
Kamanda, Sirro amesema mtuhumiwa
baada ya kufikishwa kituo cha polisi na
kuhojiwa, alikiri kuhusika na matukio
mbalimbali ya mauaji katika kituo cha
Polisi Stakishari na taasisi za fedha
ambazo ni Benki ya Access Mbagala, Benki
ya NMB Mkuranga, Benki ya CRDB na CBA
Chanika, Road Block ya Polisi Kongowe na
matukio mengine.
Aidha kamanda huyo maesema kuwa
mtuhumiwa huyo pia aliwataja baadhi ya
viongozi waanzilishi wa mipango ya
uvamizi na uporaji wa silaha na mauaji
kwa kutumia pikipiki ambao ni
Abdulaazizi Ndobe, Sheykh Mtozeni,
Omari Matimbwa,Haji Ulatule,Nasoro
Utaule Sasoro Mpemba na wenzake.
Mtuhumiwa huyo pia alitaja mipango yote
ilifanyika katika msikiti wa Kitonga na
yeye akiwa mtaalam na mshauri wa
kitaalam kwa upande wa utumiaji wa
silaha.
Wakati huo huo.Jeshi hilo linamtafuta,
Heri Mpopezi mwenye umri kati ya miaka
35-45 kwa tuhuma za ujambazi wa
kutumia silaha. Mtuhumiwa huyo
ameshiriki katika matukio mbalimbali ya
uvamizi wa vituo vya Polisi, na taasisi za
kibenki na kupora fedha pamoja na
mauaji.
Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa
mfanyakazi wa chuo cha JKU Zanzibar na
anapendelea kutembelea na kuishi
Zanzibar, Chanika, Mbagala, Mbande,
Kimara, Kitonga, Mwamdimkongo, Bupu,
Bagamoyo,Tanga, Kilwa, Ikwiriri, Rufiji na
Dondwe.
Amesema kuwa muonekano wa
mtuhumiwa huyo ni Maji ya kunde, urefu
wa wastani, kipara kidogo na anapendelea
kuvalia vazi la Kanzu na mavazi mengine
ya kawaida. Hivyo basi, natoa rai kwa
wananchi raia wema watoe taarifa za
uhakika za kukamatwa kwa mtuhumiwa
huyo kituo chochote cha Polisi.
Akizungumzia suala la Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
amesema walimkamata mbunge huyo Juni
29 mwaka huu na wamemhoji kutokana
na kutoa maneno ya uchochezi na kutoa
lugha za kashfa dhidi ya Rais Pombe
Magufuli ambayo aliyatoa baada ya
kutoka Mahakamani Kisutu juzi.
Tundulisu alikuwa akituhumiwa kwa kosa
la uchochezi na alikuwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
alipotoka alitoa maneno ya kumkashifu
Rais na maneno ya kichochezi sasa leo
(jana) tumempeleka Mahakamani kujibu
mashtaka hayo.chanzo michuzi blog.